Friday, January 8, 2016
Wednesday, January 6, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mashauriano
kuhusu mgogoro wa Burundi baina ya Tanzania, Angola, Uganda na Jumuiya ya
Afrika Mashariki
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameihakikishia dunia
leo kuwa mazungumzo ya kuleta amani nchini Burundi bado yanaendelea vizuri licha
ya taarifa zilizosambaa kuwa mazungumzo hayo yamegonga mwamba.
Dkt. Mahiga ameyasema hayo kwenye mkutano na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashauriano baina yake na Mhe. George
Pinto Chicoti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola na Mwenyekiti wa Baraza la
Mawaziri wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR); Mhe. Dkt. Crispus Kiyonga,
Waziri wa Ulinzi wa Uganda ambaye ni mwakilishi wa msuluhishi wa mgogoro wa
Burundi Rais Yoweri Kaguta Museveni, pamoja na Dkt. Richard Sezibera, Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 6 Januari 2016.
Akielezea madhumuni ya mashauriano hayo Dkt.
Mahiga alisema kuwa wadau hawa wanaunga mkono na kusifu jitihada zinazofanyika
ndani na nje ya Burundi zenye lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa
kisiasa na kiusalama nchini humo kwa njia ya majadiliano.
Aidha Waziri Mahiga alisema mazungumzo hayo
pia yanalenga kubadilishana ushauri, mawazo na kuandaa taarifa ya pamoja kabla
ya mikutano mikubwa ya kikanda; yaani ule wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu
(ICGLR Summit), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Summit) na Umoja wa Afrika (AU
Summit) inayotarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka huu.
Dkt. Mahiga alisema mazungumzo yao
yaliyojumuisha nchi za Tanzania, Angola na Uganda ambazo zimekasimiwa majukumu ya
uenyekiti na usuluhishi na jumuiya zao, yatatoa uelewa wa pamoja wa jinsi ya kuendesha
mashauriano ya kuleta amani ya kudumu kabla ya mikutano tarajiwa ambayo pamoja
na mambo mengine, itajadili pia suala la amani na usalama nchini Burundi.
“Naomba nirudie tena mbele yenu waandishi wa
habari kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya
uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli; kama wenyekiti wa jumuiya hii, bado
tuna nia ya dhati kabisa ya kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunapata suluhu ya
mgogoro huu, ambayo ni muhimu sana kwa usalama na maendeleo ya eneo letu na
bara la Afrika kwa ujumla” alisisitiza Dkt. Mahiga kabla ya kuanza mazungumzo
ya faragha na viongozi wenzake.
Waziri Dkt. Mahiga alipongeza jitihada za
wadau wengine na jumuiya ya kimataifa zinazoendelea ili kuhakikisha amani ya
kudumu inapatikana nchini humo.
MWISHO.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara
ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda
na Kimataifa.
06
Januari 2016
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Balozi wa India nchini
Balozi Arya naye akizungumza alipokutana na Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Kolimba |
Mkutano ukiendelea.
Picha na Reginald Philip.
|
Tuesday, January 5, 2016
Mhe. Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Song Geum-young Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.). |
Mhe. Rais akizungumza na Balozi Song Geum-young |
Balozi Song Geum-young akisaini Kitabu cha wageni alipowasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho |
Balozi Song Geum-young akiagana na kiongozi wa Bendi ya Polisi |
Mhe. Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa EU nchini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Roeland Van De Geer. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam
tarehe 05 Januari, 2016. |
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Roeland Van De Geer, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.). |
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga |
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha |
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Anthony Mtafya. |
Mhe. Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Roeland Van De Geer |
Mhe. Rais akizungumza na Balozi Roeland Van De Geer mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho |
Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Van De Geer, Mhe. Dkt. Kolimba, Msaidizi wa Rais masuala ya Diplomasia, Bi. Zuhura Bundala (wa kwanza kulia) pamoja na wajumbe kutoka Ubalozi wa EU. |
Balozi Roeland Van De Geer akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu |
Balozi Roeland Van De Geer akisikiliza wimbo wa taifa wa Tanzania na EU kutoka Bendi ya Polisi ikiwa ni kwa heshima yake |
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akiagana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi |
Mhe. Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Palestina nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Palestina hapa nchini, Mhe. Hazem Shabat. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Januari, 2016. |
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Shabat Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.). |
Mhe. Balozi Shabat akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bw. Batholomeo Jungu. |
Mhe. Rais Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Shabat |
Mhe. Rais Magufuli akiwa kwenye mazungumzo na Balozi Shabat mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho |
Mazungumzo yakiendelea |
Balozi Shabat akisaini Kitabu cha wageni alipowasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho |
Balozi Shabat (katikati) akisikiliza wimbo wa taifa lake ulipopigwa na Bendi ya Polisi kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Kushto kwake ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na kulia kwake ni Mnikulu. |
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana akifuatilia wimbo wa Taifa |
Balozi Shabat akiagana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi. |
Subscribe to:
Posts (Atom)