Thursday, February 4, 2016

Serikali ya Tanzania yalaani kudhalilishwa kwa mwanafunzi nchini India

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali juu ya kitendo cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania nchini India. Hatua hizo ni pamoja na kikao chake na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya ambapo Serikali ilimtaka Balozi huyo kufikisha ujumbe nchini kwake wa kuwahakikishia ulinzi raia wa Tanzania waliopo India na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo. Mkutano ulifanyika Wizarani tarehe 04 Februari, 2016
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo.


Sehemu nyingine ya Waandishi wa Habari
Mkutano ukiendelea
Wanahabari wakiwa kazini

==================================================

Serikali ya Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania na Kundi la watu katika jimbo la Bangalore nchini India.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi alipokutana na Wandishi wa Habari kwa ajili ya kuwaeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kitendo hicho cha kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Kitanzania nchini India.

Balozi Mwinyi alisema kuwa, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini India kuiandikia Serikali ya nchi hiyo kuomba maelezo kamili kuhusu tukio hilo pamoja na kuitaka Serikali ya India kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika pamoja na kuimarisha usalama katika maeneo wanayoishi wanafunzi wa Kitanzania.

Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa amemwita Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya na kumweleza masikitiko ya Serikali ya Tanzania kufuatia kitendo hicho cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania.

Katika mazungumzo yao, Balozi Arya alieleza bayana kuwa Serikali ya India imesikitishwa na tukio hilo la udhalilishaji na kwamba Serikali imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kutekeleza uovu huo.
 Alisema kuwa Waziri Mkuu wa Jimbo la Bangalore aliongea na umma kuelezea masikitiko yake kuhusu uovu huo na kuahidi kuwa mamlaka za jimbo hilo zitaimarisha usalama katika maeneo yote wanayoishi wanafunzi wa Tanzania na raia wengine kutoka nje.

Balozi Arya aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa India inaheshimu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, hivyo itashughulikia suala hilo kwa ukamilifu na hadi wakati huu tayari watu watano wanashikiliwa na vyombo vya usalama wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Sanjari na taarifa hiyo, Balozi Mwinyi aliwaomba Watanzania kutohusisha tukio hili la uhalifu na ajali ya Mtanzania, Bw. Christian Benjamin Mlyansi iliyotokea nchini India jana usiku na kusababisha kifo chake. Alisema kuwa Bw. Mlyansi alipata ajali ya kawaida alipokuwa anaendesha pikipiki ambapo ilipoteza mwelekeo na kugonga ukingo wa kati wa barabara. 

-Mwisho-







Balozi Mwinyi akutana na Katibu Mtendaji wa ALAT

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (Association of Local Authorities of Tanzania-ALAT), Bw. Abraham Shamumoyo. Katika mazungumzo hayo, Bw. Shamumoyo alitoa taarifa fupi kuhusu muundo na utendaji kazi wa ALAT. Aidha, Bw. Shamumoyo alitoa taarifa za awali kuwa Jumuiya hiyo kwa upande wa Kanda ya Mashariki mwa Afrika inakusudia kutuma maombi Serikalini ili makao makuu yake yawe Tanzania.
Mazungumzo yakiaendelea, wengine katika picha, kutoka kulia ni Bw. Elisha Suku na Balozi Baraka Luvanda ambao ni maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje. Pembeni kwa Bw. Shamumoyo ni maafisa wa ALAT.

Wednesday, February 3, 2016

Dkt. Mahiga aapa kuwa Mbunge

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt.  Augustine Mahiga akiapa  Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016.


Monday, February 1, 2016

Kampuni Binafsi za Tanzania zashiriki Maenesho ya Utalii nchini Uholanzi


Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiwa katika ya pamoja na Bi. Selma Kamm-Melai (kulia) na Bw. Yohannes Ngomi- Kamm (wa pili kutoka kulia) Wawakilishi wa Kampuni ya Utalii ya MAKASA SAFARIS iliyopo Moshi, Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Utalii ya Holiday Fair 2016 (Vakatiebeurs 2016) yaliyofanyika hivi karibuni mjini Utrecht.  Kushoto ni Bi. Agnes Kiama Tengia, Afisa Ubalozi.

Baadhi ya Makampuni binafsi ya Utalii nchini Tanzania yalishiriki katika Maonesho hayo maarufu yanayofanyika kila mwaka katika miji ya Amsterdam, Utrecht na Maastricht, Uholanzi ambapo huvutia maelfu ya washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani. Maonesho ya Vakantiebeurs hutoa fursa kwa nchi kujitangaza hususan katika sekta ya utalii. Ubalozi wa Tanzania ulihudhuria Maonesho hayo na kukutana na Wawakilishi wa baadhi ya Makampuni hayo binafsi kutoka Tanzania.


Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Kassim Abdallah, Mwakilishi wa Kampuni ya BOBBY TOURS kutoka Arusha Tanzania aliyeshiriki katika Maonesho ya Vakantiebeurs 2016 yaliyofanyika katika miji ya Amsterdam na Utrecht, Uholanzi hivi karibuni. Kutoka kulia ni Bi. Flora Williams, Bw. Peter Mihyona Bi. Agnes K. Tengia.


Mhe. Balozi Irene F.Kasyanju akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya KILIDOVE ya Arusha, Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Vakatiebeurs 2016 yaliyofanyika mjini Utrecht hivi karibuni.

Thursday, January 28, 2016

Naibu Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Comoro nchini

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Comoro nchini, Mhe. Ahmed El Badaoui Mohamed Fakih. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Comoro.  
Maafisa wa Ubalozi wa Commoro nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Fakih na Balozi Muombwa (hawapo pichani), wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Balozi Bw. Bacar Salim na kulia ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi huo Bw. Failladhu Mbae Charif.
Balozi Fakih naye akimwelezea jambo Balozi Muombwa (Kulia) wakati wa mazungumzo yao.

Picha na Reginald Philip



Wednesday, January 27, 2016

India marks 67th years of Independence

Permanent Secretary for the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dr. Aziz Ponary Mlima addresses distinguished invited guests including members of the Diplomatic Community, Government Officials and representatives from private sector during the celebration to mark 67 years of India Independence. In his speech, Dr. Mlima insisted the importance of Tanzania and India to deepen and strengthen diplomatic and economic cooperation with a focus on increasing investment and trade volumes.The celebrations was hosted by the Indian High Commission in Dar es Salaam.  
Indian High Commissioner, H.E Sandeep Arya delivers his speech in the celebration of the 67th Anniversary of the Independence of India. The event took place at Hyatt Regency, Kilimanjaro Hotel in Dar Es Salaam yesterday.
Deputy Permanent Secretary for the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Ramadhani Mwinyi Muombwa (second left) was among the senior government officials who attended the ceremonies.
Permanent Secretary (R) and Indian High Commissioner toasting for the progress and prosperity of their Nations.
Former President of the United Republic of Tanzania, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (with a red tie) was also present at the ceremonies. On his left is the former Prime Minister of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Salim Ahmed Salim.
Indian High Commissioner (L) receives invited guests at the ceremonies hall.


Permanent Secretary, Dr. Mlima (R) chats with ambassadors prior to the official opening of an event.

Tuesday, January 26, 2016

Dkt. Mlima akutana na Katibu Mkuu wa EAC

Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera (kushoto) akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Aziz P. Mlima. Dkt. Sezibera alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa madhumuni ya kusalimia pamoja na kutoa taarifa fupi ya masuala mbalimbali yanayoendelea katika Jumuiya.
Kutoka kushoto ni Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao ni Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Stephen Mbundi; Mhandisi John Kiswaga; Bw. Amos Tengu na Bw. Antony Ishengoma wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.