Rais
Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika
wa Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya amewasili jijini Tunis nchini
Tunisia kushiriki Mkutano wa nane wa nchi Jirani ya Libya. Mkutano huo
ulioitishwa na Serikali ya Tunisia ni muendelezo wa jitihada za nchi
jirani kusaidia kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya. Rais
Mstaafu amewasili Tunis akitokea Salalah nchini Oman aliposhiriki
Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.
Akiwa
jijini Tunis, Rais Mstaafu Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri
wa Masuala ya Maghreb, Arab na Afrika wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader
Messaleh aliyemtembelea hotelini kwake. Katika mazungumzo yao, Waziri
Messaleh alimpongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa
Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya ambapo alimuelezea hali
ya usalama na kisisa ya Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora
ya utatuzi wa mgogoro huo.Mheshimiwa Abdelkader
Messaleh Alimhakikishia Rais Mstaafu ushirikiano wa
Serikali ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa
Afrika.
Kwa
upande wake, Rais Mstaafu Kikwete alimshukuru Waziri Abdelkader
Messaleh kwa maelezo aliyompatia na ushirikiano aliomuahidi na kumuelezea
matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo madhali nchi
jirani na Libya na Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote
kuhakikisha mgogoro huo unatatulika ambapo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alisisitiza kuwa hatimaye suluhu ya
kudumu ya mgogoro wa Libya uko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje ya Oman Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah mjini Salalah, Oman kuzungumzia mgogoro wa Libya. Katika mkutano wao wamebadilishana mawazo juu ya suluhisho la kudumu la hali ya siasa, usalama na amani nchini Libya.
Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu. Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.
Picha ya pamoja.
=====================
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje ya Oman Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah mjini Salalah, Oman kuzungumzia mgogoro wa Libya. Katika mkutano wao wamebadilishana mawazo juu ya suluhisho la kudumu la hali ya siasa, usalama na amani nchini Libya.
Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu. Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.
Picha ya pamoja.
=====================
Katika
ziara yake nchini Tunisia, mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa nchi
Jirani na Libya, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa pia kukutana
na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Libya
(Presidency Council) Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj, wadau wengine wa
Libya pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa Libya
iliyoko jijini Tunis. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea
nchini tarehe 25 Machi, 2016.
Rais
Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwakilishi Maalum
wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki
Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya
Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman.
Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,
Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
Katika
Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa
Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu na
Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya
hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao ikiwa ni pamoja na
dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa
wajumbe hao kuwapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za
Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.
Rais
Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta
suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya
(Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko
Shkirat, Morocco na kuwahimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya
kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa
kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema
iwezekanavyo.
Mwakilishi
huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa
Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme
za Kiarabu (Arab League) na wadau wengine wote kusaidia jitihada za
wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini
Libya.
MWISHO.