Tuesday, August 2, 2016

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Japan nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo Mhe. Waziri alieleza mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi ya ushirikiano na Serikali ya Japan hususan miradi ya miundombinu na Sekta ya Elimu. 
Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida akieleza nia ya Serikali ya Japan katika kuimarisha ushirikiano hususan katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu unaenda sambamba na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Bertha Makilagi (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea

Monday, August 1, 2016

Waziri Mahiga akutana na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Kaimu Balozi wa Oman nchini, Bw. Mohammed Sulaiman Alrawahi. Mazungumzo yao ambayo yalijikita zaidi katika masuala ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2016. 
Mazungumzo yakiendelea
=========================================

...Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Italia nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Kushoto) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe.Roberto Mengon ambaye alimtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Roberto kwa mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolea na Serikali ya Italia katika kusaidia Sekta ya Elimu, miundombinu na afya kwamba Tanzania itazidi kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo.
Mhe. Robert katika mazungumzo yake alieleza kuwa amefurahishwa sana na hali ya amani iliyopo nchini Tanzania kwa kuwa wananchi wa makabila na imani tofauti wameweza kuchanganyika na kuishi pamoja na kutumia lugha moja ya Kiswahili na kwamba ni mfano unaotakiwa kuigwa na mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo, Kanda ya Afrika Mashariki ya Italia iliyopo Nairobi, Kenya Bi. Teresa Savanella ambaye alifuatana na Mhe. Roberto akieleza namna ambavyo Taasisi hiyo ambayo inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Ufundi inavyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana wa Afrika Mashariki kupata elimu ya ufundi kwa ajili ya kujiajiri. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Italia nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Antony Mtafya wakifuatilia mazungumzo.
Picha ya pamoja

===========================================

...Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga  na Naibu Meya wa Bermuda 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Meya wa Mji wa Hamilton nchini Bermuda, Mhe. Donal Smith kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri alieleza nia ya Serikali  ya Tanzania katika kushirikiana na wawekezaji mbalimbali wanaotaka kuja  nchini hususan katika miradi ambayo ina tija kwa Taifa na ambayo itatoa ajira kwa Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya  Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016
Mhe. Donal nae akimweleza Mhe. Waziri Mahiga kuhusu lengo la ziara yake nchini kuwa ni kuitambulisha Kampuni ya Nelson & Pade inayojishughulisha na kilimo cha kisasa cha mbogamboga na ufugaji wa samaki inayotaka kuja kuwekeza nchini. Pia alimweleza nia ya nchi yake ya kuja kuwekeza kwenye uchimbaji wa mawe aina ya lime (limestone) na matumizi yake katika ujenzi wa kisasa pamoja na kuleta wawekezaji  katika viwanda vya kutengeneza madawa ya binadamu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha wakifuatilia mazungumzo.
Mhe. Waziri Mahiga akiangalia moja ya miradi ya kilimo inayofanywa na Kampuni ya Nelson & Pade
Mazungumzo yakiendelea

Friday, July 29, 2016

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa DRC nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba, alipomtembelea Wizarani Jijiji Dar es Salaam. Katika Mazungumzo yao Mhe Waziri alieleza Serikali ya Tanzania inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha wafanyabiashara kutoka nchini Congo hawapati shida katika kusafirisha bidhaa zao kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Mhe. Mutamba akizungumza ambapo alieleza umuhimu wa kufanyika vikao vya Tume ya Pamoja kati ya Tanzania na DRC, pamoja na kuweka makubaliano yatakayowezesha wafanyabiashara kunufaika na kuweza kukuza uchumi wa mataifa yao badala ya kuwa na tozo nyingi zinazorudisha nyuma biashara zao.
Wakati mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga akiagana na Mhe. Balozi Mutamba

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Saharawi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Balozi wa Saharawi nchini Mhe. Brahim Salem Buseif alipomtembea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo tarehe 29 Julai, 2016
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Buseif, ambapo katika mazumgumzo yao alimpa pole kwa  msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Polisario cha nchini Saharawi. Pia alisisitiza kuwa mataifa haya mawili yataendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali.
Mhe. Buseif akizungumza ambapo alieleza kuwa nchi ya Saharawi ipo tayari kushirikiana na Tanzania na kuishukuru kwa kuiunga mkono katika masuala mbalimbali.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea.

Mtanzania atunukiwa Tuzo ya Juu ya Malkia wa Thailand

Profesa Pauline Peter Mella aliyetunukiwa Tuzo ya Juu ya Malkia wa Thailand Srinagarindra kwa kutambua mchango wake kwenye sekta ya afya, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyoandaliwa na Ubalozi wa Thailand nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Tuzo hiyo inatolewa  na Malkia wa Thailand Srinagarindra kwa kutambua mchango wa watu mbalimbali kwenye sekta ya afya. Profesa Mela ambaye kitaaluma ni Muuguzi kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha masuala ya Tiba cha Hubert Kairuki cha Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Profesa Pauline Peter Mella hayupo pichani. Wa pili kutoka kulia ni Balozi Mteule wa Thailand nchini, Mhe. Prasittiporn Wetprasit
Profesa Pauline Peter Mella akiwa ameshikilia Tuzo yake kwenye picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake nchini Nairobi Mhe. Prasittiporn Wetprasit na familia yake.

Profesa Mella akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi Wateule nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Italia hapa nchini, Mhe. Roberto Mengon. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule wa Italia hapa nchini mara baada ya kupokea Nakala zake za utambulisho. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine akifuatiwa na  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana .

...Nakala za Hati za Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), pia akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Watu wa Korea (DPRK) hapa nchini, Balozi Kim Yong Su hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam hivi karibuni

...Nakala za Utambulisho za Balozi wa Thailand

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake nchini Nairobi Balozi Prasittiporn Wetprasit (kushoto) leo katika Ofisi yake jijini Dar es Salaam
Waziri Mahiga akimweleza jambo Balozi Mteule, Mhe. Wetprasit mara baada ya kupokea nakala zake za utambulisho.

...Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi wa Somalia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akiisoma Nakala ya Hati ya  Utambulisho  ya a Balozi Mpya wa Jamhuri ya Somalia hapa nchini Balozi Mteule wa Somalia nchini, Mhe. Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuipokea. Tukio hilo lilifanyika Wizarani hivi karibuni.
Dkt. Mahiga akizungumza na Balozi Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kupokea nakala zake
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Hassan Abdi

Waziri Mahiga ashiriki hafla ya kuwaaga Mabalozi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akizungumza kwenye hafla  ya kuwaaga Mabalozi wa nchi za Ireland, Canada na Uingereza wanaomaliza muda wao wa uwakilishi nchini. Kutoka kushoto ni  Mhe. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland, Mhe. Alexandre Leveque, Balozi wa Canda na Mhe. Dianna Melrose, Balozi wa Uingereza. Katika mazungumzo hayo Dkt. Mahiga aliwashukuru kwa kuendeleza na kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Mataifa yao hapa nchini hususan katika kuchangia miradi mbalimbali ya  maendeleo. 
Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza.
Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine akitoa neno la shukrani. 
Waziri Mahiga akimkabidhi picha yenye mchoro wa ndege zilizochorwa kwa ustadi wa hali ya juu
Balozi wa Canada akipokea zawadi
Balozi Melrose naye akipokea zawadi yake
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi  hao
Picha ya pamoja

Thursday, July 28, 2016

Waziri Mahiga aagana na Mabalozi waliomaliza muda wa kazi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Dianna Melrose alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
 Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimpongeza Balozi Melrose kwa kuiwakilisha nchini yake vema na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Uingereza. Kwa upande wa Balozi Melrose, alisema anaishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa anaupata kipindi chote cha uwakilishi wake.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.
Mazungumzo yakiendelea

=====================================

Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza  na Balozi wa Canada nchini, Mhe Alexandre Leveque alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu na Biashara. Pia Mhe . Alexandre Leveque alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara kwa ushirikiano katika kipindi chake chote cha uwakilishi hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Lilian Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Balozi Mahiga akiagana na Balozi Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo

=========================================

 .... Mazungumzo na Balozi wa Ireland hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan alipokuja Wizarani kuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland katika sekta mbalimbali. Kwa upande wa Mhe. Gilsenan alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano.