Wednesday, August 10, 2016

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu wa China

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Zhaoxing ambaye ameongoza ujumbe kutoka Taasisi ya Diplomasia ya Umma ya China. Ujumbe huo upo nchini kwa ajili ya kuhamasisha  ushirikiano katika masuala ya Habari na Mawasiliano hususan kupitia vyombo vya habari ambavyo ni msingi katika kueleimisha umma masuala mbalimbali ya maendeleo.
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Mhe. Zhaoxing ukifuatilia mazungumzo kati yake na Mhe. Waziri Mahiga
Sehemu nyingine ya ujumbe kutoka China.
Mhe. Zhaoxing naye akimweleza jambo Mhe. Waziri Mahiga
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Halmenshi Lunyumbu wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Zhaoxing (hawapo pichani).
Waziri Mahiga akimkabidhi zawadi ya Kahawa na Majani ya Chai yanayozalishwa nchini 
Waziri Mahiga na Mhe. Zhaoxing na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano wakiwa katika picha ya pamoja. 

Thursday, August 4, 2016

Waziri Mahiga akutana na Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill na Melinda ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mwakilishi kutoka Taasisi ya Bill na Belinda Gates ya Marekani, Bi. Rosita Najmi. Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimweleza Bi. Najmi kuwa Tanzania inathamini mchango unaotolewa na Taasisi ya Bill na Melinda katika miradi mbalimbali  ikiwemo kuboresha sekta ya afya na kilimo kwa maendeleo ya Taifa.
 Bi. Rosita  akimwelezea namna Taasisi hiyo ilivyojipanga kuendelea kushirikiana na Tanzania.
Bw. John Ndunguru, Afisa wa Program kutoka Taasisi ya Bill na Melinda naye akichangia jambo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) akiwa na  Bi. Ramla Hamis (katikati) na Bi. Prisca Mwanjesa, Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia  mazungumzo ya Dkt. Mahiga na Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill na Belinda Gates (hawapo pichani).
Mazungumzo yakiendelea
Picha ya pamoja .

Waziri Mahiga apokea Nakala za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ireland nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ireland nchini, Mhe.Paul Sherlock. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es salaam tarehe 04 Agosti, 2016
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza ambapo alimkaribisha Mhe. Balozi Sherlock na kumweleza kuwa Tanzania na Ireland zimekuwa zikishirikiana vizuri tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kidiplomasia baina yao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Balozi huyo katika muda wake wote wa uwakilishi hapa nchini.



Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha walishiriki makabidhiano hayo.
 Mazungumzo yakiendelea

Wednesday, August 3, 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Asia akutana na Balozi wa China nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Astralasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Dkt. Lu Younqing alipomtembelea Wizarani jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika kujadili masuala ya ushirikiano, maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya ushirikiano baina ya Tanzania na China, pamoja na mipango ya uwekezaji inayotarajiwa kufanywa na Serikali ya China nchini.
wakati mazungumzo yakiendelea. 
Picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.

Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati akutana na Balozi wa Kuwait nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima (kulia), akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jaseem Al Najem. Balozi huyo alifika Wizarani  kwa ajili ya kuishukuru kwa ushirikiano alioupata wakati wa zoezi la kukabidhi madawati yaliyotolewa na Ubalozi huo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa tukio lililofanyika hivi karibuni katika Shule ya Msingi ya Chamazi Jijini Dar es Salaam.   
Balozi Kilima akiwa katika mazungumzo na Balozi Al-Najem. Kulia kwa Balozi Kilima ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Tahir

Kaimu Katibu Mkuu azungumza na Wataalam Elekezi kuhusu ushirikiano na Washirika wa Maendeleo


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Mtaalam Mwelekezi kuhusu masuala ya Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo, Dkt. James Adams alipotembelea Wizarani na ujumbe wake kwa ajili ya kupata maoni mbalimbali ya namna bora ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wake wa Maendeleo. Dkt. Adams aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia na Mkurugenzi wa Benki hiyo hapa nchini.

Dkt. Adams nae akieleza jambo kwa Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy naye akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Kaimu Katibu Mkuu na Dkt. Adams (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizarani, Bw. James Lugaganya (katikati) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu.
Bw. Lugaganya akichangia hoja
Ujumbe uliofuatana na Dkt. Adams nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Bw. Steve Kayizzi-Mugerwa na Bw.Mugisha Kamugisha.

Tuesday, August 2, 2016

Waziri Mahiga ampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia  maendeleo ya nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa  hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016.
Waziri Mahiga akizungumza huku Mhe. Waziri Ayrault akimsikiliza.
Wajumbe waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Mahiga alipotembelea Wizarani leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga na mgeni wake Waziri Ayrault wakiwa katika picha ya pamoja.
Waziri Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Ayrault mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Japan nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo Mhe. Waziri alieleza mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi ya ushirikiano na Serikali ya Japan hususan miradi ya miundombinu na Sekta ya Elimu. 
Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida akieleza nia ya Serikali ya Japan katika kuimarisha ushirikiano hususan katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu unaenda sambamba na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Bertha Makilagi (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea

Monday, August 1, 2016

Waziri Mahiga akutana na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Kaimu Balozi wa Oman nchini, Bw. Mohammed Sulaiman Alrawahi. Mazungumzo yao ambayo yalijikita zaidi katika masuala ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2016. 
Mazungumzo yakiendelea
=========================================

...Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Italia nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Kushoto) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe.Roberto Mengon ambaye alimtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Roberto kwa mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolea na Serikali ya Italia katika kusaidia Sekta ya Elimu, miundombinu na afya kwamba Tanzania itazidi kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo.
Mhe. Robert katika mazungumzo yake alieleza kuwa amefurahishwa sana na hali ya amani iliyopo nchini Tanzania kwa kuwa wananchi wa makabila na imani tofauti wameweza kuchanganyika na kuishi pamoja na kutumia lugha moja ya Kiswahili na kwamba ni mfano unaotakiwa kuigwa na mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo, Kanda ya Afrika Mashariki ya Italia iliyopo Nairobi, Kenya Bi. Teresa Savanella ambaye alifuatana na Mhe. Roberto akieleza namna ambavyo Taasisi hiyo ambayo inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Ufundi inavyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana wa Afrika Mashariki kupata elimu ya ufundi kwa ajili ya kujiajiri. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Italia nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Antony Mtafya wakifuatilia mazungumzo.
Picha ya pamoja

===========================================

...Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga  na Naibu Meya wa Bermuda 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Meya wa Mji wa Hamilton nchini Bermuda, Mhe. Donal Smith kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri alieleza nia ya Serikali  ya Tanzania katika kushirikiana na wawekezaji mbalimbali wanaotaka kuja  nchini hususan katika miradi ambayo ina tija kwa Taifa na ambayo itatoa ajira kwa Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya  Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016
Mhe. Donal nae akimweleza Mhe. Waziri Mahiga kuhusu lengo la ziara yake nchini kuwa ni kuitambulisha Kampuni ya Nelson & Pade inayojishughulisha na kilimo cha kisasa cha mbogamboga na ufugaji wa samaki inayotaka kuja kuwekeza nchini. Pia alimweleza nia ya nchi yake ya kuja kuwekeza kwenye uchimbaji wa mawe aina ya lime (limestone) na matumizi yake katika ujenzi wa kisasa pamoja na kuleta wawekezaji  katika viwanda vya kutengeneza madawa ya binadamu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha wakifuatilia mazungumzo.
Mhe. Waziri Mahiga akiangalia moja ya miradi ya kilimo inayofanywa na Kampuni ya Nelson & Pade
Mazungumzo yakiendelea