Friday, August 19, 2016

Waziri Mahiga akutana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Japan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Balozi Junzo Fijita aliyetembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Agosti, 2016.
Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida  (kushoto) pamoja na Afisa aliyefuatana naye wakifuatilia mazungumzo.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea
Wakiagana mara baada ya mazungumzo

Wanawake wa Mambo ya Nje wamuaga Balozi Mulamula

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akiongea na Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki katika kikao cha kumuaga Balozi Liberata Mulamula, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Balozi Mulamula ambaye amestaafu utumishi wa umma alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza  Wizara ya Mambo ya Nje pia mlezi wa Umoja wa Wanawake wa Wizara hiyo (Nje Women). Mhe. Naibu Waziri alimshukuru Balozi Mulamula kwa kuimarisha umoja wa wanawake wa Wizara na kuahidi kuendelea kuenzi mchango wake kwenye umoja huo.
Balozi Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe (hawapo pichani) ambapo aliwaasa kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa bidii huku wakizingatia weledi ili kuwa mfano bora kazini, kwenye familia na taifa kwa ujumla.
Balozi Mulamula akimkabidhi Naibu Waziri, Mhe. Kolimba mwongozo wa Umoja huo baada ya kuchaguliwa kuwa Mlezi mpya.
Sehemu ya Watumishi wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia kikao.
Sehemu nyingine ya Watumishi hao wakifuatilia kikao
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi. Amisa Mwakawago akitoa taarifa fupi ya Umoja kwa mama mlezi mteule na kwa Wajumbe wengine walioshiriki kikao. Kulia ni Katibu wake, Bi. AnnaGrace Rwalanda.
Dkt. Kolimba akimkabidhi zawadi Balozi Mulamula. 
Bibi. Mwakawago akimkabidhi Balozi Mulamula zawadi ya picha yake ya kuchorwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawsiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni mjumbe wa Umoja wa Wanawake (Nje Women) akitoa neno la shukrani kwa Balozi Mulamula.
Kikao kikiendelea
Picha ya Pamoja ya walezi na uongozi wa Nje Women

Picha ya pamoja.


Mkutano wa tano wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuanza Arusha

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
 


Simu: 255-22 211906-12, 2126827  

Fax: +255-22 2116600, 2120488/2126651
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Tovuti: www.foreign.go.tz/ www.meac.go.tz


                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
            11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa tano wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuanza  Arusha
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) linatarajia kuanza vikao vyake mapema wiki ijayo Jijini Arusha, Tanzania, kwa muda wa wiki mbili kuanzia Jumatatu Agosti 22, 2016 hadi Ijumaa Agosti 2, 2016.

Pamoja na mambo mengine Bunge hilo linatarajia kujadili ripoti ya ukaguzi wa hesabu kutoka Kamati ya Fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2015. Ripoti hiyo inayozingatia na kuonyesha taarifa za ukaguzi wa hesabu za fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2015, inahusisha taasisi na vyombo mbalimbali vilivyopo chini ya Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Miradi 20 inayotelezwa na kusimamiwa na Sekretariati, kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 134 ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tume ya ukaguzi iliwasilisha ripoti yake kwenye Baraza la Mawaziri na kujadiliwa na Baraza hilo Mei 24, 2016. Ripoti hii ya tume ya ukaguzi inayoonesha kuwa bajeti imetekelezwa kwa 65% inajadiliwa kipindi ambacho Jumuiya inapitia kipindi kigumu cha ukosefu wa fedha.
Pia Bunge linatarajia kujadili ripoti ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili kuhusu uangalizi wa shughuli za Utalii katika Jumuiya. Vilevile Bunge litajadili ripoti nyingine ya kamati ya Kilimo, Utalii na Biashara ambapo itaangazia hali ya ujangili ndani ya JumuiyaKama sehemu ya kudumisha ushirikiano na wadau wengine kwenye kanda, EALA itapokea ripoti kuhusu masuala ya vijana ndani ya Jumuiya kufuatia matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika la Afrika Mashariki (The East African Institute) chini ya uangalizi wa Shirika la Mtandao wa Maendeleo la Aga Khan (Aga Khan Development Network)
Vikao vya EALA vinafanyika kwa utaratibu wa mzunguko miongoni mwa Nchi Wanachama kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakati huohuo Bunge linafanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali sambamba na kupokea taarifa kuhusu Bunge hilo. Bunge hilo linatarajiwa kuongozwa na Spika wake Mhe. Daniel Kadega.

Mwisho
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 26 Mei 2016.




Thursday, August 18, 2016

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa China nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Agosti, 2016. Mazungumzo yao yalijikita katika kujadili masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na China na taratibu zinazoendelea kwa upande Serikali za kuhamia Dodoma. 
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Mbelwa Kairuki pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Halmenshi Lunyumbu wakifuatilia mazungumzo. 
Mazungumzo yakiendelea

Wakiwa katika  picha ya pamoja

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Israel nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Agosti, 2016. Katika mazumgumzo yao walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa yao hususan katika sekta za Kilimo, Elimu na Masuala ya kuwawezesha Wanawake katika kufikia maendeleo.
Mhe. Yahel akimweleza Waziri Mahiga namna Serikali ya Israel ilivyofanikiwa katika miradi ya kilimo na umwagiliaji ambayo imesaidia katika kuwahakikishia wananchi wake upatikanaji wa chakula.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto) pamoja na Maafisa  Mambo ya Nje  Bw. Hangi Mgaka (wa pili kushoto) na Bi. Kisa Doris Mwaseba wakifuatilia mazungumzo
Mazungumzo yakiendelea
Wakijadili jambo mara baada ya mazungumzo

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya SMH RAIL ya Malaysia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Aziz Mlima (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Masoko wa SMH RAIL Bw. S. Rajamohan ya Malaysia alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao walijadili kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususan katika miundombinu ya reli.
Bw. S. Rajamohan akielezea namna kampuni ya SMH RAIL inavyofanya shughuli zake na utayari wao wa kuja kuwekeza nchini.
Mazungumzo yakiendelea



Wednesday, August 17, 2016

Waziri Mahiga apokea hati za utambulisho za Mwakilishi mpya wa WFP nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi mpya wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) hapa nchini, Bw. Michael Dunford. Hafla hiyo fupi ilifanyika Wizarani tarehe 17 Agosti, 2016.
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Bw. Dunford mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Bw. Dunford nae akimweleza jambo Mhe. Waziri
Mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Bw. Dunford yakiendelea. Wengine katika picha ni Bi. Eva Ng'itu (kushoto) na Bi. Sekela Mwambegele, Maafisa Mambo ya Nje.

Tuesday, August 16, 2016

WAHESHIMIWA MABALOZI WAJITOKEZA KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO

Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland Nchini Bw. Simo-Pekla Perviainen (aliyeketi) akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Jamhuri ya Msumbiji Nchini Mhe. Monica Patricio Clement Mussa akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam
Kaimu Balozi wa Burundi Nchini Bw. Prefere Ndayishimiye akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Ubalozi wa Angola Nchini Bw. Joel Cumbo akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam
Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Sudan Bw. Abuzied Shamseldin  Ahmed akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Cuba Nchini Mhe. Jorge Luis Tormo akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam

Waziri Mahiga aomboleza kifo cha Hayati Aboud Jumbe Mwinyi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi kilichotokea tarehe 14 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam. Mhe. Mahiga alisaini kitabu hicho  aliposhiriki mazishi ya Hayati Alhaji Aboud Jumbe yaliyofanyika Zanzibar tarehe 15 Agosti, 2016.

Friday, August 12, 2016

Waziri Mahiga azungumza na Waandishi wa Habari


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  kuhusu  Mkutano wa 18 wa  Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama  ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC  uliofanyika Maputo, Msumbiji kuanzia tarehe 1-5 Agosti, 2016. Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulizungumzia hali ya usalama na amani katika nchi za Lesotho, DRC na Madagascar.
Mhe. Waziri Mahiga akiwaeleza waandishi kuhusu 
Kitabu cha Harakati za Ukombozi katika Nchi za Kusini mwa Afrika ambacho kimepewa jina la Hashim Mbita  kufuatia mchango Mkubwa wa Hayati Brigedia Jenerali (Mstaafu) Balozi Hashimu Mbita katika harakati za ukombozi na uandishi wa kitabu hicho.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga.
 Mkutano huo ukiendelea

Thursday, August 11, 2016

BALOZI HAULE AAGWA NAIROBI

Mhe. Haule akiongea wakati wa hafla ya kumuaga jana. Kushoto ni mkewe Mary.
Mhe. Balozi Haule (aliyeketi katikati) katika picha ya pamoja na Maofisa Ubalozi. Kushoto ni  Mama Mary Haule na Kulia ni Mkuu wa Utawala Ubalozini, Bi. Talha Waziri.
Mwakilishi wa Watanzania waishio Kenya, Bw. Victor Matemba akitoa salamu zao kwa Mhe. Haule.

Mhe. Haule na mkewe katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wanaotoka Kenya (Local staff).

Wednesday, August 10, 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atembelea Kiwanda cha kushona nguo cha Tooku

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agosti 10, 2016.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Adelhem Meru na wapili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.


Mfano wa suruali ya Jeans zinazotengenezwa na kiwanda hicho zikiwa na utambulisho wa kutengenezwa nchini Tanzania. Hivi sasa kiwanda kimeanzisha programu ya kutoa mafunzo kwa vijana 400 kila mwezi katika miezi 12 na ifikapo mwisho wa mwaka jumla ya watanzania 6000 watakuwa wameajiriwa. 
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agosti 10, 2016.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Adelhem Meru na wapili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam  Agost 10, 2016 .  Kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing na kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kutembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kushona nguo cha  Tooku kilichopo eneo la EPZ,Mabibo External jijini Dar es salaam baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza, Agosti 10,2016.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhem Meru na kulia kwake ni Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing.