Friday, September 15, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb) katikati, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Aziz Mlima (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiaono wa Afrika Mashariki.
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mahiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani), wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango Joachim Otaru pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Rodney Tadeusi (katikati).
Sehemu ya wahariri wa vyombo vya habari wakinukuu maswala mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kuzungumzwa na Dkt. Mahiga.
Juu na Chini Mkutano ukiendelea

Tuesday, September 12, 2017

Katibu Mkuu Mtendaji wa ICGLR atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Aziz Mlima (kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) Balozi Zackaria  Muburi Muita, ambapo walizungumzia  masuala mbalimbali yanayoendelea katika jumuiya hiyo.
Mkutano ukiendelea
Dkt. Mlima pamoja na Balozi Muita wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Monday, September 11, 2017

Joint Communique of the bilateral trade meeting between the United Republic of Tanzania and the Republic of Kenya held on 06TH – 08TH September, 2017,at Mwalimu Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es salaam



JOINT COMMUNIQUE OF THE BILATERAL TRADE MEETING TO ADDRESS TRADE-RELATED CONCERNS BETWEEN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE REPUBLIC OF KENYA
HELD ON 06TH – 08TH SEPTEMBER, 2017 AT MWALIMU JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE IN DAR ES SALAAM

1.        As agreed during the bilateral meeting between Tanzania and Kenya held in Namanga on 03rd August 2017, a bilateral technical meeting to address trade-related concerns between the two countries was convened on 06th- 08th September 2017 in Dar es Salaam.

2.        The meeting was co-chaired by Prof. Adolf Mkenda, Permanent Secretary of the Ministry of Industry, Trade and Investment of the United Republic of Tanzania, and Dr. Chris Kiptoo, Principal Secretary in the Ministry of Industry, Trade and Cooperatives of the Republic of Kenya.

3.        During the meeting, which was held in a friendly and cordial atmosphere, the two sides noted the impetus to enhance and ease bilateral trade between the two countries that has been given by the two Heads of State, His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania and His Excellency Uhuru Muigai Kenyatta, President of the Republic of Kenya.

4.        The two sides underscored the significance of having regular bilateral meetings to discuss concerns and opportunities with a view of promoting trade in the two countries for the mutual benefit of the two countries and its people.

5.        During the meeting, the two sides deliberated on inter-alia, concerns related to the retail sector, customs, freight forwarding, market access, administrative bottlenecks, and implementation of the relevant East African Community directives. In this regard, the two sides called for the effective and timely implementation of the agreements reached in the bilateral meeting with a view to ease the flow of goods and services.

  1. Overall, the meeting noted with satisfaction the smooth conduct and flow of trade between the two countries, and that the Presidential Directives regarding the free flow of LPG, wheat flour, milk and milk product have been implemented. Among other things, the two sides agreed to the following:

·           The Management of Uchumi and Nakumatt Supermarkets should work with their suppliers to come up with a roadmap on how to settle the outstanding payments, and policy measures should be instituted to ensure that the retail sectors do not face a recurrence of similar challenges;
·           To implement the SCT system to speed up clearance of goods, and in particular perishable goods;
·           To speed up the development and adoption of regional cargo tracking system;
·           To encourage the Chiefs of Immigration Services in the two countries to convene a meeting to resolve immigration issues between the two countries;
·           To conduct verification exercise on lubricants, edible oils, cement and textiles produced outside EPZs in order to ascertain the origin of the product, and fair competition issues on textiles in particular; and,
·           To ratify and implement EAC SPS Protocol, which requires EAC Partner State to establish regulatory institutions and harmonize SPS control measures. KEBS and TFDA to cooperate on harmonization of SPS measures.

7.        In addition, a sideline meeting for wheat farmers and millers from Tanzania and Kenya was held on the margins of the bilateral meeting, and was equally co-chaired by Prof. Mkenda and Dr. Kiptoo. The meeting brought together key wheat stakeholders from the two countries to jointly discuss measures to support wheat farming in both countries. The meeting agreed to prioritize wheat produced locally in order to support the farmers. Thus, while the Namanga agreement stands Millers have agreed to voluntarily mop up wheat grains produced locally (Tanzania and Kenya) before importing from outside the region.

8.        Following the conclusion of the meeting, the co-chairs signed the minutes of the bilateral meeting and the sideline meeting for wheat stakeholders outlining the way forward.

9.        It was agreed that the next bilateral trade meeting will be held in November, 2017 in the Republic of Kenya.

Friday, September 8, 2017

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Iran na Balozi wa Palestina nchini Tanzania

Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang akiwa na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Augustine Mahiga wakimsikiliza mkalimani wa Kitanzania Bi. Maisara Ally  anayefanya kazi na Ubalozi wa Iran hapa nchini wakati viongozi hao walipokutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 8 Septemba 2017.

Balozi wa Palestina nchini Tanzania Mhe. Hazem Shabat akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.




Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa China nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Wizarani Balozi wa China anayemaliza muda wake wa kazi nchini, Mhe. LU Youqing ambaye alifika Wizarani kwa lengo la kuaga. Hafla fupi ya kumuaga Balozi LU Youqing ilifanyika Wizarani tarehe 07 Septemba, 2017.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha Waziri Mahiga na Balozi LU kuzungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Balozi LU iliyofanyika Wizarani.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi LU wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani. Katika mazungumzo yao Mhe. Mahiga alimpongeza Balozi LU kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini. Mhe. Mahiga alimwelezea Balozi LU kama mtu wa tofauti katika utendaji kazi na utekelezaji wake wa majukumu kwa kuwa alijitolea kikamilifu kuhakikisha ushirikiano kati ya Tanzania na China unaimarika na kukua zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Balozi LU (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi LU. Katikati ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi.
Sehemu ya ujumbe kutoka Ubalozi wa China ambao ulifuatana na Balozi LU.
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi Maalum ya Nembo ya Taifa inayowakilisha utendaji uliotukuka wa Balozi LU
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi nyingine ya Kinyago cha UMOJA kuonesha umoja na mshikamano uliopo kati ya Tanzania na China
Mhe. Balozi LU akipokea zawadi nyingine ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro pamoja na Tembo kama kumbukumbu kwa Balozi LU ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini na pia mchango wa China katika mapambano dhidi ya ujangili wa pembe za ndovu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Rogers Sianga nae akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi LU.
Balozi LU akifurahia zawadi ya Ngozi ya Pundamilia kutoka kwa Kamishna Sianga ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa China katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya
Picha ya pamoja kuhitimisha hafla ya kumuaga Balozi LU

Wednesday, September 6, 2017

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akutana na Balozi wa India nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Innocent Shiyo akizungumza na Balozi wa India hapa nchini, Mhe.Sandeep Arya alipotembelea Wizarani hivi karibuni. Katika mazungumzo yao Balozi Shiyo alimweleza Balozi Arya masuala mbalimbali kuhusu Tanzania na ushiriki wake katika masuala ya kikanda ikiwemo amani, siasa na usalama hususan katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Mazungumzo yakiendelea kati ya Balozi Shiyo na Balozi Arya. Wengine katika picha ni Afisa kutoka Ubalozi wa India (Kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Isaac Isanzu (kulia)
Balozi Shiyo na Balozi Arya katika picha ya pamoja
Balozi Shiyo akiagana na Balozi Arya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Tuesday, September 5, 2017

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wahitimu mafunzo ya JKT

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo ya JKT kuanza. Mafunzo hayo yalifanyika Kambi ya JKT ya Oljoro mkoani Arusha kwa kipindi cha wiki sita kuanzia tarehe 24 Julai hadi 04 Septemba 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa mahafali hayo akiwa katika jukwaa kwa ajili ya kupokea heshima kutoka kikosi cha Vijana cha Operesheni Viwanda (hakipo pichani) ambacho kimejumuisha watumishi 30 wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Mgeni Rasmi, Balozi Mlima akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima yake na kikosi kilichohitimu mafunzo ya JKT ambacho kilijumuisha watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje
 Mgeni Rasmi, Balozi Aziz Mlima wakiwa wamesimama pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (kulia) na Kamanda wa Kambi ya Oljoro kwa ajili kuangalia vikosi vikipita mbele yao katika mwendo wa pole na kasi
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole

Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa kasi

Mgeni Rasmi akikabidhi zawadi kwa waliofanya vizuri zaidi. 



Bi. Khadija Othman akipokea zawadi yake

Bw. Graison Ishengoma akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni Rasmi

Bw. Edward Komba akipokea zawadi yake.

Wahitimu wa mafunzo ya JKT kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakila kiapo cha utii

Risala kwa Mgeni Rasmi. katika risala hiyo waliahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote waliyoyapata watakaporejea katika kituo chao cha kazi. Walijifunza uzalendo, utii, ustahamilivu, ukakamavu na mengine mengi.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao nao washapitia mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wakiwashuhudia wenzao wakihitimu mafunzo ya JKT katika awamu ya pili.

Burdani ilikuwepo siku ya mahafali. Hapo bendi ya Jeshi ikitumbwiza.

Onesho la Makamandoo hapo mmoja wao amebeba ndoo za maji kwa kutumia meno yake.

Mkuu wa Kambi ya Oljoro akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkuu wa JKT ili amkaribishe Mgeni Rasmi

Mwakilishi wa Mkuu wa JKT akimkaribisha Mgeni Rasmi atoe hotuba ya kufunga mafunzo hayo. Kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi alisisitiza umuhimu wa taasisi nyingine za umma kuiga Wizara ya Mambo ya Nje kwa kupeleka watumishi wao ili kupata mafunzo ya JKT ambayo ni muhimu kwa kujenga uzalendo, nidhamu na umoja.

Mgeni Rasmi akisoma hotuba yake. Alitoa ushuhuda kuwa watumishi walioshiriki mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wameonesha umahiri mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ndio sababu amepeleka kundi lingine katika awamu ya pili. Aliahidi atawapeleka watumishi wa Wizara yake wenye sifa ikiwemo ya umri (chini ya miaka 40) hatua kwa hatua hadi watakapomalizika.

Wahitimu wa mafunzo ya JKT wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi
 Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali hayo. Hapo afande anateta na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bw. Othman Rashid.
Mkurugenzi wa Utawala katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nigel Msangi akimpongeza Bw. Wambura kwa kuhitimu mafunzo ya JKT.
Tumemaliza salama, shukran kwa Wizara kwa kutuandalia mafunzo haya yenye tija kubwa kwetu.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala; Bi. Ngusekela Nyerere na Mwalimu wa somo la Uzalendo ambaye alikuwa Msadizi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.

Furaha tumemaliza mafunzo, Kutoka kushoto ni Felista Rugambwa, Teodos Komba na Rose Mbilinyi.


Wanaimba nyimbo za jeshi.

Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi na wahitimu wa JKT.