Balozi Silima mara baada ya mazungumzo na Profesa Ubeid. |
Tuesday, March 26, 2019
Balozi wa Tanzania nchini Sudan akutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika
Mtanzania ateuliwa kuongoza Taasisi ya Kimataifa nchini China
Balozi Ali Mchumo ============================================================= |
Balozi Mstaafu, Mhe. Ali Mchumo (Pichani) kutoka Tanzania ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya International Network
for Bamboo and Rattan (INBAR) yenye makao yake makuu mjini Beijing, China. Taarifa ya
uteuzi wake imetangazwa tarehe 25 Machi 2019 katika tovuti ya taasisi ya INBAR. Taasisi ya
INBAR ilianzishwa mwaka 1997 kwa madhumuni ya kukuza matumizi ya mianzi (Bamboo) kama
njia endelevu ya utunzaji wa mazingira . Taasisi hiyo inaundwa na nchi wanachama
45 na ina ofisi zake za kanda nchini
Ethiopia, Ghana na Equador. Tanzania ni mojawapo ya nchi mwanachama
mwanzilishi wa taasisi hiyo na imenufaika na uwepo wa taasisi hiyo kupitia
miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na INBAR pamoja na mafunzo kwa wataalam wa zao la mianzi.
Mawaziri wa Afrika wakutana Morocco
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe akifuatilia
mazungumzo na michango ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakati wa mkutano
huo.
|
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe wa tatu kutoka
kushoto, mstari wa nyuma, akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri na
Wawakilishi wa Mawaziri walioshiriki mkutano huo.
|
Monday, March 25, 2019
Nafasi za ajira katika Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
NAFASI ZA AJIRA KATIKA
JUMUIYA YA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR)
Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba
nafasi za ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu
(ICGLR) yenye makao makuu Bujumbura, Burundi; Kituo cha Kikanda cha Kupambana
na Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia (Regional Training Facility on SGBV)
kilichopo Kampala, Uganda na Kituo cha Demokrasia na Utawala Bora cha Levy
Mwanawasa (Levy Mwanawsa Regional Centre for Democracy and Good Governance)
kilichopo Lusaka, Zambia. Ajira hizo ni kama ifuatavyo:-
SEKRETARIETI YA MAZIWA MAKUU
- Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (Director, Administration and Finance);
- Mkurugenzi wa Nyaraka na Mikutano (Director, Documentation and Conferences);
- Mkurugenzi wa Mawasiliano (Director, Communications);
- Mshauri wa Masuala ya Sheria (Legal Adviser).
KITUO CHA DEMOKRASIA
NA UTAWALA BORA CHA LEVY MWANAWASA
- Mkurugenzi wa Kanda (Regional Director);
- Mkuu wa Utafiti (Head, Research);
- Mkuu wa Jukwaa na Uchunguzi (Head, Fora and Observatories).
KITUO CHA KIKANDA CHA KUPAMBANA NA UKATILI NA
UNYANYASAJI WA KIJINSIA
- Mratibu wa Mafunzo (Training Coordinator) na
- Mratibu wa masuala ya TEHAMA, Utafiti na Elimu (IT, Research and Knowledge Coordinator).
Waombaji wa nafasi
hizo wanapaswa kuwasilisha barua za maombi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kabla ya tarehe 4 Aprili 2019 ili yaweze kuwasilishwa kwenye Sekretarieti ya ICGLR
kwa wakati.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dodoma
25 Machi 2019
Sunday, March 24, 2019
Prof. Kabudi afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya wajumbe wa Baraza wakati wa mkutano wao wa mwaka |
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao ni wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wakifuatilia mkutano |
Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ukiendelea na wajumbe wakifuatilia |
Wajumbe wa Baraza |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa TUGHE wa Wizara |
Picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza |
Rais Nyusi aishukuru Tanzania kwa misaada ya dawa na chakula
....Picha zinazoonesha madhara yaliyotokana na Kimbunga... |
|
Saturday, March 23, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje azungumza na Watumishi wa Wizara
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichani alipozungumza nao |
Sehemu nyingine ya Watumishi wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano wao na Mhe. Waziri |
Mkutano ukiendelea huku Watumishi wa Wizara wakifuatilia |
Sehemu nyingine ya Watumishi |
Mhe. Waziri akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Ilani ya Chama cha Mapinduzi |
Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Joachim Otaru |
Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Bw. Wilbroad Kayombo |
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Watumishi na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo |
Friday, March 22, 2019
Prof. Kabudi awasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Taarifa kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) (hawapo pichani) wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara kilichofanyika kwenye Ofisi za Bunge, Dodoma tarehe 22 Machi, 2019. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan M. Mwinyi. |
Kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikiendelea |
Sehemu ya Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati hiyo wakifuatilia kikao |
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya NUU |
Wajumbe wa Kamati wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) |
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao |
Mjumbe wa Kamati akichangia hoja wakati wa kikao hicho |
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara wakiwa kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya NUU |
Mjumbe wa Kamati akichangia jambo wakati wa kikao na Wizara |
Mjumbe mwingine wa Kamati ya Bunge ya NUU akichangia hoja wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara |
Mhe. Mbunge akichangia hoja |
Subscribe to:
Posts (Atom)