Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Kombo Haji,
amekutana na kufanya mazungumzo rasmi na Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Kimataifa cha Afrika (International University of Africa - IUA), Profesa
Kamal Muhammed Ubeid, mjini Khartoum, Sudan. Katika mazungumzo baina yao, Prof. Ubeid alimhakikishia
Balozi Silima kuwa, chuo hicho kitaendeleza ushirikiano na Tanzania kwa
kuendelea kutoa ufadhili wa elimu ya juu kwa wanafunzi wengi zaidi wa
Kitanzania kadri hali itakavyoruhusu.
Takribani wanafunzi wa Kitanzania wapatao 517 wanaosoma katika
vyuo mbalimbali nchini Sudan ambapo 490 kati yao wanasoma katika chuo hicho
kilichopo Khartoum katika fani mbalimbali zikiwemo uhandisi wa mafuta na gesi,
uchumi, udaktari na dawa na maabara, sheria, lugha na fani nyinginezo.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.