Mkutano ukiendelea kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wa Cuba ukioongozwa na Mhe. Guastavo Rodriguez Roller. |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali ya Cuba kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo kwa mtazamo wake wa kuanzisha ushirikiano mpana zaidi baina ya Zanzibar na Tanzania katika sekta hiyo muhimu.
Akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, katika makao makuu ya wizara hiyo mjini Havana, Balozi Seif alieleza kuwa, Zanzibar na Cuba zimekuwa na ushirikiano ya karibu katika sekta za afya na elimu kwa kipindi kirefu sasa suala ambalo limeleta mafanikio makubwa.
Balozi Seif alibainisha kuwa, kwa kuwa maonyesho ni moja ya njia ya kubadilishana mawazo kitaaluma alimuomba Waziri wa Kilimo wa Cuba kutenga muda wa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Tanzania yanayofanyika mwezi Agosti wa kila mwaka nchini.
Kwa upande wake, Mhe. Roller alibainisha kwamba, Cuba imebarikiwa kuwa na hekta milioni 10,000,000 ambazo zinatoa ajira kwa wakulima zaidi ya 5,000.Alifafanua kuwa, asilimia 70% ya ardhi hiyo ina maliasili, asilimia 3.5 inatumika kufuga na zaidi ya asilimia 60 inatumika katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo pekee.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.