TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NAFASI ZA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA
YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira katika Sekretarieti ya
Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.
Ajira hizo ni kama ifuatavyo:-
1.
Mshauri wa masuala ya
Miundombinu na Usanifu wa Majengo (Advisor
Infrustructure and Architecture);
2.
Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Senior
Director, Economic, Youth and Sustainable
Development) na
3.
Mshauri na Mkuu wa
Kitengo cha Biashara na Ushindani (Advisor and Head, Trade and Competitiveness section).
Watanzania wenye sifa wanahamasishwa kuomba nafasi hizo hasa ikizingatiwa kuwa, nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambazo hazina watumishi wengi katika ngazi ya maafisa waandamzi watapewa kipaumbele ili kuimarisha uwiano wa kikanda katika nafasi hizo za ajira.
Kwa kuzingatia sera ya Jumuiya ya Madola ya usawa wa kijinsia, Sekretarieti ya taasisi inawahimiza wanawake wengi zaidi wenye vigezo kuomba nafasi hizo.
Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hizo za ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti http://thecommonwealth.org.jobs.
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo ni tarehe 10 Aprili, 2019; tarehe 16 Aprili, 2019 na tarehe 17 Aprili, 2019, mtawalia.
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dodoma
28 Machi, 2019.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.