Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza alipotembelea Jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki linalojengwa kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Mkuu alizipongeza baadhi ya Wizara kwa kukamilisha majengo ya Ofisi zao na kuzitaka Wizara zote kuhakikisha zinakamilisha hatua za mwisho za ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kusawazisha maeneo na kuweka miundombinu muhimu kama maji na umeme kabla ya tarehe 15 Aprili 2015. Aidha, aliziagiza Taasisi kama TANESCO, TARULA na DUWASA kukamilisha kuweka huduma hizo muhimu za umeme, maji na barabara kwenye mji huo. Tayari Wizara 20 zimekamilisha majengo ya ofisi zao kwa zaidi ya asilimia 98. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega (kulia) na Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe (katikati). Ziara hiyo imefanyika tarehe 27 Machi 2019 |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.