Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Evelyne Assenga akikabidhiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia, Hemedi Iddi Mgaza baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wanaolazwa ICU. Wengine katika picha ni wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia. Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo leo, balozi huyo amesema wataendelea kuandaa mafunzo ya huduma za afya kwa wataalam mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo. Kauli hiyo imetolewa leo na balozi huyo wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kuhusu upumuaji kwa wataalam kutoka hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Bugando, Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Hospitali ya Benjamini Mkapa na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema kwamba Muhimbili itaendelea kutoa ushirikiano kwa wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia ili kuhakikisha wataalam wabadilisha uzoefu na wenzao kutoka Saudia Arabia. Mafunzo hayo yameandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Al balsam Cure and Care International Charity Organization. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.