TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa kuhusu ziara ya
Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda
Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, atawasili nchini tarehe 7 Machi 2019
kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Mhe.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ziara hii itatoa fursa kwa viongozi hao wawili
kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi
hizi mbili. Aidha, Viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya
mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe. Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, atawasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa Tisa Alasiri tarehe 7
Machi 2019 na kupokelewa na mwenyeji wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Rais Kagame anatarajia kuondoka nchini tarehe 8
Machi, 2019.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
6 Machi
2019
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.