Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Dkt. Richard Sezibera. Katika mazungumzo yao, Mhe. Sezibera alimpongeza Mhe. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo. Mhe. Sezibera yupo nchini kwa ajili ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.