Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Malawi, Mhe. Glad Chembe Munthali (kushoto), Balozi wa Msumbiji, Mhe. Monica D.C. Mussa (wa pili kushoto) na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini, Mhe. Martin Tavenyika (wa tatu kushoto) wakati wa zoezi la kuwakabidhi mabalozi hao misaada ya dawa na chakula ambavyo Serikali ya Tanzania imetoa kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika. Tukio hilo limefanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi 2019
|
Mhe. Prof. Kabudi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhe. Waziri Ummy kuhusu aina ya dawa zilizotolewa msaada kwenye nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko yaliyozikumba nchi hizo |
|
Sehemu ya magari yaliyobeba shehena ya msaada wa dawa na chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kwenye nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kama inavyoonekana kabla ya kuanza kupakiwa kwenye ndege
|
Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha kwenye magari na kupakia kwenye ndege misaada ya madawa na chakula ambavyo Serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika |
|
|
Askari hao wakiwajibika |
|
Mhe. Prof. Kabudi akiwa ameongozana na Mhe. Waziri Ummy , Mabalozi na Viongozi mbalimbali mara baada ya kukamilisha zoezi la kuwakabidhi Mabalozi misaada ya dawa na chakula vilivyotolewa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya nchi zao zilizopatwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko kufuatia tufani kali iliyozikumba baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. |
|
Brigedia Jenerali Francis Shirima wa kikosi cha anga cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa jukumu la kuipeleka misaada ya dawa na chakula katika nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe ambazo zimekumbwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo la kusini mwa Afrika |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.