TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
NAFASI ZA AJIRA KATIKA
JUMUIYA YA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR)
Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba
nafasi za ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu
(ICGLR) yenye makao makuu Bujumbura, Burundi; Kituo cha Kikanda cha Kupambana
na Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia (Regional Training Facility on SGBV)
kilichopo Kampala, Uganda na Kituo cha Demokrasia na Utawala Bora cha Levy
Mwanawasa (Levy Mwanawsa Regional Centre for Democracy and Good Governance)
kilichopo Lusaka, Zambia. Ajira hizo ni kama ifuatavyo:-
SEKRETARIETI YA MAZIWA MAKUU
- Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (Director, Administration and Finance);
- Mkurugenzi wa Nyaraka na Mikutano (Director, Documentation and Conferences);
- Mkurugenzi wa Mawasiliano (Director, Communications);
- Mshauri wa Masuala ya Sheria (Legal Adviser).
KITUO CHA DEMOKRASIA
NA UTAWALA BORA CHA LEVY MWANAWASA
- Mkurugenzi wa Kanda (Regional Director);
- Mkuu wa Utafiti (Head, Research);
- Mkuu wa Jukwaa na Uchunguzi (Head, Fora and Observatories).
KITUO CHA KIKANDA CHA KUPAMBANA NA UKATILI NA
UNYANYASAJI WA KIJINSIA
- Mratibu wa Mafunzo (Training Coordinator) na
- Mratibu wa masuala ya TEHAMA, Utafiti na Elimu (IT, Research and Knowledge Coordinator).
Waombaji wa nafasi
hizo wanapaswa kuwasilisha barua za maombi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kabla ya tarehe 4 Aprili 2019 ili yaweze kuwasilishwa kwenye Sekretarieti ya ICGLR
kwa wakati.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dodoma
25 Machi 2019
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.