Kikosi cha wanajeshi kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania kinachoshiriki Mazoezi ya Kijeshi ya Pamoja nchini India yanayojulikana kama "Africa-India Field Training Exercise- AFINDEX-2019" kikiwa katika picha. Mazoezi hayo ambayo yanafanyika katika mji wa Pune nchini India yameanza tarehe 18 Machi 2019. Lengo kuu la mazoezi hayo pamoja na mambo mengine, yamelenga kujenga uwezo wa majeshi ya nchi zinazoshiriki kulinda amani katika vikosi vya Umoja wa Mataifa duniani ambapo India na Afrika inachangia wanajeshi wengi katika vikosi hivyo. Mbali na Tanzania, nchi
nyingine za Mataifa ya Afrika zinazoshiriki mazoezi hayo ya kijeshi ya pamoja
na India ni Afrika ya Kusini, Benin, Botswana, Ghana, Kenya, Mauritius, Misri,
Msumbiji, Namibia, Niger, Nigeria, Senegal, Sudani, Uganda, Zambia na Zimbabwe. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.