Wednesday, April 3, 2019
Thursday, March 28, 2019
TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL
28 Machi 2019
TAARIFA KWA UMMA
TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL
UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inatangaza ufadhili wa mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini
Israel. Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba
makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na
mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.
SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI
- Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia.
- Awe amehitimu mafunzo ya Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,Stashahada au Astashahada ya Vyuo vya kilimo vinavyotambulika nchini.
- Awe na afya njema.
- Awe na ujuzi wa kuandika na kuongea lugha ya Kiingereza.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi na watu wa tamaduni mbalimbali.
- Awe tayari kurejea nchini baada ya mafunzo yake.
UTARATIBU WA KUFANYA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakiwa
yameambatishwa na nakala za nyaraka zifuatazo:
i. Cheti cha kuzaliwa na uraia.
ii. Vyeti vya kitaaluma.
iii. Hati ya Kusafiria au uthibitisho wa maombi ya pasipoti.
iv. Cheti cha kuthibitisha afya kutoka hospitali inayotambulika.
v. Barua ya kuonesha sababu za kushiriki mafunzo hayo (Motivation letter) kwa lugha ya Kiingereza.
vi. Wasifu (Curriculum Vitae).
vii. Picha mbili ndogo (Passport size).
viii. Majina na anwani za wadhamini watatu wanaoishi nchini akiwemo mwalimu wa Chuo ulichohitimu.
Maombi yote yatumwe kupitia
anwani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Jengo
la LAPF
Ghorofa
ya 6,
Barabara
ya Makole,
S.L.P 2933,
DODOMA.
DODOMA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
Fursa za ajira.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NAFASI ZA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA
YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira katika Sekretarieti ya
Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.
Ajira hizo ni kama ifuatavyo:-
1.
Mshauri wa masuala ya
Miundombinu na Usanifu wa Majengo (Advisor
Infrustructure and Architecture);
2.
Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Senior
Director, Economic, Youth and Sustainable
Development) na
3.
Mshauri na Mkuu wa
Kitengo cha Biashara na Ushindani (Advisor and Head, Trade and Competitiveness section).
Watanzania wenye sifa wanahamasishwa kuomba nafasi hizo hasa ikizingatiwa kuwa, nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambazo hazina watumishi wengi katika ngazi ya maafisa waandamzi watapewa kipaumbele ili kuimarisha uwiano wa kikanda katika nafasi hizo za ajira.
Kwa kuzingatia sera ya Jumuiya ya Madola ya usawa wa kijinsia, Sekretarieti ya taasisi inawahimiza wanawake wengi zaidi wenye vigezo kuomba nafasi hizo.
Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hizo za ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti http://thecommonwealth.org.jobs.
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo ni tarehe 10 Aprili, 2019; tarehe 16 Aprili, 2019 na tarehe 17 Aprili, 2019, mtawalia.
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dodoma
28 Machi, 2019.
Balozi Seif Ali Iddi akutana na Rais wa Bunge la Cuba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Rais wa Bunge la Cuba, Mhe. Esteban Lazo Harnandez, mjini Havana, Cuba.
|
Mhe. Harnandez kulia akipokea zawadi ya mlango
wa mji Mkongwe kutoka kwa Balozi Seif kama ishara ya kufunguliwa milango ya
kuitembelea Zanzibar.
|
Mhe. Harnandez akimtembeza Mhe. Balozi Iddi katika sehemu mbalimbali za jengo la Bunge ya Cuba lenye historia ya muda mrefu ambazo zimewekwa kama kumbukumbu ya taifa hilo. |
Mhe. Balozi Iddi wa pili
kutoka kulia na ujumbe wake akifanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya mjini Havana, Cuba.
|
=====================================
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amelitembelea Bunge la Cuba na
kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa bunge la nchi hiyo, Mhe. Esteban
Lazo Harnandez.
Katika
mazungumzo baina ya viongozi hao wawili, Mhe. Harnandez ameahidi kuwa, Cuba
itaendelea kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, katika kuendeleza wananchi wake licha ya taifa hilo la Caribean
kupita katika mabadiliko ya kisiasa, uchumi na utamaduni.
Mhe.
Harnandez alieleza kuwa, kutokana na mabadiliko yaliyopo sasa katika mfumo wa
dunia katika masuala ya uchumi, siasa na utamaduni Jamhuri ya Cuba
imelazimika kufanya mabadiliko ya katiba yake ili yalingane na mfumo huo wa
dunia inayoizunguka.
Alifafanua
kuwa, tayari Bunge la Cuba limeshafanya marekebisho katika katiba yake kutoa
nafasi kwa wananchi wake kuwa na uwezo na uhuru wa kumiliki nyumba, ardhi
pamoja na uwepo wa waziri mkuu atakayekuwa na mamlaka ya kusimamia utendaji wa
serikali.
Mhe.
Harnandez alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kwamba katika vikao
vya bunge hilo vinavyotarajiwa kuanza wiki ijayo baada ya kukamilika kwa
uchaguzi wa wabunge, serikali ya nchi hiyo itakuwa imepiga hatua kubwa zaidi ya
maendeleo kutokana na mabadiliko hayo.
Rais huyo
wa Bunge la Cuba alisisitiza kwamba taasisi za kifedha zitalazimika kuzingatia
ukusanyaji bora zaidi wa mapato katika maeneo yote ya uchumi ili kuimarisha
ushiriki wa wananchi waliowengi katika mfumo huo.
Mhe.
Harnandez alihitimisha kwa kumuhakikishia Balozi Seif kwamba, uhusiano wa
muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili utaendelea kuimarishwa na kukuzwa
katika muda wote.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Iddi alimpongeza Mhe. Harnandez kwa
kuchaguliwa tena kuliongoza bunge hilo na kueleza kuwa, hatua hiyo inaonesha wazi ishara halisi ya kukubalika
vyema na wananchi wa nchi hiyo kupitia viongozi wake.
Halikadhalika,
Mhe. Balozi Iddi alieleza kuwa, kwa ujumla Zanzibar itaendelea kufuatilia
mabadiliko ya Cuba na kuangalia endapo inaweza kuiga mabadiliko hayo ili
kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi walio wengi.
Mhe.
Balozi Iddi na ujumbe wake ulihitimisha ziara yake nchini humo kwa
kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya ya Cuba uliokuwa ukiongozwa na
Naibu Waziri, Mhe. Bibi Marcia Cobas, katika makao makuu ya wizara hiyo
yaliyopo Havana, Cuba.
Katika
mazungumzo hayo ya ushirikiano wa kindugu, Balozi Iddi alisema matunda ya
darasa la madaktari wazalendo waliosimamiwa na wataalamu pamoja na wahadhiri wa
nchi ya Cuba yameanza kutoa matumaini.Alifafanua kuwa, kitendo cha
Serikali ya Cuba kukubali kupunguza gharama kubwa ya kuwaendeleza madaktari hao
wazalendo wapatao 15 katika shahada ya juu ya udaktari wa uzamili nchini humo
kinaendelea kuleta faraja kubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja
na watu wake.
Alisema
wakati Zanzibar ikiendelea kutekeleza sera ya afya ya kuwa na miuondombinu ya
huduma za afya katika umbali usiozidi kilomita tano kundi hilo na madaktari
linaloendelea kuongezeka kila mwaka litakuwa mkombozi wa utekelezaji wa sera
hiyo muhimu.
Naye
Kaibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Bibi Asha Ali Abdullah, aliueleza uongozi
huo wa Wizara ya Afya Cuba kwamba, hivi sasa Zanzibar inapita katika
kipindi cha kujiimarisha kwenye mapambano yake dhidi ya maradhi yasiyoambukiza.
Bibi
Abdullah alisema maradhi yasiyoambukiza kama Kisukari pamoja na Shindikizo la
Damu hivi sasa yamekuwa yakiathiri wananchi walio wengi na kuleta vifo vingi.
Hata hivyo, jitihada zinachukuliwa ili kupunguza kasi ya athari za
maradhi hayo na kuimaliza kabisa kadhia hiyo kabisa.
Alibainisha
kuwa, maradhi ya Malaria hivi sasa yamepungua kutokana na kampeni kubwa
iliyofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi na mataifa wahisani katika
kuangamiza vilui lui vya maradhi hayo.
Katibu
Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alimuhakikishia Naibu Waziri wa Afya wa
Cuba kwamba ushauri wote walioupata katika ziara yao kwenye taasisi za Afya
nchini Cuba likiwemo suala la upatikanaji wa dawa litazingatiwa na iwapo
linaweza kuleta afueni ya gharama kwa Zanzibar litachukuliwa hatua mara moja.
Mhe. Dkt. Ussi atembelea Shamba Asilia nchini Cuba
Mhe. Dkt. Ussi akiendelea kupata maelezo juu ya kilimo cha miwa. |
Juu na chini Mhe. Dkt. Ussi akipata maelezo namna ya utengenezaji wa mbolea isiyokuwa na kemikali yeyote. |
Bw. Lopezi akimwonyesha Mhe.Dkt. Ussi teknolojia ya kifaa cha kupandia mazao. |
Mhe. Dkt. Ussi akizungumza na mmoja wa wakulima kwenye shamba hilo, aliyeonekana kufurahishwa na ujio wa Watanzania. |
Sehemu ya mazao yanayopatikana kwenye shamba hilo. |
Mhe. Balozi Seif ahudhuria maonesho ya kilimo Cuba.
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitizama kikundi cha wakulima waliokuwa wameandaliwa kutoa burudani kwenye maonyesho hayo. |
Burudani zikiendelea kutolewa na vikundi mbalimbali vya wakulima. |
Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Mhe. Jose Miguel Rodriquez De Armas, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo. |
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea na kujionea mazao mbalimbali yanayolimwa nchini Cuba kwenye mabanda ya makampuni mbalimbali ya wafanyabiashara na yawakulima. |
Balozi Seif Ali Iddi afanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa Cuba.
Mkutano ukiendelea kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wa Cuba ukioongozwa na Mhe. Guastavo Rodriguez Roller. |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali ya Cuba kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo kwa mtazamo wake wa kuanzisha ushirikiano mpana zaidi baina ya Zanzibar na Tanzania katika sekta hiyo muhimu.
Akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, katika makao makuu ya wizara hiyo mjini Havana, Balozi Seif alieleza kuwa, Zanzibar na Cuba zimekuwa na ushirikiano ya karibu katika sekta za afya na elimu kwa kipindi kirefu sasa suala ambalo limeleta mafanikio makubwa.
Balozi Seif alibainisha kuwa, kwa kuwa maonyesho ni moja ya njia ya kubadilishana mawazo kitaaluma alimuomba Waziri wa Kilimo wa Cuba kutenga muda wa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Tanzania yanayofanyika mwezi Agosti wa kila mwaka nchini.
Kwa upande wake, Mhe. Roller alibainisha kwamba, Cuba imebarikiwa kuwa na hekta milioni 10,000,000 ambazo zinatoa ajira kwa wakulima zaidi ya 5,000.Alifafanua kuwa, asilimia 70% ya ardhi hiyo ina maliasili, asilimia 3.5 inatumika kufuga na zaidi ya asilimia 60 inatumika katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo pekee.
Wednesday, March 27, 2019
Waziri Mkuu atembelea Mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma
Mhe. Waziri Mkuu akikagua moja ya chumba cha ofisi katika jengo la Wizara lililopo Mtumba |
Sehemu ya Watumishi wa Umma walioshiriki ziara ya Waziri Mkuu kwenye Mji wa Serikali |
Watumishi wakimsikiliza Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani) |
Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe kwa kuratibu mpango huo kikamilifu. |
Fursa za mafunzo nchini Thailand
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
FURSA ZA UFADHILI
WA MASOMO KWA WATANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu katika fani
mbalimbali kutoka Serikali ya Thailand.
Kozi hizo zitakazotolewa kwenye Vyuo
mbalimbali nchini humo, zitajikita katika fani za Filosofia ya Uchumi Timilifu; Mabadaliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula; Afya ya Jamii
na Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Wizara inawahimiza Watanzania wenye
sifa kuomba nafasi hizo za mafunzo zilizotangazwa na Serikali ya Thailand kwa
mwaka 2019.
Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni
tarehe 31 Machi 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba,
tafadhali tembelea tovuti ifuatayo: http://www.tica.thaigov.net
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya
Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
27 Machi 2019
Nchi za SADC zimeahidi kushikamana na Saharawi
Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Rais wa Saharawi, Mhe. Brahim Ghali katika ukumbi wa mikutano jijini Pretoria. |
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC na wawakilishi wa Wakuu Nchi na Marafiki wa Sharawi walioshiriki mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja. |
Subscribe to:
Posts (Atom)