Thursday, April 25, 2019

Tanzania na China zaadhimisha miaka 55 ya ushirikiano

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb.) akitoa hotuba kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China yaliyofanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye Maktaba  ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tarehe 24 Aprili, 2019.

 Katika hotuba yake, Prof. Ndalichako ameipongeza China kwa kuimarisha ushirikiano  na  Tanzania hususan katika sekta za Elimu, Biashara na Ujenzi wa miundombinu. Aidha,   amesema kuwa mahusiano kati ya Tanzania na China ni ya muda mrefu na mchango wa nchi hiyo kwenye maendeleo ya Tanzania ni dhahiri akitolea mfano  ujenzi wa Reli ya TAZARA pamoja na ujenzi wa viwanda mbalimbali vya nguo nchini. Vilevile China imeendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa kubadilishana uzoefu.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda, Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara, na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi  za umma na binafsi nchini. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda akiwa na mke wake Mhe. Tunu Pinda (kushoto)  pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Prof. Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.
Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia hotuba hiyo.

Prof. Ndalichako akiendelea kuhutubia kwenye maadhimisho hayo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Mhe. Wang Ke naye akihutubia kwenye maadhimisho hayo. 
Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho hayo.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda pamoja na mke wake Mhe. Tunu Pinda (kushoto) pamoja na viongozi wengine kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakipitia kitabu chenye kuonyesha ushirikiano wa Tanzania na China kwenye sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza (kushoto) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara (kulia) wakipitia kitabu kinachoonesha namna Tanzania na China zinavyoshirikiana kwenye sekta mbalimbali.
Maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijadiliana jambo wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akitambulishwa kwa wageni walioshiriki maadhimisho hayo.
Mshehereshaji, Bi. Bertha Makilagi akitoa mwongozo wa ratiba ya maadhimisho hayo kwa wageni waalikwa.
 Juu na chini ni maonyesho mbalimbali yakiendelea kuonyeshwa na vikundi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo


Mgeni Rasmi pamoja na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati nyimbo za  mataifa ya Tanzania na China zikiimbwa.
Kikundi chenye mchanganyiko wa wanafunzi kutoka Tanzania na China wakiongoza kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania na China kabla maadhimisho hayo kuanza.
Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wasanii aliyekuwepo kwenye maadhimisho hayo
Mhe. Prof. Ndalichako na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.

















 















Wednesday, April 24, 2019

PUBLIC NOTICE




Nafasi za Ajira Katika Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali


Dodoma, 24 Aprili 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nafasi za Ajira

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa ya ajira iliyotangazwa na Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (Organization for the Prohibition of Chemicals Weapons-OPCW) iliyopo The Hague, Uholanzi. Nafasi hiyo ni ya Technical Support Officer-P3 ambapo mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 06 Juni 2019.

Wenye sifa zinazohitajika, wanashauriwa kufanya maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya sekretarieti; www.opcw.org

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Thursday, April 18, 2019

Fursa ya Ajira.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NAFASI YA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa, kuomba nafasi ya ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR).

Ajira hiyo ni Mtaalam wa Uhakiki wa Nyaraka. Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hiyo ya ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti www.icglr.org.

Maombi yote yatumwe kwenda katika barua pepe jobs@icglr.org na nakala itumwe katika barua pepe gerard.nayuburundi@icglr.org  yakiwa na kichwa cha habari Maombi ya nafasi ya Mtaalam wa Uhakiki wa Nyaraka.

Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hiyo ni  tarehe 25 Aprili, 2019.

    Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
      Dodoma.

Wednesday, April 17, 2019

Dkt. Ndumbaro afanya mazungumzo na Mwakilishi wa JICA nchini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.), amefanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini, Bw.Naofumi Yamamura, hivi karibuni katika ofisi za wizara Dodoma. Mazungumzo hayo, yanalenga kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia shirika hilo katika masuala ya miundombinu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini, Bw. Naofumi Yamamura,mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara. 

Mazungumzo yakiendelea.
Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Bi. Bertha Makilagi na Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Charles Faini, wakifuatilia mazungumzo hayo.
Afisa Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Takusaburo Kimura, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini, Bw. Naofumi Yamamura na Afisa Mwandamizi wa shirika hilo, Bw. Takusaburo Kimura, wakimsikiliza Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (hayupo pichani).


Tuesday, April 16, 2019

Dkt. Ndumbaro afanya mazungumzo na balozi wa Italia nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mheshimiwa Roberto Mengoni katika ofisi za wizara Dodoma. Katika mazungumzo hayo, miongoni mwa mambo mengine, Tanzania na  Italia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta za uwekezaji, utalii pamoja na  kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia.  
Mazungumzo yakiendelea.
Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Charles Faini (wa kwanza na kulia) na Afisa wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Kisa Mwaseba (wa mwisho kushoto), wakifuatilia mazungumzo baina ya  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(Mb.) na Balozi wa Italia nchini, Mheshimiwa Roberto Mengoni.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) na Balozi wa Italia nchini, Mheshimiwa Roberto Mengoni, wakiagana mara baada ya mazugumzo.

Monday, April 15, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje yafanya kikao cha kwanza cha Menejimenti katika Mji wa Serikali Mtumba

Leo tarehe 15 Aprili, 2019, Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imefanya kikao cha kwanza cha Menejimenti katika Mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini Dodoma uliosimikwa rasmi na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 13 Aprili 2019. Pichani: Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Kasidi Faraji Mnyepe, akiongoza kikao hicho.
Baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa katika kikao hicho.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Caroline Chipeta, akifuatilia kikao hicho.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Bibi Agnes Kayola, akifuatilia kikao hicho.
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Paul Kabale akifuatilia kikao hicho.
Kikao kikiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Kasidi Faraji Mnyepe (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara mara baada ya kumaliza kikao chao cha kwanza cha Menejimenti kilichofanyika kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deus Kaganda kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi Mona Mahecha na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Caesar Waitara wakibadilishana mawazo mara baada ya kikao.
Balozi Mteule, Dkt. Mpoki Ulisubisya kwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Stephen Mbundi na Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota wakibadilishana mawazo mara baada ya kikao.

Saturday, April 13, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje yashiriki uzinduzi wa mji wa serikali

Leo tarehe 13 Aprili, 2019, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeshiriki katika hafla ya kuuzindua Mji wa Serikali iliyofanyika katika eneo la Mtumba, Dodoma. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.Pichani:Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (wa nne kutoka kulia) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi huo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb.), (aliye katika mimbari) akisisitiza jambo wakati wa kutoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa  Mji wa Serikali.



Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa dini wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani).




Umati ulioshiriki katika uzinduzi wa Mji wa Serikali ukifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.


Kanali Mbuge akipiga saluti kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe  Magufuli, kwa kumpandisha cheo kuwa Brigadia Jenerali baada ya kushiriki kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu katika ujenzi wa miradi mbalimbali  ya serikali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa Mererani na  ukuta wa Ikulu ya Chamwino na nyumba za watumishi wa umma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, akikata  utepe katika jengo la Ofisi ya Rais, Utumishi, kuashiria uzinduzi wa jengo hilo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akibadilishana mawazo na baadhi ya mawaziri walioshiriki katika uzinduzi wa Mji wa Serikali.


Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akiteta jambo na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali.

Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi,akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Mheshimiwa Livingstone Lusinde, kulia kwa waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Kasidi Faraji Mnyepe.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, akibadilishana mawazo na Mwanasheria wa Serikali, Prof. Adelaus Kilangi.