Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiendelea kuzungumza na Mhe. Bi. GE Huijun pamoja na ujumbe alioambatana nao. |
Monday, July 22, 2019
Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la jimbo la Zhejiang nchini China
Friday, July 19, 2019
Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Switzerland na Denmark waliyomaliza muda wa kazi nchini
Balozi wa Italy Mhe. Roberto Mengoni (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Waziri Bw. Charles Mbando wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) |
Kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed naye akizungumza neno wakati wa hafla ya kuwaaga Mabalozi wa Switzerland na Denmark (hawapo pichani) |
Prof. Kabudi apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule nchini
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Balozi mteule Sanjiv Kohli mara baada ya kupokea nakala zake |
Mazungumzo yakiendelea |
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi Mteule Mhe. Sanjiv Kohli mara baada ya kumalizaka kwa hafla hiyo |
Ubalozi wa Tanzania nchini India wafanikisha hafla ya uzinduzi wa safari za Air Tanzania mjini Mumbai
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai nchini India |
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania, Mhandisi Emmanuel Korosso nae akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za Air Tanzania mjini Mumbai, India |
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo |
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa tayari kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa safari za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai, India |
Mhe. Kamwele akiwa na Viongozi wengine kutoka Tanzania na India wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa safari za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai |
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akikata keki maalum kuashiria kuanza rasmi kwa safari za Ndege za Air Tanzania mjini Mumbai, India |
Matukio mbalmbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Air Tanzania mjini Mumbai |
Mhe. Waziri Kamwelwe akipokea Jarida la Travel ambalo ambalo huandika taarifa kuhusu masuala ya usafirishaji na uchukuzi kwa ujumla |
Mhe. Waziri Kamwelwe (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (wa tatu kushoto), viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na India pamoja na Marubani waliofamikisha ndege ya kwanza ya Air Tanzania kutua Mumbai kwa ajili ya safari za kibiashara |
Mhe. Balozi Luvanda katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki uzinduzi wa safari za ndege ya Air Tanzania mjini Mumbai. Kushoto ni Bw. Kheri Goloka, Afisa wa Ubalozi Mwandamizi. |
Wafanyabiasha kutoka China ziarani nchini kutafuta fursa za biashara
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Wafanyabiashara
kutoka Jimbo la Zhejiang, China kuja nchini kutafuta fursa za biashara
Ujumbe wa
wafanyabiashara 25 kutoka Kampuni kubwa 15 za Jimbo la Zhejiang nchini China
ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Jimbo hilo, Mhe. Bi.
GE Huijun utafanya ziara nchini kuanzia tarehe 20 hadi 23 Julai 2019 kwa lengo
la kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za biashara
na uwekezaji zilizopo nchini.
Ziara
hiyo inalenga kukuza mahusiano ya kiuchumi baina ya Jimbo la Zhejiang na
Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile teknolojia, mawasiliano,
ujenzi na uchukuzi, afya na madini.
Mhe. GE
Huijun pia atafuatana na viongozi 13 wa Serikali ya Zhejiang kwenye ziara hiyo
ambayo itaanzia Zanzibar tarehe 20 Julai 2019.
Ujumbe
huo ukiwa nchini, pamoja na masuala mengine, unategemea kukutana na Viongozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kwa ajili ya kujadiliana nao kuhusu fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji
zilizopo nchini.
Ukiwa
Zanzibar, ujumbe huo utatembelea maeneo ya viwanda ya Amani na Fumba kwa ajili
ya kujionea fursa za uwekezaji. Aidha, ujumbe huo utakutana na Mamlaka ya
Uwekezaji na Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) pamoja na
kukutana na wafanyabiashara wa Zanzibar kwa madhumuni ya kuanzisha ushirikiano.
Kadhalika
ujumbe huo utashiriki ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Wafanyabiashara
wa Tanzania na Wafanyabiashara kutoka Zhejiang utakaofanyika jijini Dar es
Salaam tarehe 22 Julai 2019.
Ujumbe
huo unategemea kukamilisha ziara yao nchini tarehe 23 Julai, 2019.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
19 Julai
2019
Thursday, July 18, 2019
VACANCY ANNOUNCEMENT
PRESS
RELEASE
VACANCY
ANNOUNCEMENT FROM THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)
The Ministry of Foreign
Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice No. 21D-2019/BDT-DDR/External/D2
from the International Telecommunication Union (ITU) inviting qualified
Tanzanians to apply for the post of Deputy
to the Director and Chief of the Administration and Operations Coordination
Department (DDR).
Application
details can be found through the ITU website: http://www.itu.int/employment/Recruitment/index.html.
Closing
date for application is Sunday 25th August 2019.
Issued by;
Government
Communication Unit,
Ministry of Foreign
Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
18th July
2019.
Wednesday, July 17, 2019
Prof. Kabudi azungumza na Mabalozi wastaafu wa Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kwa nia ya kupata ushauri na maoni yao kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo Prof. Palamagamba John Kabudi ameongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (wa kwanza kulia). |
Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani).
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) |
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), Naibu Waziri Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani |
Tuesday, July 16, 2019
Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo hapa nchini.
Katika mazungumzo hayo Prof. Palamagaba John Kabudi amewafahamisha hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutanao ya wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyopangwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019
Kwa upande wa waheshimiwa Mabalozi hao walifurahishwa kwa hatua ya maandalizi iliyofikiwa, na kuelezea furaha yao kuhusu uwamuzi wa Serikali kuwashirikisha mapema katika maandalizi hayo.
Sehemu ya Mabalozi wa Nchi za Afrika na wanachama wa Jumuiya ya SADC wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya watumishi kutoka Balozi za Afrika zilizopo nchini |
Prof. Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi alipokutana nao |
Balozi wa Afrika Kusini Mhe. Thamsanga Mseleku akielezea jambo katika mkutano na Waziri Prof. Palamagamba John Kabudi |
Mkutano ukiendelea. |
Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech watua nchini kutafuta fursa za biashara na uwekezaji
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Wafanyabiashara
na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech watafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini
Tanzania
Ujumbe wa wafanyabiashara na
wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wamewasili nchini tarehe 13 Julai, 2019 kwa lengo
la kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali nchini ili kujadili fursa
za biashara na uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali hususan afya, kilimo, miundombinu
ya barabara na reli,nishati, madini,utalii na wa ujenzi wa viwanda vya madawa na
vifaa tiba.
Ziara hiyo inatokana na juhudi
za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa
Tanzania uliopo nchini Ujerumani ambao pia unawakilisha Tanzania katika Jamhuri
ya Czech na wadau wengine muhimu katika kushawishi wafanyabiashara wakubwa kuja
kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.
Ujumbe huo wa watu kumi na mbili
(12) ukiwa nchini, pamoja na masuala mengine, unategemea kukutana na uongozi wa
Wizara naTaasisi mbalimbali zikiwemo, Wizara ya Viwanda na Biashara, Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC), Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bohari Kuu ya Dawa na Halmashauri ya Jiji la
Dar es Salaam.
Vilevile, ujumbe huo unategemea kushiriki katika Kongamano la
Uwekezaji wa Viwanda vya Kutengeneza Madawa na Vifaa Tiba kwa ubia kati ya
Serikali na Sekta Binafsi, lililoandaliwa na Bohari Kuu ya Dawa. Kongamano hilo
limepangwa kufanyika tarehe 17 Julai, 2019 katika Ukumbi wa Mkutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ziara ya ujumbe huo nchini ni
chachu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Czech.
Kadhalika, ziara ya ujumbe huo ni moja ya mikakati ya utekelezaji wa Sera ya
Mambo ya Nje inayojikita katika diplomasia ya uchumi na kuhamasisha uwekezaji katika
sekta ya viwanda ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi
wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
Mhe. Dkt. Abdallah Saleh
Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania
asiye na makazi nchini Czech ameambatana na ujumbe huo wa wafanyabiashara na wawekezaji.
Ujumbe huo kutoka Jamhuri ya
Czech unategemea kukamilisha ziara yao nchini tarehe 17 Julai, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
16 Julai 2019
Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania asiye na makazi nchini Czech akiwa kwenye mkutano kati ya ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech na Kituo cha UwekezajiTanzania (TIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai 2019. Mhe. Balozi Possi ameambatana na ujumbe huo hapa nchini ambao una lengo la kutafuta fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta za afya, kilimo, nishati na madini na ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba. |
Sehemu ya Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech ukufuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) |
Sehemu nyingine ya Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech |
Mkutano ukiendelea |
Mhe. Balozi Possi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa TIC na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech. |
Subscribe to:
Posts (Atom)