Sunday, November 10, 2019
Friday, November 8, 2019
DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA ALGERIA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa
Algeria, Balozi Rachid Bladehane
Katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro wamekubaliana kuimarisha
ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria hususan katika masuala ya Biashara na
Uwekezaji. Wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo kwa kufanya
nmkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) hivi karibu ili kupitia
na kuangalia maeneo ya ushirikiano yenye manufaa kwa nchi
IMARISHENI MIPANGO YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI ILI KUACHAANA NA UTEGEMEZI- RAIS MAGUFULI AZIAMBIA NCHI ZA AFRIKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha zinaimarisha
mipango ya kujikomboa kiuchumi ili ziweze kuwa huru kweli na kuachana na
utegemezi.
"Viongozi wengi wa
Afrika wametambua kuwa mustakabali wa nchi zetu uko mikononi mwetu na kwamba
uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na maana sana endapo mataifa yetu yataendelea
kuwa tegemezi kiuchumi,hatuwezi kuwa na uhuru wetu wenyewe endapo mataifa yetu
yataendelea kuwa ombaomba," amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amesema hayo
jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje
wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini.
Amesema kuwa kutafuta
ukombozi wa kiuchumi ndio jukumu ambalo liko mbele yao viongozI wa Bara la
Afrika na kuzitaka nchi za Afrika kuimarisha uhusiano na nchi za Nordic katika
maeneo ya uwekezaji wa kibiashara na viwanda ili kuondokana na utegemezi kwa
nchi nyingine.
Amezitaka nchi za Afrika kushirikiana
kuwekeza katika viwanda ili kuzalisha bidhaa
kutoka katika malighafi ambazo nchi zinauwezo wa kuwa nazo.
"Ni lazima kujenga
viwanda na kuchakata malighafi ambazo tutawauzia nchi nyingine na hivyo kuweza
kujikomboa kutoka katika utegemezi wa mataifa mengine, hatuwezi kuwa huru kama
tutaendelea kuwa na utegemezi kwa nchi zilizoendelea," alisisitiza mhe.
Rais
Amesema Nchi za
Afrika zina kitu kikubwa cha kujifunza
kutoka kwa nchi za Nordic ambazo zina
jumla ya watu milioni 27 huku Pato lao
kwa mwaka likiwa ni Dola za Marekani trilioni 1.7 huku Tanzania yenye watu ni milioni 55, mara
mbili zaidi ya nchi za Nordic ikiwa na pato
la taifa lenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 56.99.
"Tuna jambo kubwa la
kujifunza kwa nchi za Nordic Tanzania tuko mara mbili zaidi kwao pata letu
halifiki kwao, Tuko milioni 57 pata letu ni trillions 1.7 wenzetu wako milioni 27 pata lao ni trillions 1.6,"
alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa ni lazima Afrika ijifunze kutoka katika
nchi hizo ili kujua ni wapi zimekosea,
tuko hapa leo hii na hawa marafiki zetu tutumie nafasi hii kujifunza kutoka
kwao.
Ameongeza kuwa Pato la nchi za Afrika lina thamani ya
Dola za Marekani trilioni 2.334 huku pato la mtu mmoja likiwa ni wastani wa
Dola za Marekani 62,963. Lakini kwenye nchi za Afrika ni wastani wa Dola za
Marekani 1,945.
Amesema Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweeden;
licha ya kuwa na eneo dogo (kilomita za mraba milioni 3.5) na idadi ya watu
wapatao milioni 27 tu; zina uchumi mkubwa. Pato lao kwa mwaka jana (2018)
lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 1.7.
Amezishukuru nchi za
Nordic kwa kuliunga mkono bara la Afrika kuanzia wakati wa harakati za ukombozi
wa Afrika licha ya ukweli kwamba kwa wakati ule suala hilo lilikuwa gumu sana
lakini nchi za Nordic zilikuwepo.
Mhe. Rais amezikaribisha
nchi za Nordic, pamoja na mataifa mengine, yakiwemo ya Afrika, kuja kuwekeza
nchini Tanzania ambapo kuna mazingira wezeshi ya uwekezaji ni muafaka na
yanatabirika, kutokana na amani na utulivu wa kisiasa, lakini pia mwenendo wa
ukuaji wa uchumi ni mzuri ambapo, kwa sasa, ni wastani wa asilimia 7.
Thursday, November 7, 2019
PROF. KABUDI AKUTANA NA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY, FINLAND NA DENMARK
Na
Mwandishi wetu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana na
kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Denmark, Finaland na
Norway ambao wamekuja nchini kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya
Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamezungumzia na kukubaliana
kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kirafiki na kihistoria yaliyopo
baina ya nchi hizo.
Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amezieleza nchi
hizo kuhusu msimamo wa Serikali ya Tanzania katika kujiimarisha kiuchumi
kupitia ukusanyaji wa mapato ya ndani ili iendelee kutoa elimu bure na bora kwa
watoto wa kitanzania, huduma bora za afya kwa watanzania, kuwezesha upatikanaji
wa maji safi na salama kwa wananchi wote na kufikisha huduma za Nishati kwa
watanzania wote hasa wa vijijini.
Amesema kwamba Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele
kwa Siasa za maendeleo ili kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na
wa viwanda inafikiwa.
“Tanzania haiangalii Siasa za nguvu, tunaangalia
Siasa za kuletea wananchi maendeleo, na kwa mpango huo tutaendelea kuimarisha
ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani na kumfanya kila mtanzania kulipa kodi ili
tuendelee kutoa elimu bure ya msingi na sekondari kwa watoto wa Kitanzania,
kuboresha huduma za afya hadi vijijini, upatikanaji wa maji safi na salama na
kuhakikisha huduma za nishati ya umeme zinawafikia watanzania wote hadi wa
vijijini,” alisema Prof. Kabudi.
Amewahahakishia mawaziri hapo kuwa Tanzania
itaendelea kuheshimu makubaliano ya Kimataifa hasa katika suala la wakimbizi na
kuwafanya watu wanaokuja kutafuta hifadhi za kisiasa nchini kwetu wana pata
hifadhi hizo.
Akizungumza alipokutana na Prof. Kabudi Waziri wa
Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Koffod amemuhakikishia Prof. Kabudi Serikali
ya Denmark itaendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha
huduma za jamii kama vile utoaji wa elimu bure, huduma za afya na maji
salama.
Pia amesisitiza kwamba wataendelea kuunga mkono
mpango wa utoaji wa elimu ya ufundi nchini na kuwafanya vijana wa kike na wa
kiume Nchimbi kushiriki katika harakati za ujenzi wa taifa lao.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka
Haavisto ameahidi nchi yake kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo ya
misitu, utawala bora, ukusanyaji mapato, haki za binadamu na Tehama.
Amesema Finland pia itaendelea kuisaidia Tanzania
kwenye Elimu kwakuwa Elimu imekuwa na mchango mkubwa na hivyo kutoa viongozi wa
baadae.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe.
Ine Eriksen Soreide ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi kubwa inayofanya
ya kupambana na rushwa na ufisadi na hivyo kuongeza imani ya Norway
kuwezesha zaidi nchini. Aidha, ameahidi kuwa nchi yake itaendeleza Ushirikiano
wake na Tanzania.
Prof. Kabudi pia amekutana na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Msumbiji Mhe. Jose Pacheco na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo
kuimaraisha mahusiano baina ya Msumbiji na Tanzania.
Mawaziri hao wako nchini kuhudhuria mkutano wa 18
wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika jijini
Dar es Salaam.
Wednesday, November 6, 2019
Job Announcement at Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW)
PRESS RELEASE
Job Announcement at Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons.
Dodoma, 06 November, 2019
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Legal Adviser (Director) (D-2)
For more details on the vacant post kindly click HERE
Closing date for application is 16th October 2019.
Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Tuesday, November 5, 2019
MABALOZI WA NCHI ZA SADC, NEW DELHI WAENDELEA KUPAZA SAUTI KUPINGA VIKWAZO DHIDI YA ZIMBABWE
Wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Balozi Luvanda (hayupo pichani) alipohutubia wakati wa hafla ya SADC Day |
Mhe. Balozi Luvanda akiwa na Mabalozi na Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Siku ya SADC |
Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fortune Chasi, Waziri wa
Nishati wa Zimbabwe ambaye alishiriki hafla ya Siku ya SADC kama Mgeni Maalum
|
Rais Xi atembelea Banda la Tanzania Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Nje.
Banda la Tanzania |
Banda la Tanzania lilivyopendeza |
Bidhaa za Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje nchini China |
Bidhaa za Tanzania zikiwa katika vifungashio bora kabisa zilivutia watu wengi katika maonesho hayo. |
Subscribe to:
Posts (Atom)