Sunday, November 10, 2019

MAADHIMISHO YA MIAKA 105 YA VITA YA KWANZA NA MIAKA 75 YA VITA VYA PILI VYA DUNIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakipokea heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anasoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa amesimama pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kushoto) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kulia) Mhe. Joerg Herrera wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Meja Jenerali Sherrif  Sheikh Othman (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya Makamanda kutoka Ujerumani na Uingereza wakiwa wamesimama kutoa heshima katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Baadhi ya askari wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kama ishara ya heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa ameongozana Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kulia) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kushoto) Mhe. Joerg Herrera kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiweka mashada ya maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
 Mmoja wa wapiganaji wa vita ya pili ya dunia Mzee Malagila Shimba mwenye umri wa miaka 98 akipiga saluti mara baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiwaongoza  baadhi ya makamanda kutoka nchi za Tanzania,Ujerumani na Uingereza kuweka shada la maua katika mnara wa askari ulioko Posta Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.





Friday, November 8, 2019

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA ALGERIA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Balozi Rachid Bladehane

Katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria hususan katika masuala ya Biashara na Uwekezaji. Wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo kwa kufanya nmkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) hivi karibu ili kupitia na kuangalia maeneo ya ushirikiano yenye manufaa kwa nchi





IMARISHENI MIPANGO YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI ILI KUACHAANA NA UTEGEMEZI- RAIS MAGUFULI AZIAMBIA NCHI ZA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezitaka  nchi za Afrika kuhakikisha zinaimarisha mipango ya kujikomboa kiuchumi ili ziweze kuwa huru kweli na kuachana na utegemezi.

"Viongozi wengi wa Afrika wametambua kuwa mustakabali wa nchi zetu uko mikononi mwetu na kwamba uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na maana sana endapo mataifa yetu yataendelea kuwa tegemezi kiuchumi,hatuwezi kuwa na uhuru wetu wenyewe endapo mataifa yetu yataendelea kuwa ombaomba," amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini.

Amesema kuwa kutafuta ukombozi wa kiuchumi ndio jukumu ambalo liko mbele yao viongozI wa Bara la Afrika na kuzitaka nchi za Afrika kuimarisha uhusiano na nchi za Nordic katika maeneo ya uwekezaji wa kibiashara na viwanda ili kuondokana na utegemezi kwa nchi nyingine.

Amezitaka nchi za Afrika kushirikiana kuwekeza katika viwanda ili  kuzalisha bidhaa kutoka katika malighafi ambazo nchi zinauwezo wa kuwa nazo.

"Ni lazima kujenga viwanda na kuchakata malighafi ambazo tutawauzia nchi nyingine na hivyo kuweza kujikomboa kutoka katika utegemezi wa mataifa mengine, hatuwezi kuwa huru kama tutaendelea kuwa na utegemezi kwa nchi zilizoendelea," alisisitiza mhe. Rais

Amesema Nchi za Afrika  zina kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwa nchi za  Nordic ambazo zina jumla ya watu milioni 27  huku Pato lao kwa mwaka likiwa ni Dola za Marekani trilioni 1.7  huku Tanzania yenye watu ni milioni 55, mara mbili zaidi ya nchi za Nordic  ikiwa na pato la taifa lenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 56.99.

"Tuna jambo kubwa la kujifunza kwa nchi za Nordic Tanzania tuko mara mbili zaidi kwao pata letu halifiki kwao, Tuko milioni 57 pata letu ni trillions 1.7 wenzetu  wako milioni 27 pata lao ni trillions 1.6," alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa ni lazima Afrika ijifunze kutoka katika nchi hizo ili kujua ni  wapi zimekosea, tuko hapa leo hii na hawa marafiki zetu tutumie nafasi hii kujifunza kutoka kwao.

Ameongeza kuwa Pato la nchi za Afrika lina thamani ya Dola za Marekani trilioni 2.334 huku pato la mtu mmoja likiwa ni wastani wa Dola za Marekani 62,963. Lakini kwenye nchi za Afrika ni wastani wa Dola za Marekani 1,945.
Amesema Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweeden; licha ya kuwa na eneo dogo (kilomita za mraba milioni 3.5) na idadi ya watu wapatao milioni 27 tu; zina uchumi mkubwa. Pato lao kwa mwaka jana (2018) lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 1.7.

Amezishukuru nchi za Nordic kwa kuliunga mkono bara la Afrika kuanzia wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika licha ya ukweli kwamba kwa wakati ule suala hilo lilikuwa gumu sana lakini nchi za Nordic zilikuwepo.

Mhe. Rais amezikaribisha nchi za Nordic, pamoja na mataifa mengine, yakiwemo ya Afrika, kuja kuwekeza nchini Tanzania ambapo kuna mazingira wezeshi ya uwekezaji ni muafaka na yanatabirika, kutokana na amani na utulivu wa kisiasa, lakini pia mwenendo wa ukuaji wa uchumi ni mzuri ambapo, kwa sasa, ni wastani wa asilimia 7.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania katika mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza wakati akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide akizungumza wakati akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Thursday, November 7, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY, FINLAND NA DENMARK

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana ofisini jijini Dar es Salaam. Mawaziri hao wapo Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam. Tukio hili lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania katika nchi za Nordic, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Msumbiji Mhe. Jose Pacheco akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) walipokutana jijini Dar es Salaam.  

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Denmark, Finaland na Norway ambao wamekuja nchini kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamezungumzia na kukubaliana  kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kirafiki na kihistoria yaliyopo baina ya nchi hizo.

Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amezieleza nchi hizo kuhusu msimamo wa Serikali ya Tanzania katika kujiimarisha kiuchumi kupitia ukusanyaji wa mapato ya ndani ili iendelee kutoa elimu bure na bora kwa watoto wa kitanzania, huduma bora za afya kwa watanzania, kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote na kufikisha huduma za Nishati kwa watanzania wote hasa wa vijijini.

Amesema kwamba Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwa Siasa za maendeleo ili kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na wa viwanda inafikiwa.

“Tanzania haiangalii Siasa za nguvu, tunaangalia Siasa za kuletea wananchi maendeleo, na kwa mpango huo tutaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani na kumfanya kila mtanzania kulipa kodi ili tuendelee kutoa elimu bure ya msingi na sekondari kwa watoto wa Kitanzania, kuboresha huduma za afya hadi vijijini, upatikanaji wa maji safi na salama na kuhakikisha huduma za nishati ya umeme zinawafikia watanzania wote hadi wa vijijini,” alisema Prof. Kabudi.


Amewahahakishia mawaziri hapo kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu makubaliano ya Kimataifa hasa katika suala la wakimbizi na kuwafanya watu wanaokuja kutafuta hifadhi za kisiasa nchini kwetu wana pata hifadhi hizo.

Akizungumza alipokutana na Prof. Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Koffod amemuhakikishia Prof. Kabudi Serikali ya Denmark itaendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha huduma za jamii kama vile utoaji wa elimu bure, huduma za afya na maji salama. 
Pia amesisitiza kwamba wataendelea kuunga mkono mpango wa utoaji wa elimu ya ufundi nchini na kuwafanya vijana wa kike na wa kiume Nchimbi kushiriki katika harakati za ujenzi wa taifa lao.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto ameahidi nchi yake kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo ya misitu, utawala bora, ukusanyaji mapato, haki za binadamu na Tehama.

Amesema Finland pia itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye Elimu kwakuwa Elimu imekuwa na mchango mkubwa na hivyo kutoa viongozi wa baadae. 

Naye Waziri  wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi kubwa inayofanya ya kupambana na rushwa na ufisadi na hivyo kuongeza imani ya  Norway kuwezesha zaidi nchini. Aidha, ameahidi kuwa nchi yake itaendeleza Ushirikiano wake na Tanzania.

Prof. Kabudi pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Jose Pacheco na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kuimaraisha mahusiano baina ya Msumbiji na Tanzania.

Mawaziri hao wako nchini kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Wednesday, November 6, 2019

Job Announcement at Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW)





PRESS RELEASE

Job Announcement at Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons. 


Dodoma, 06 November, 2019 

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Legal Adviser (Director) (D-2)


For more details on the vacant post kindly click HERE

Closing date for application is 16th October 2019. 


Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Tuesday, November 5, 2019

MABALOZI WA NCHI ZA SADC, NEW DELHI WAENDELEA KUPAZA SAUTI KUPINGA VIKWAZO DHIDI YA ZIMBABWE

Balozi wa Tanzania nchini India na Mwenyekiti wa Kundi la Mabalozi wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Baraka Luvanda, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya SADC (SADC Day) yaliyofanyika Jijini New Delhi tarehe 02 Novemba 2019.
Wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Balozi Luvanda (hayupo pichani) alipohutubia wakati wa hafla ya SADC Day
Mhe. Fortune Chasi, Waziri wa Nishati wa Zimbabwe na Mgeni Maalum akihutubia wakati wa hafla ya Siku ya SADC iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini, Jijini New Delhi tarehe 02 Novemba 2019

Mgeni rasmi wa hafla ya Siku ya SADC, Bwana Rajesh Swami, Mkurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya India, Sehemu ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika akihutubia wakati wa hafla ya Siku ya SADC iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini India, Jijini New Delhi tarehe 02 Novemba 2019.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa na Mabalozi na Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Siku ya SADC

Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fortune Chasi, Waziri wa Nishati wa Zimbabwe ambaye alishiriki hafla ya Siku ya SADC kama Mgeni Maalum

Picha ya pamoja 
==================================================================

Mabalozi wa nchi za SADC, New Delhi waendelea kupaza sauti kupinga vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Mabalozi wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo nchini India chini ya Uenyekiti wa Mhe. Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini humo walikutana katika hafla ya Siku ya SADC (SADC Day), iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Luvanda jijini New Delhi, India tarehe 2 Novemba 2019.

Wakati wa hafla hiyo, Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuelezea pamoja na mambo mengine, suala la kuondolewa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za Ulaya dhidi ya Zimbabwe. Alieleza kuwa Tamko dhidi ya vikwazo hivyo liliwasilishwa rasmi kwenye Mamlaka za Serikali ya India siku ya tarehe 25 Oktoba 2019 siku ambayo iliamuliwa na Viongozi Wakuu wa Nchi za SADC kuwa siku maalum ya kupaza sauti dhidi ya vikwazo hivyo.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Mkurugenzi katika Wizara ya Nje ya India, Sehemu ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bwana Rajesh Swami alieleza kuwa kwa miaka mingi uhusiano baina ya India na nchi za SADC umekuwa mzuri na kuwezesha biashara, uwekezaji, utalii, elimu, afya na uhusiano wa mtu na mtu kuimarika kwa kiwango cha juu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mgeni Maalum, Mhe. Fortune Chasi, Waziri wa Nishati wa Zimbabwe, alimshukuru Balozi Luvanda, Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za SADC nchini India na Mabalozi wote wa nchi za SADC nchini humo kwa kuandaa hafla hiyo na jinsi walivyosimamia suala la kupaza sauti kupinga vikwazo dhidi ya nchi yake na kuwaomba waendelee na juhudi hizo hadi vikwazo hivyo vitakapoondolewa.

Rais Xi atembelea Banda la Tanzania Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Nje.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Xi atembelea Banda la Tanzania Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Nje.   
Dar Es Salaam, 05 Novemba 2019
Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje (China International Importation Expo) yamefunguliwa na Rais wa China, Mhe Xi Jinping tarehe 05 Novemba 2019.  Maonesho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa Mataifa 64 akiwemo Rais wa Ufaransa Mhe Emmanuel Macron, Mawaziri Wakuu wa Jamaica; Serbia na Greece. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa.

Baada ya kufungua maonesho hayo Rais wa China ametembelea Mabanda ya nchi tano likiwemo Banda la Tanzania.  Nchi nyingine ambazo Rais Xi ametembelea mabanda yao ni Ufaransa; Ugiriki; Serbia na Jamaica.

Katika ziara ya kutembelea Banda la Tanzania, Rais Xi Jinping alifuatana na Waziri Mkuu wa Jamaica; Greece na Serbia na kupokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Innocent Bashungwa na alitumia muda wa dakika 10 katika banda la Tanzania.  Rais Xi na wageni wake walipata maelezo kuhusu bidhaa mbalimbali za kilimo na madini zinazopatikana nchini Tanzania na vivutio vya utalii. Vile vile, Rais Xi alipokea salamu salaamu za  Mhe Rais Dk John Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Rais wa China ameipongeza Tanzania kwa kushiriki katika maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje na ametuma salaamu za pongezi kwa Mhe Rais Magufuli kwa kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na China.  Aidha, Rais Xi alivutiwa zaidi na bidhaa ya korosho za Tanzania na madini ya Tanzanite ambapo alitaka kufahamu zaidi juu ya upatikanaji wa bidhaa hizo katika soko la China na bei ya Tanzanite. Alipewa majibu ya kutosha.

Maonesho ya Kimataifa yataendelea hadi tarehe 10 Novemba 2019.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Banda la Tanzania
Banda la Tanzania lilivyopendeza

Bidhaa za Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje nchini China
Bidhaa za Tanzania zikiwa katika vifungashio bora kabisa zilivutia watu wengi katika maonesho hayo.