Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein. |
Tuesday, July 13, 2021
BALOZI WA SOMALIA NCHINI TANZANIA, BALOZI ABDI MOHAMED HUSSEIN AAGA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA UWAKILISHI HAPA NCHINI
Monday, July 12, 2021
SERIKALI YAKUTANA NA TAASISI,MASHIRIKA NA MABALOZI KUJADILI MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI
Na Mwandishi wetu
Katika
kukuza Diplomasia ya Uchumi, kuimarisha na kushirikisha Jumuiya za Kimataifa Serikali
imekutana na Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa
zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha
2021/22 pamoja na mbinu za pamoja za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19.
Mkutano
huo umefanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wizara za Kisekta zikiwemo Fedha
na Mipango, Viwanda na Biashara, Afya, Maliasili na Utalii, Uwekezaji na Wizara
ya Fedha na Mipango – Zanzibar pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa mashirika
ya Kimataifa 54 kutoka nchi na taasisi mbalimbali.
Lengo
la Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ni kuwapitisha Mabalozi na Wawakilishi
wa Mashirika ya Kimataifa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2021/22, Mipango ya
Utekelezaji wake na Maeneo ya Ushirikiano.
Akiongoza
Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametaja sababu za Serikali kukutana na Mabalozi
pamoja na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa ambao pia ni wadau
wa maendeleo ili kuwajengea uelewa katika mipango na utekelezaji wa Bajeti ya
Serikali ya 2021/22 pamoja na maeneo ya Ushirikiano.
“tumeona
tuweke utaratibu wa kukutana na wadau hawa wa maendeleo ili kujenga uelewa wa
pamoja katika maeneo muhimu yaliyoainishwa katika bajeti ya Serikali ili waweze
kupata picha halisi ya mipango na mikakati ya Serikali katika utekelezaji wa
Bajeti,” amesema Balozi Mulamula
Kwa
Upande wake Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo
Fanti amesema uamuzi wa Serikali wa kukutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika
na Taasisi za Kimataifa umekuwa mzuri sana umesaidia kufahamu mipango na
mikakati mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa bajeti yake ya 2021/22.
“Kupitia
mkutano wa leo tumeweza kupata picha halisi ya ushirikiano wetu na Tanzania na umezidi
kuimarika lakini pia tumeweza kuona na kujadili baadhi ya vipaumbele vya bajeti
ya Serikali ya Tanzania, mipango ya maendeleo jambo ambalo sisi kama wadau wa
maendeleo limetuhamasisha kuendelea kushirikiana kwa ukaribu n a uwazi zaidi,” amesema
Balozi Fanti
Mkutano
huo umehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigula Nchema (Mb), Waziri
wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kutoka
Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, Pamoja na Naibu
Waziri Wizara ya Uwekezaji Mhe. William Tate Olenasha (Mb).
Pamoja na Mambo mengine, Mawaziri hao wamepata fursa ya kutoa ufafanuzi katika maeneo yanayohusu wizara zao ikiwa ni pamoja na mipango ya Serikali katika kukuza uchumi, kukusanya mapato, kukuza Viwanda, kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji, kukuza utalii na jinsi Serikali inavyojipanga kuboresha sekta ya afya nchini hasa katika kupambana na janga la UVIKO 19.
Saturday, July 10, 2021
CHODOTA; MIRADI YA MIUNDOMBINU INAYOTEKELEZWA NCHINI ITACHAGIZA KASI YA USTAWI WA EAC
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere. |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere. |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea mradi wa ujezi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere. |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi – Lungalunga) |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi–Lungalunga) |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa kipande cha barabara ya Tanga miji hadi Pangani. |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa kwenye ziara ya kutembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga. |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wakiangalia ukarabati wa jengo la Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga. |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga. |
Friday, July 9, 2021
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KENYA BALOZI RAYCHELLE OMAMO AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA UHURU KENYATTA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Balozi Wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dany Kazungu (kushoto) na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. John Simbachawene (kulia) wakati wakimsubiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo anayetarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa Nchini |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo mara baada ya kuwasili Nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine na Viongozi,Maafisa waandamizi wa Wizara za Mambo ya Nje wa Kenya na Tanzania |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) barua rasmi ya mualiko wa kutembelea Kenya |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo walipokutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake wa Tanzania |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake. Aliyekaa Kushoto kwa Balozi Mulamula ni Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akigonga glasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo kupongezana wakati akihitimisha ziara yake ya siku moja ya kikazi hapa nchini (Aliyevaa koti ni Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) |
Thursday, July 8, 2021
BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO 112 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA,CARIBBEAN NA PACIFIC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 112 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific unaofanyika kwa njia ya mtandao |
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said akifuatilia mjadala katika Mkutano wa 112 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pazific unaofanyika kwa njia ya mtandao - Dar es Salaam Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said (kushoto) akiwa na Kamishna wa fedha za Nje wa Wizara ya feda na Mipango Bi Sauda Msemwa (katikati) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw. Hassan Mwamweta wakifuatilia mjadala katika Mkutano wa 112 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pazific unaofanyika kwa njia ya mtandao - Dar es Salaam |
TANTRADE, BALOZI ZA TANZANIA ZAELEKEZWA KUTANGAZA FURSA ZA BIASHARA
Na Mwandishi wetu, Dar
Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeelekezwa kushirikiana na Balozi
za Tanzania katika kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji hapa nchini.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“…………….Balozi
zetu zina uhusiano wa karibu na TanTrade ambapo TanTrade moja kati ya majukumu
yake ni kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata taarifa
sahihi ili kusaidia kujua ni bidhaa gani za Tanzania zinaweza kuuzwa nje kwa
urahisi lakini pia kujua ni nchi husika yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” amesema
Balozi Fatma
Balozi
Fatma ameongeza kuwa ili bidhaa za Tanzania ziendelee kuuzwa katika masoko ya
kimataifa ulimwenguni, TanTrade iendelee kushirikiana kwa karibu na Balozi za
Tanzania katika kuhakikisha kuwa inatoa taarifa sahihi za bidhaa.
“Ushirikiano
baina ya TanTrade na Balozi zetu uendelee kuimarishwa ili kuwawezesha
wafanyabiashara kupata taarifa sahihi na kwa wakati, lakini pia ushirikiano huu
utasaidia kutangaza fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania katika Mataifa
ya Kigeni,” amesema Balozi Fatma
Balozi
Fatma pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya maonesho ya Sabasaba
kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika
maonesho hayo ili kujua ni kwa namna gani wataweza kunufaika na fursa za kuuza
bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa
“Kupitia
maonesho haya watanzania watumie fursa hii kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara
kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika maonesho haya, lakini pia kuangalia ni
namna gani watanufaika na fursa za kuuza bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa,”
Amesema Balozi Fatma Rajab.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika
Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akipokea nakala ya Jarida la Diplomasia linalochapishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es
salaam |
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akimsikiliza mtumishi wa Wizara alipokuwa akimpatia maelezo juu ya
baadhi ya viongozi (Mawaziri) waliohudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki tangu mwaka 1961 hadi sasa mwaka 2021 |
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akiongea na waandishi wa habari wakati alipokuwa katika banda la
Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
Afisa
kutoka Tume ya Utalii Zanzibar akimfafanulia jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati
alipotembelea banda la tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
Afisa kutoka Bodi ya Mapato Zanzibar akimuelezea jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |