Tuesday, July 13, 2021

BALOZI WA SOMALIA NCHINI TANZANIA, BALOZI ABDI MOHAMED HUSSEIN AAGA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA UWAKILISHI HAPA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein. Balozi Abdi Mohamed Hussein amefika kuagana na Balozi Mulamula baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa Nchini

Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein akisisitiza jambo wakati alipokutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) (hayupo pichani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkabidhi zawadi  Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein.Balozi Abdi Mohamed Hussein amefika kuagana na Balozi Mulamula baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa Nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiagana na  Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein. Balozi Abdi Mohamed Hussein ameaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa Nchini
 

Monday, July 12, 2021

SERIKALI YAKUTANA NA TAASISI,MASHIRIKA NA MABALOZI KUJADILI MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI

Na Mwandishi wetu

Katika kukuza Diplomasia ya Uchumi, kuimarisha na kushirikisha Jumuiya za Kimataifa Serikali imekutana na Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mbinu za pamoja za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19.

Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wizara za Kisekta zikiwemo Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Afya, Maliasili na Utalii, Uwekezaji na Wizara ya Fedha na Mipango – Zanzibar pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa 54 kutoka nchi na taasisi mbalimbali.

Lengo la Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ni kuwapitisha Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2021/22, Mipango ya Utekelezaji wake na Maeneo ya Ushirikiano.

Akiongoza Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametaja sababu za Serikali kukutana na Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa ambao pia ni wadau wa maendeleo ili kuwajengea uelewa katika mipango na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya 2021/22 pamoja na maeneo ya Ushirikiano.

“tumeona tuweke utaratibu wa kukutana na wadau hawa wa maendeleo ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo muhimu yaliyoainishwa katika bajeti ya Serikali ili waweze kupata picha halisi ya mipango na mikakati ya Serikali katika utekelezaji wa Bajeti,” amesema Balozi Mulamula

Kwa Upande wake Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti amesema uamuzi wa Serikali wa kukutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa umekuwa mzuri sana umesaidia kufahamu mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa bajeti yake ya 2021/22.

“Kupitia mkutano wa leo tumeweza kupata picha halisi ya ushirikiano wetu na Tanzania na umezidi kuimarika lakini pia tumeweza kuona na kujadili baadhi ya vipaumbele vya bajeti ya Serikali ya Tanzania, mipango ya maendeleo jambo ambalo sisi kama wadau wa maendeleo limetuhamasisha kuendelea kushirikiana kwa ukaribu n a uwazi zaidi,” amesema Balozi Fanti   

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigula Nchema (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kutoka Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, Pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji Mhe. William Tate Olenasha (Mb).  

Pamoja na Mambo mengine, Mawaziri hao wamepata fursa ya kutoa ufafanuzi katika maeneo yanayohusu wizara zao ikiwa ni pamoja na mipango ya Serikali katika kukuza uchumi, kukusanya mapato, kukuza Viwanda, kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji, kukuza utalii na jinsi Serikali inavyojipanga kuboresha sekta ya afya nchini hasa katika kupambana na janga la UVIKO 19. 

Baadhi ya Mawaziri walioshiriki katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mbinu za pamoja za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19. Aliyevaa kitenge katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongoza Mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 

Sehemu ya Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini wakifuatilia Mkutano 


Balozi wa Canada hapa nchini, Mhe. Pamela O'Donnell akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22  

Balozi wa Kenya hapa nchini, Mhe. Dan Kazungu akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Mhe. Christine Musisi akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  

 

Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  

Balozi wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Charles Karamba akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na waandishi wa habari leo Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  


Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  





Saturday, July 10, 2021

CHODOTA; MIRADI YA MIUNDOMBINU INAYOTEKELEZWA NCHINI ITACHAGIZA KASI YA USTAWI WA EAC


Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameleza kuwa, utekelezaji wa miradi ya nishati ya umeme na barabara inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini itachagiza ustawi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa itarahishisha shughuli za usafirishaji na upatikanaji wa huduma. 

Bw. Chodota ameeleza haya alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kutembelea miradi ya Kikanda ya Miundombinu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopitishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayohusisha Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydropower Project), Utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi –Lungalunga), Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR, na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Holili, jijini Tanga. Bw. Chodota amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea hali ya utendaji na hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki katika kiwango cha lami unahusisha barabara yenye urefu wa Kilomita 245 kwa upande wa Tanzania, ambayo itaanzia Bagamoyo hadi Makurunge, Tanga. Utekelezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu nne tayari umeshaanza. Mfano, ujenzi unaoendelea sasa wa sehemu ya kwanza ya barabara hii kutoka Pangani (Tanga) hadi Mkange (Pwani) yenye jumla ya kilomita 50. Barabara hii inatarajiwa kuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na Nchi zingine za Afrika Mashariki.

Bw. Chodota ameeleza kuwa miradi hii pindi itakapo kamilika inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa nishati ya umeme wa kutosha, kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini na katika Jumuiya kwa kuwa itarahisisha zaidi usafirishaji wa bidhaa hususani baina ya Tanzania na Kenya na upatikanaji wa huduma za jamii kwa urahisi na haraka. Sambamba na hayo, Bw. Chodota ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika ujenzi wa miradi mikubwa nchini hususani katika Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, ambapo asilimia 89% ya wataalam ni Watanzania.

Katika ziara hiyo Bw. Chodota ambaye ameambatana na baadhi ya Watalaam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wamevutiwa na kasi na ubora wa kazi katika utekelezaji wa miradi yote iliyotembelewa.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere. 
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea mradi wa ujezi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi – Lungalunga)
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi–Lungalunga)
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa kipande cha barabara ya Tanga miji hadi Pangani.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa kwenye ziara ya kutembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wakiangalia ukarabati wa jengo la Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.

Friday, July 9, 2021

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KENYA BALOZI RAYCHELLE OMAMO AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA UHURU KENYATTA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Balozi Wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dany Kazungu (kushoto) na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. John Simbachawene (kulia) wakati wakimsubiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo anayetarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa Nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo mara baada ya kuwasili Nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo katika mazungumzo ya faragha kabla ya kuanza kwa mazungumzo rasmi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine na Viongozi,Maafisa waandamizi wa Wizara za Mambo ya Nje wa Kenya na Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) barua rasmi ya mualiko wa kutembelea Kenya 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo walipokutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake wa Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Wafanyabiasahara na Wajasiriamali Wanawake wa Tanzania (hawapo pichani) Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo na kushoto ni Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake. Aliyekaa Kushoto kwa Balozi Mulamula ni Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akigonga glasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo kupongezana wakati akihitimisha ziara yake ya siku moja ya kikazi hapa nchini (Aliyevaa koti ni Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) 


 

Thursday, July 8, 2021

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO 112 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA,CARIBBEAN NA PACIFIC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 112 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific  unaofanyika kwa njia ya mtandao 

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said akifuatilia mjadala katika Mkutano wa 112 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pazific unaofanyika kwa njia ya mtandao - Dar es Salaam

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said (kushoto) akiwa na Kamishna wa fedha za Nje wa Wizara ya feda na Mipango Bi Sauda Msemwa (katikati) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw. Hassan Mwamweta wakifuatilia mjadala katika Mkutano wa 112 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pazific unaofanyika kwa njia ya mtandao - Dar es Salaam




 

TANTRADE, BALOZI ZA TANZANIA ZAELEKEZWA KUTANGAZA FURSA ZA BIASHARA

Na Mwandishi wetu, Dar

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeelekezwa kushirikiana na Balozi za Tanzania katika kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji hapa nchini.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

“…………….Balozi zetu zina uhusiano wa karibu na TanTrade ambapo TanTrade moja kati ya majukumu yake ni kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata taarifa sahihi ili kusaidia kujua ni bidhaa gani za Tanzania zinaweza kuuzwa nje kwa urahisi lakini pia kujua ni nchi husika yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” amesema Balozi Fatma 

Balozi Fatma ameongeza kuwa ili bidhaa za Tanzania ziendelee kuuzwa katika masoko ya kimataifa ulimwenguni, TanTrade iendelee kushirikiana kwa karibu na Balozi za Tanzania katika kuhakikisha kuwa inatoa taarifa sahihi za bidhaa.

“Ushirikiano baina ya TanTrade na Balozi zetu uendelee kuimarishwa ili kuwawezesha wafanyabiashara kupata taarifa sahihi na kwa wakati, lakini pia ushirikiano huu utasaidia kutangaza fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania katika Mataifa ya Kigeni,” amesema Balozi Fatma

Balozi Fatma pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya maonesho ya Sabasaba kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika maonesho hayo ili kujua ni kwa namna gani wataweza kunufaika na fursa za kuuza bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa

“Kupitia maonesho haya watanzania watumie fursa hii kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika maonesho haya, lakini pia kuangalia ni namna gani watanufaika na fursa za kuuza bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa,” Amesema Balozi Fatma Rajab. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akipokea nakala ya Jarida la Diplomasia linalochapishwa na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akimsikiliza mtumishi wa Wizara alipokuwa akimpatia maelezo juu ya baadhi ya viongozi (Mawaziri) waliohudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tangu mwaka 1961 hadi sasa mwaka 2021


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akiongea na waandishi wa habari wakati alipokuwa katika banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 


Afisa kutoka Tume ya Utalii Zanzibar akimfafanulia jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea banda la tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 


Afisa kutoka Bodi ya Mapato Zanzibar akimuelezea jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam