Na mwandishi wetu, Dar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) amemuaga Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul ambaye amemaliza
muda wake wa uwakilishi.
Balozi
Mulamula amempongeza Balozi Verheul kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha
uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uholanzi na Tanzania wakati wote wa uwakilishi
wake hapa nchini.
“Tanzania
tunakuahidi ushirikiano lakini pia tunakutakia kila la kheri katika maisha yako
nje ya Tanzania na ni imani yangu kuwa utakuwa balozi mzuri wa Tanzania
duniani," Amesema Balozi Mulamula
Balozi
wa Uholanzi aliyemaliza muda wake wa Uwakilishi Mhe. Verheul ameishukuru Tanzania
kwa ushirikiano iliompatia wakati wote alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya
uwakilishi hapa nchini.
“Nawashukuru
sana kwa ushirikiano mlionipatia wakati wote niliokuwa hapa nikitekeleza
majukumu yangu kama Balozi, hakika nilifarijika sana……….Ninawaahidi kuwa balozi
mwema kote niendako,” Amesema Balozi Verheul
Katika
tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Falme
za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi katika Ofisi
Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao walijadili masuala ya kukuza, kuimarisha na
kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na UAE.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul wakati wa
hafla ya kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini katika
Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo
za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Libarata
Mulamula akimkabidhi moja kati ya zawadi Balozi wa Uholanzi nchini aliyemaliza
muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Jeroen Verheul
Balozi
wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi
akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Libarata Mulamula wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akiongea
na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed
Al-Marzooqi wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Libarata Mulamula na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini Mhe.
Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi yakiendelea