Monday, October 10, 2022

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA RAIS RUTO IKULU DAR ES SALAAM

Mkuu wa Itifaki Tanzania Balozi Yusuph Mndolwa akiwa na Mkuu wa Itifaki Kenya Balozi Betty Cherwon wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto nchini  

 
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akizungumza wakati wa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan walipokutana Ikulu Dar es Salam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto  walipokutana Ikulu jijini Dar es Salaam   

Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (katikati) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Dkt. Alfred Mutua (kushoto) wakati wa mazungumzo rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam 










 

RAIS DKT. RUTO ALIPOWASILI IKULU DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungno Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe Haroun Ali Suleiman alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene  alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Azizi alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.


 

 

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Ruto na mke wake Mama Rachel Ruto wako nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili waliwasili nchini tarehe 09/10/2022 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akiwa Ikulu Mhe. Dkt. Ruto alifanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na baadaye walikuwa na mazungumzo rasmi ambayo yalihudhuriwa na wajumbe wa pande zote mbili.

Viongozi hao walipomaliza mazungumzo yao walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia walichojadili kwa umoja wao.

Baadaye viongozi hao walielekea katika ukumbi maalum ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliandaa dhifa malum kwa ajili ya mgeni wake Mhe. Rais Ruto.

Baada ya dhifa hiyo Mhe. Rais Ruto na ujumbe wake waliondoka nchini kurejea Kenya.

Sunday, October 9, 2022

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

 

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege alipowasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Tracy-Chantelle Mmbando alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini

 

 


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na Mke wake Mama Rachel Ruto wakizungumza na watoto Joseph Mmbando  na Tracy-Chantelle Mmbando baada ya kupokea maua  walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini



Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na mmoja wa maafisa waliofika ukatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea alipowasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakielekea katika chumba cha mapumziko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (kulia) Mama Rachel Ruto (wa pili kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Alfred Mutua (wa kwanza kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchin.




 

 

 



Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili. Mhe. Dkt. Ruto ambaye ameambatana na mke wake Mama Rachel Ruto, amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam Mhe. Dkt. Ruto alikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kuelekea hotelini kwa mapumziko.

Tarehe 10 Oktoba 2022 asubuhi, Mhe. Dkt. Ruto atawasili katika Ikulu ya Dar es salam ambapo atpokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao watakuwa na mazungumzo rasmi ambayo yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili.

Baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo rasmi viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na walichojadili katika ziara hiyo na baadaye watahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuandalia mgeni wake Mhe. Dkt. Ruto.

baada ya kumalizika kwa Dhifa hiyo ya Kitaifa, Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka kurejea nchini Kenya.


TAARIFA KWA UMMA: RAIS RUTO KUWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI


 

Friday, October 7, 2022

DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.  Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.  Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), amekutana na kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.  Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Mhe. Mkingule alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Mhe. Waziri na kumpongeza kufuatia uteuzi alioupata hivi karibuni na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Mhe. Mkingule pia alipokea maelekezo kutoka kwa Mhe. Waziri Dkt. Tax tayari kuelekea katika kituo cha kazi nchini Zambia.

DKT. TAX AWATAKA WATUMISHI KUCHAPA KAZI KWA BIDII NA KUSHIRIKIANA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa amepokea shada la maua kutoka kwa Bi. Theresia Msendo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alipowasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz alipowasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma

Naibu Waziri  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kulia) akizungumza katika kikao cha katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (hawapo pichani) kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula. Kushoto ni Mhe. Balozi Mbarouk, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kilichofanyika mtumba jijini Dodoma


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Alex Mfungo akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati ya Mhe. Dkt. Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mulamula kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akikibidhi rasmi Ofisi kwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bi Mariam Haji Mrisho akitoa neno la shukurani katika hafla ya Makabidhino ya Ofisi kwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakifuatilia hafla ya Makabidhino ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula (hawapo pichani) iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakifuatilia hafla ya Makabidhino ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula (hawapo pichani) iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara baada ya kukamilika kwa hafla ya Makabidhino ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara baada ya kukamilika kwa hafla ya Makabidhino ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma

 

 

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewataka watumishi wa Wizara kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi na kushirikiana ili kufikia matarajio ya serikali na wananchi kwa ujumla.

Dkt. Tax ametoa rai hiyo leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.

Dkt. Tax amesema watumishi wa Wizara wanatakiwa kuhakikisha wanatumia weledi na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ya Wizara ili kuleta tija na ufanisi wakati wote.

“Sisi ni timu ya ushindi, tuendelee kuchapa kazi, nitashirikiana na watumishi wote wa Wizara, kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa viwango na kwa muda sahihi, tuwe wabunifu na tujitahidi kufanya kazi kama timu ili kufikia matarajio ya Serikali yetu na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Dkt. Tax

Ameongeza kuwa kazi ya kukuza uhusiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali, Jumuiya za kikanda na kimataifa haiwezi kufanikiwa ikiwa watumishi hawatashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kama timu huku wakizingatia weledi, uzalendo na ubunifu kwa maslahi mapana ya taifa.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Balozi Liberata Mulamula amewashukuru Watumishi wa Wizara kwa ushirikiano waliompatia alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao ulimuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

“Nimeacha timu imara nawashukuru wote kwa ushirikiano mlionipatia na niwaombe muendelee na moyo huohuo katika kufanikisha majukumu ya wizara,” alisema Balozi Mulamula.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbrouk Nassor Mbarouk amemshukuru Balozi Mulamula kwa ushirikiano aliompatia katika kipindi chake na kumsihi aendelee kushirikiana nao kwa kuzingatia hazina kubwa ya uzoefu na ujuzi alionao katika sekta ya mambo ya nje.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alisema Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kumuahidi Dkt. Tax kuwa watumishi wako imara na wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na hivyo kuleta tija kwa wizara na taifa kwa ujumla









Thursday, October 6, 2022

TANZANIA, INDIA KUIMARISHA SEKTA YA UCHUMI

Tanzania na India zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika sekta ya uchumi hususan kuendeleza miradi ya maendeleo ya kiuchumi, kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo pamoja na ujenzi wa viwanda.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine alipokutana kwa Mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje India, Mhe. Dammu Ravi leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

“Tumekubaliana kuwa ni wakati muafaka wa kuongeza ushirikiano wa kiuchumi, hasa kwa kuwa na miradi ya ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo kuwa na viwanda vitakavyojengwa nchini na kuanza kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo awali zilikuwa zinapatikana nchini India,” amesema Balozi Sokoine.

Viongozi hao pia wamejadili namna ya kuwekeza katika maeneo maalumu ya kibiashara ambapo kutakuwa na uzalishaji wa bidhaa kwa masoko ya nje na ya ndani na kuendeleza falsafa ya Tanzania ya Viwanda. 

“Tanzania inamakubaliano na India ya kushirikiana katika masuala ya teknolojia hususan Tehama ambapo hadi sasa India imekubali kuanzisha tawi la Taasisi ya Tehama nchini Tanzania na taasisi hiyo inategemewa kuanza kutoa mafunzo mwakani, ameongeza Balozi Sokoine.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje India, Mhe. Dammu Ravi amesema wamekubaliana namna ya kushirikiana na kuimarisha sekta ya uchumi hususan biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande zote mbili.

Serikali ya India inaamini kuwa Tanzania inaweza kuisaidia katika uwekezaji wa viwanda vikubwa zaidi lakini pia kwa kuwekeza Tanzania, ni rahisi ya kulifikia soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki…….“tunataka kuwaleta wawekezaji kutoka India na kuja kuwekeza katika viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa Tanzania,” amesema Mhe. Ravi

Mhe. Ravi ameongeza kuwa endapo Serikali ya Tanzania itawapatia eneo maalumu la biashara (Special Economic Zone) la uwekezaji ambalo litasaidia kushawishi wawekezaji kutoka India kuja kuwekeza nchini.  

Mwezi Agosti, 2022, Tanzania na India ziliahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano ikiwemo kuhakikisha sekta za afya na nyingine zinaimarika ikiwemo kilimo.

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje India, Mhe. Dammu Ravi akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje India, Mhe. Dammu Ravi leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje India, Mhe. Dammu Ravi yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika picha ya pamoja na Ujumbe wa India unaoongozwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje India, Mhe. Dammu Ravi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Tuesday, October 4, 2022

PAPA FRANCIS AMTUNUKU MTANZANIA NISHANI YA HESHIMA

Baba Mtakatifu Papa Francis amtunuku Padre Richard Mjigwa, C.PP.S., kutoka Tanzania Nishani ya Msalaba wa Kanisa na Papa kutokana na huduma ya mawasiliano ya Kanisa kupitia Radio Vatican Idhaa ya Kiswahili.

Padre Mjigwa pia anahudumu katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican ni mtanzania wa pili kutunukiwa Nishani hiyo baada ya miaka 6 tangu Mtanzania wa kwanza aliyehudumu katika Baraza hilo, Mama Thabita Janeth Mhella kutunukiwa Nishani hiyo mwezi Septemba 2016. 

Padre Mjigwa ambaye ni Mwanashirika wa Shirika la Damu Azizi, alikabidhiwa Nishani hiyo na Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano la Kipapa, Dkt. Andrea Tornielli kwa niaba ya Papa Francis kufuatia juhudi zake za kuhudumia jamii katika kueneza sauti na miongozo ya Papa katika lugha ya Kiswahili kupitia Radio Vatican kwenye mataifa yanayozungumza lugha hiyo. 

Padre Mjigwa aliyezaliwa Tanzania mwaka 1964 alianza shughuli ya huduma ya uandishi wa habari kama mshirika mnamo mwaka 1994 hadi 1999 na baadaye kuanza rasmi katika Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican kuanzia mwaka 2008 hadi sasa. 

Katika hatua nyingine, Padre Mjigwa kwa niaba ya Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican alipokea Nishani ya maadhimisho ya miaka 30 ya Idhaa hiyo ambayo ilianzishwa rasmi Tarehe 27 Septemba 1992. Tuzo hiyo ameipokea wakati muafaka ambapo Lugha ya Kiswahili imeendelea kutambulika duniani kama lugha kuu mojawapo ya mawasiliano. 

Utangazaji katika lugha ya Kiswahili kwenye Radio Vatican ulianza mapema mwezi Novemba 1961 baada ya Wamisionari wa Afrika (White Fathers) kuanza kuandaa makala kwa lugha ya Kiswahili kufuatia uzinduzi uliofanywa na Papa Mtakatifu Yohane XXIII na kupelekea kurushwa matangazo hayo ya kila siku kwa Afrika.


Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano la Kipapa, Dkt. Andrea Tornielli akimkabidhi Nishani ya Msalaba wa Kanisa na Papa, Padre Richard Mjigwa, (C.PP.S.) kutoka Tanzania kutokana na huduma ya mawasiliano ya Kanisa kupitia Radio Vatican Idhaa ya Kiswahili

Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano la Kipapa, Dkt. Andrea Tornielli akimpongeza Padre Richard Mjigwa, (C.PP.S.) kutoka Tanzania baada ya kupokea Nishani ya Msalaba wa Kanisa na Papa, kutokana na huduma ya mawasiliano ya Kanisa kupitia Radio Vatican Idhaa ya Kiswahili

Picha ya pamoja 



TANZANIA YACHAGULIWA MJUMBE WA BARAZA LA ITU

Tanzania imefanikiwa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) katika uchaguzi uliofanyika wakati wa mkutano mkuu wa ITU jijini Bucharest, Romania leo, tarehe 3 Oktoba 2022. Tanzania imepata kura 141 kati ya kura 180 zilizopigwa na nchi wanachama wa Shirika hilo. 

Baraza la ITU husimamia shughuli za Shirika katika kipindi cha kati ya mikutano mikuu ambayo hufanyika kila baada ya miaka 4.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu uliongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Mnauye (Mb) na kujumuisha maofisa waandamizi wengine kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mashirika na Taasisi za Mawasiliano nchini.

Kwa kuchaguliwa kwake, Tanzania sasa itakuwa mjumbe wa Baraza la ITU kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Ushindi huu ni mafanikio makubwa kwa Tanzania na ni kielelezo cha kazi nzuri anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan katika medani ya kimataifa na hivyo kuifanya nchi iweze kukubalika na kuaminiwa. 

Ushindi huu pia ni matokeo ya kampeni ya kimkakati iliyoendeshwa na Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa - Geneva. Aidha, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Taasisi zilizopo chini yake zilizifanya kazi kubwa ya kampeni na kutoa raslimali muhimu kwa ajili hii. 

Itakumbukwa kuwa Tanzania iliwahi kuwa mjumbe wa Baraza hili kabla ya kushindwa katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2018, Dubai UAE.

Miongoni mwa faida za kuwa mjumbe wa Baraza la ITU ni pamoja na:

• Kuwa katika nafasi nzuri ya kutambua fursa zilizopo na hatimaye kunufaika na misaada na huduma zinazotolewa na Mashirika na pia kupata taarifa muhimu za miradi na shughuli za ITU kwa urahisi na haraka

• Kujua na kuratibu mwenendo wa teknolojia mpya ili kuandaa njia za utatuzi wa changamoto zake.

• Kukuza uwezo wa kiutendaji wa wataalamu nchini wanaoshiriki katika shughuli za Baraza ikiwa ni pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu na nchi nyingine katika masuala mbalimbali.

• Kupata fursa ya kupokea na kuchambua taarifa mbalimbali za utendaji wa ITU, kutoa mapendekezo na kuboresha mwenendo wa Umoja. 

• Kuwasilisha mapendekezo ya nchi juu ya uendeshaji wa ITU.

• Kushawishi maamuzi yatolewayo na Baraza yasiwe na matokeo hasi kwa sekta ya mawasiliano.

• Kuitangaza nchi na kuchangia maendeleo ya sekta ya mawasiliano barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Mnauye (wa pili kutoka kulia) ukisubiri kutangazwa kwa matokeo ya kura ya uchaguzi wa Baraza la Shirika la Mawasiliano (ITU). Wengine katika picha, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza na kushoto kwa Mhe. Waziri Nape ni Katibu Mkuu wa Wizara ya  Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Ujumbe wa Tanzania ukishangilia ushindi baada ya kutangazwa kwa matokeo
Picha ys pamoja ya ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa ITU, Bucharest, Romania