|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba wakizindua
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa wakikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba kwa ajili ya kuzindua Ubalozi huo katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole na kushoto ni Mke wa Mhe. Dkt. Mwinyi Mama Mariam Mwinyi
|
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba wakati wa hafla
ya uzinduzi wa ubalozi huo iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa
akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba
2023 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Ubalozi huo Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amesema kufunguliwa kwa
Ubalozi huo mwaka 2019 kunaonesha nia ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha uhusiano
wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kujibu kitendo cha Cuba
ilipofungua Ubalozi wake nchini mwaka 1962.
“kufunguliwa
kwa Ubalozi huu mwaka 2019 kunaonesha nia ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha uhusiano
wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kujibu kitendo cha Cuba
ilipofungua Ubalozi wake nchini mwaka 1962,” alisema Dkt. Mwinyi.
Amesema
kufunguliwa kwa ubalozi huo mwaka 2019 kunarahisisha uratibu wa shughuli za
nchi zetu katika kuimarisha ushirikiano wa maendeleo ya kijamii na kuwaletea
maendeleo wananchi wa nchi hizo.
Dkt.
Mwinyi ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Serikali ya Jamhuri ya Cuba
kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Havana tangu ulipoanzishwa
mwaka 2019 hadi wakati huu kitu ambacho kimeuwezesha Ubalozi huo kutekeleza
majukumu yake kwa ufanisi.
“Kwa
niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namshukuru Mhe. Waziri wa
Mambo ya Nje wa Cuba, Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Serikali ya Jamhuri ya Cuba
kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi huu tangu mwaka 2019 ulipofunguliwa,
kitendo hicho kimeuwezesha Ubalozi wetu kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,”
alisema Dkt. Mwinyi.
Akiongea
katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes
Mesa amesema Serikali ya Jamhuri ya Cuba inauthamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake
na Tanzania na itaendelea kufanya hivyo kwani uhusiano uliopo ni wa kindugu na wa
kihistoria na kufanya hivyo ni kuwaenzi waanzilishi wa mataifa hayo.
“Mhe.
Rais na Wananchi wote wa Tanzania, Serikali ya Cuba inauthamini uhusiano na
ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania na itaendelea kuuthmini, uhusiano wetu
ni wa Kindugu na wa kihistoria na kufanya hivi ni kuwaenzi waanzilishi wa
mataifa yetu,” alisema Mhe. Mesa
Mhe
Mesa amesema Serikali ya Cuba inaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi
wake wa kufungua Ubalozi nchini Cuba na kuahidi kuendelea kushirikiana na
Tanzania na kuuwezesha Ubalozi huo kufanya kazi na kufikia malengo ya kuanzishwa
kwake.
Akizungumza
awali Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole amesema Tanzania itaendelea
kuimarisha uhusiano wake na Cuba uhusiano ambao ni wa kindugu na hasa
ikizingatiwa kuwa Cuba ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kuanzisha uhusiano wa
kidiplomasia na Tanzania.
Amesema
Tanzania imeendelea kushirikiana na Cuba katika sekta ya Afya na elimu ambapo wamekuwa
wakibadilishana wataalamu kuanzia miaka ya 1960 hadi nyakati hizi kwa
ajili ya kusaidia jamii za kitanzania katika eneo hilo.
Uzinduzi
wa Ubalozi huo wa Tanzania Havana uliofunguliwa
mwaka 2019 ulihudhuriwa na Jumuiya ya Wanadiplomasia mbalimbali walioko
jijini Havana.