Wednesday, September 27, 2023
WAZIRI BYABATO AHIMIZA KASI NA UFANISI WA PROGRAMU NA MIRADI INAYOTEKELEZWA JIJINI MWANZA KUPITIA LVBC
Tuesday, September 26, 2023
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA CANADA
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.January Makamba
(Mb.) akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas
katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.January Makamba
(Mb.) akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas
katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.January Makamba katika picha na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas
walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.January Makamba katika picha na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas
walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba
(Mb.) amekutana na kuzungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas
katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao
wamejadiliana njia za kuendelea kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia kati
ya Tanzania na Canada.
Mhe. Balozi Nunas pia ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Jukwaa la Chakula (AGRF) uliofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Septemba 2023.
Monday, September 18, 2023
Saturday, September 16, 2023
NAIBU WAZIRI BYABATO AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA BIASHARA WA JAMAICA
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina John Smith pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea kuridhishwa kwao na hali ya uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Jamaica na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi ili kuimarisha uhusiano huo.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Byabato amemuelezea Mhe. Smith kuwa Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo na kuongeza kuwa kuna haja ya kuhakikisha uhusiano huo wa kidplomasia unaimarishwa na kufikia hatua ya juu.
Amemuhakikishia utayari wa Serikali ya Tanzania kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Jamaica katika maeneo yatakayozinufaisha pande zote mbili.
Pia amemuelezea nia ya Tanzania kupanua wigo wa maeneo ya ushirikiano na kuingiza sekta za uchumi wa buluu, biashara na uwekezaji.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Smith alisema pamoja na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania, Jamaica inaiomba Tanzania kuiunga mkono katika nafasi mbili inazogombea kimataifa katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Bahari (IMO) na Kamati ya Urithi wa Dunia iliyo chini ya UNESCO.
DKT. MWINYI AHUTUBIA MKUTANO WA NCHI ZA KUNDI LA G77+CHINA
Washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China katika picha ya pamoja jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023 Washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China katika picha ya pamoja jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amehutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundo la G77+ China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akihutubia katika Mkutano huo,
Dkt. Mwinyi amesema Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni nguzo muhimu
kwa nchi zinazoendelea kujiletea maendeleo ya kiuchumi
na kuongeza kuwa nchi hizo zinaweza kuendelea kiuchumi kupitia maendeleo katika
sekta muhimu za kilimo,
nishati, elimu, afya, madini, maendeleo ya muindombinu, maji
na mazingira.
Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amekumbusha namna nchi zinazoendelea
zilivyoathirika na janga la maradhi ya UVIKO-19, bidhaa kupanda bei, mizozo ya kisiasa na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza kuwa baadhi ya changamoto zilisababisha
kupanda kwa gharama za maisha na kudhoofisha jitahada za kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Dkt. Mwinyi alikumbushia namna nchi
zilizoendelea zilivyobanwa na teknolojia ya kutengeneza
chanjo na kunyimwa msaada wa kiteknolojia ili zitengeneze chanjo zao na kusababisha kampuni za kutengeneza dawa za mataifa
tajiri kupata faida kubwa kwa kuziuzia nchi zinazoendelea
chanjo ya
UVIKO-19.å
Mhe.Dkt. Mwinyi amezitanabaisha nchi za kundi la
G77+China kuchukua changamoto
hizo kama somo na
zisibweteke kusubiri msaada kutoka mataifa yaliyoendelea.
Mkutano huo unaofanyika jijini Havana nchini Cuba tarehe 15-16 Septemba 2023 unayakutanisha mataifa yanayoendelea unajadili changamoto zinazoikabili dunia baada ya kuathirika na janga la UVIKO-19 na migogoro inayoendelea duniani na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi.
Mkutano huo umejikita kutafuta namna bora ya kujenga ustahimilivu kupitia maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu ili kundi la G77+China liweze kufikia malengo yake kwa pamoja.
Kaulimbiu ya Mkutani inasema, “Changamoto za Maendeleo: Nafasi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu”.
Friday, September 15, 2023
TANZANIA ITAENDELEA KUHESHIMU MISINGI YA MTANGAMANO, DKT. BITEKO
Kamishina wa Miundombinu na Nishati wa Umoja wa Afrika, Bibi Amani Abou-Zeid akihutubia Kikao cha Umoja wa Afrika cha Nne cha Kamati Maalumu ya Kitaalam kuhusu Uchukuzi, Miundombinu ya Kikanda na ya Bara, na Nishati kinachofanyika mjini Zanzibar
Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Erick Ngilangwa na Bi. Maria Ndumbalo wakifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi |
Wajumbe wakisikiliza hotuba za ufunguzi |
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiagana na baadhi ya wajumbe wanaoshiriki Kikao cha Umoja wa Afrika cha Nne cha Kamati Maalumu ya Kitaalam kuhusu Uchukuzi, Miundombinu ya Kikanda na ya Bara, na Nishati baada ya kufungua kikao hicho |
TANZANIA ,CUBA ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA ELIMU YA JUU NA KUFUNDISHA KISWAHILI NCHINI CUBA
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Waziri wa Elimu ya Juu wa Cuba Mhe. Dkt. Walter Garcia wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba kupitia elimu ya juu |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Waziri wa Elimu ya Juu wa Cuba Mhe. Dkt. Walter Garcia wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano waliyosaini kati ya Tanzania na Cuba kupitia elimu ya juu |
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Prof. William Anangisye na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Havana Prof. Miriam Garcia wakionesha Hati ya Makubaliano waliyosaini ya ushirikiano kati ya vyuo hivyo katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Havana nchini Cuba tarehe 14 Septemba 2023 |
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Cuba zimesaini Hati za Makubaliano ya kushirikiana kupitia elimu ya juu, kubadilsihana wakufunzi na wanafunzi na kufundisha lugha ya kiswahili nchini Cuba na kutengeneza kamusi ya kiswahili na kihispaniola.
Makubaliano hayo yamesainiwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana na kushuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa.Makubaliano hayo yamesainiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Waziri wa Elimu ya Juu wa Cuba Mhe. Dkt. Walter Garcia.
Makubaliano mengine yaliyosainiwa ni kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salam kilichowasilishwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. William Anangisye na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Havana Prof. Miriam Garcia
Katika makubaliano hayo Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana katika masuala ya kubadilishana ujuzi na uzoefu kupitia wahadhiri, wanafunzi, masuala ya utafiti, sayansi, teknolojia, kufundisha lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Havana na kutengeneza kamusi ya lugha ya Kiswahili na Kispaniola ili kusambaza matumizi ya kugha ya kiswahili nchini Cuba na nchi nyingine zinazozungumza lugha ya kispaniola.
Akizungumza katika hafla ya utuaji saini makubaliano hayo Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole amesema Ubalozi wa Tanzania Havana unajivunia kusainiwa kwa makubaliano hayo ambayo yanatoa mwongozo maalum wa jinsi ya kutekeleza mpango wa kufundisha lugha ya Kiswahili nchini humo.
"Haya ni mafanikio makubwa kwetu, Ubalozi wa Tanzania Havana unajivunia kusainiwa kwa makubaliano haya, sasa yatatoa mwongozo maalum utakaowezesha taasisi husika za elimu ya juu kutekeleza kikamilifu mpango wa kusambaza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Cuba," alisema Mhe. Balozi Polepole.
Makubaliano yaliyosainiwa ni kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Cuba ambapo Chuo Kikuu cha Havana kilikubaliana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kushirikiana katika masuala ya utafiti, sayansi na Teknolojia na kufanya kazi kwa pamoja ili kutunga Kamusi ya Kiswahili na Kihispaniola.
Makubaliano mengine yaliyosainiwa ni kati ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknojia na Wizara ya Elimu ya Juu ya nchini Cuba ambayo yatawezesha ubadilishanaji wa wanafunzi, wahadhiri na watafiti katika eneo la sayansi na teknolojia ili kuwawezesha wahusika kubadilishana ujuzi na uzoefu katika maeneo hayo na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa pande zote mbili.
DKT. MWINYI AZINDUA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CUBA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba wakizindua Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa wakikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba kwa ajili ya kuzindua Ubalozi huo katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole na kushoto ni Mke wa Mhe. Dkt. Mwinyi Mama Mariam Mwinyi |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ubalozi huo iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023.
Akizungumza katika uzinduzi wa Ubalozi huo Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo mwaka 2019 kunaonesha nia ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kujibu kitendo cha Cuba ilipofungua Ubalozi wake nchini mwaka 1962.
“kufunguliwa kwa Ubalozi huu mwaka 2019 kunaonesha nia ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kujibu kitendo cha Cuba ilipofungua Ubalozi wake nchini mwaka 1962,” alisema Dkt. Mwinyi.
Amesema kufunguliwa kwa ubalozi huo mwaka 2019 kunarahisisha uratibu wa shughuli za nchi zetu katika kuimarisha ushirikiano wa maendeleo ya kijamii na kuwaletea maendeleo wananchi wa nchi hizo.
Dkt. Mwinyi ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Serikali ya Jamhuri ya Cuba kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Havana tangu ulipoanzishwa mwaka 2019 hadi wakati huu kitu ambacho kimeuwezesha Ubalozi huo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namshukuru Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Serikali ya Jamhuri ya Cuba kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi huu tangu mwaka 2019 ulipofunguliwa, kitendo hicho kimeuwezesha Ubalozi wetu kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,” alisema Dkt. Mwinyi.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa amesema Serikali ya Jamhuri ya Cuba inauthamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania na itaendelea kufanya hivyo kwani uhusiano uliopo ni wa kindugu na wa kihistoria na kufanya hivyo ni kuwaenzi waanzilishi wa mataifa hayo.
“Mhe. Rais na Wananchi wote wa Tanzania, Serikali ya Cuba inauthamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania na itaendelea kuuthmini, uhusiano wetu ni wa Kindugu na wa kihistoria na kufanya hivi ni kuwaenzi waanzilishi wa mataifa yetu,” alisema Mhe. Mesa
Mhe Mesa amesema Serikali ya Cuba inaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kufungua Ubalozi nchini Cuba na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuuwezesha Ubalozi huo kufanya kazi na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.
Akizungumza awali Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Cuba uhusiano ambao ni wa kindugu na hasa ikizingatiwa kuwa Cuba ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania.
Amesema Tanzania imeendelea kushirikiana na Cuba katika sekta ya Afya na elimu ambapo wamekuwa wakibadilishana wataalamu kuanzia miaka ya 1960 hadi nyakati hizi kwa ajili ya kusaidia jamii za kitanzania katika eneo hilo.
Uzinduzi wa Ubalozi huo wa Tanzania Havana uliofunguliwa mwaka 2019 ulihudhuriwa na Jumuiya ya Wanadiplomasia mbalimbali walioko jijini Havana.
Thursday, September 14, 2023
BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI AZUNGUMZA NA ALIYEKUWA MWAKILISHI MKAZI WA UNDP MALAWI
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Malawi, Bw. Shigeki Komatsubara ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini humo mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa Tanzania, Lilongwe hivi karibuni =================================================================== |
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola amekutana
kwa mazungumzo na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP) nchini Malawi, Bw. Shigeki Komatsubara ambaye amemaliza muda
wake wa uwakilishi nchini humo.
Lengo la mazungumzo yao ambayo yalifanyika katika Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Lilongwe hivi karibuni, lilikuwa ni kumuaga Bw.
Komatsubara na kujadili ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali.
|