Saturday, September 16, 2023

DKT. MWINYI AHUTUBIA MKUTANO WA NCHI ZA KUNDI LA G77+CHINA

 






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China akizungumza jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023

 



 


Washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China katika picha ya pamoja jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023


Washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China katika picha ya pamoja jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amehutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundo la G77+ China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Akihutubia katika Mkutano huo, Dkt. Mwinyi amesema Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni nguzo muhimu kwa nchi zinazoendelea kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kuongeza kuwa nchi hizo zinaweza kuendelea kiuchumi kupitia maendeleo katika sekta muhimu za kilimo, nishati, elimu, afya, madini, maendeleo ya muindombinu, maji na mazingira.

Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amekumbusha namna nchi zinazoendelea zilivyoathirika na janga la maradhi ya UVIKO-19, bidhaa kupanda bei, mizozo ya kisiasa na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza kuwa baadhi ya changamoto zilisababisha kupanda kwa gharama za maisha na kudhoofisha jitahada za kujikwamua kiuchumi.

 

Mhe. Dkt. Mwinyi alikumbushia namna nchi zilizoendelea zilivyobanwa na teknolojia ya kutengeneza chanjo na kunyimwa msaada wa kiteknolojia ili zitengeneze chanjo zao na kusababisha kampuni za kutengeneza dawa za mataifa tajiri kupata faida kubwa kwa kuziuzia nchi zinazoendelea chanjo ya UVIKO-19.å

Mhe.Dkt. Mwinyi amezitanabaisha nchi za kundi la G77+China kuchukua changamoto hizo kama somo na zisibweteke kusubiri msaada kutoka mataifa yaliyoendelea. 

 

Mkutano huo unaofanyika jijini Havana nchini Cuba tarehe 15-16 Septemba 2023 unayakutanisha mataifa yanayoendelea unajadili changamoto zinazoikabili dunia baada ya kuathirika na janga la UVIKO-19 na migogoro inayoendelea duniani na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi.  

 

Mkutano huo umejikita kutafuta namna bora ya kujenga ustahimilivu kupitia maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu ili kundi la G77+China liweze kufikia malengo yake kwa pamoja.

 

Kaulimbiu ya Mkutani inasema, “Changamoto za Maendeleo: Nafasi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu”.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.