|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na vijana wanaoshiriki Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani
Afrika (AGRF 2023) uliofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam
|
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na vijana wanaoshiriki Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani
Afrika (AGRF 2023) uliofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam |
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
amewaeleza vijana wanaoshiriki Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani
Afrika (AGRF 2023) kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia vyema
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ili kuboresha sekta ya Kilimo
na kukuza upatikaji wa chakula nchini.
Mhe. Dkt. Samia ametoa
kauli hiyo alipozungumza na vijana walioko katika Sekta ya kilimo kuhusu
jitihada za kukabiliana na changamoto za kutafuta masoko ya mazao ya
kilimo wanaoshiriki Mkutano wa Mifumo ya Chakula barani Afrika (AGRF
2023) unaofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 5 – 8 Septemba
2023.
Mhe. Rais amesema matumizi ya teknolojia ya kisasa katika
sekta ya Kilimo yataleta matokeo chanya na kutoleo mfano wa kutumia
trekta za ‘automatic’ na zinavyosaidia kuleta tija katika sekta ya
kilimo.
Amesema Serikali ya Tanzania inategemea kufikia mwaka
2025 kuhakikisha robo tatu ya mbegu zinazotumiwa na wakulima
zinazalishwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi mahitaji kwa kutumia ICT.
Mhe.
Samia akiongelea madhumuni ya programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT)
amesema imelenga kuwawezesha vijana kushiriki katika kilimo na kuongeza
kuwa program hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuinua maisha ya vijana na
kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini.
Rais Samia
ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine, malengo ya kimkakati ya BBT ni
kuwavuta vijana kushiriki kwenye miradi ya kilimo chenye tija na faida
kwa maisha yao.
BBT ilianzishwa mwaka 2022, na tangu
ilipoanzishwa imechukua vijana 1,252 na vijana wengine 812
wamejiandikisha kupata mafunzo hayo yanayotolewa kwa miezi minne.
Kadhalika,
Rais Samia ameongeza kuwa Tanzania imejipanga kuiendeleza sekta ya
kilimo siyo tu kwa manufaa yake bali kwa manufaa ya bara la Afrika na
Dunia kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.