Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye amewasili nchini kuhudhuria Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023.
Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam Mhe. Ndayishimiye amepokelewa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila.
Mhe. Ndayishimiye ni miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Marais na Mawaziri Wakuu wastaafu kutoka barani Afrika wanaohudhuria mkutano huo mkubwa unaojadili mifumo ya chakula duniani
|
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akiteremka kwenye ndege baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023 |
|
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023 |
|
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akizungumza na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavende baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023 |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.