Thursday, September 7, 2023

RAIS RUTO AWASILI NCHNI KUSHIRIKI AGRF 2023

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa William Ruto amewasili nchini kuhudhuria Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023.

Baada ya kuwasili nchini, Mhe. Ruto amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 

Mhe. Ruto ni miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Marais na Mawaziri Wakuu wastaafu kutoka barani Afrika wanaohudhuria mkutano huo mkubwa unaojadili Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023).

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa William Ruto akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023



Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa William Ruto akitambulishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba kwa viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa William Ruto akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.