Friday, November 24, 2023

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAJADILIANO YA JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA USALAMA WA CHAKULA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto na Rais wa Burundi Mhe. Evereste Ndayishimiye kushiriki Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha.

Mkutano huo wa ngazi ya juu wa majadiliano uliandaliwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiwa ni mkutano wa pembezoni kuelekea Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika terehe 24 Novemba 2023.

Majadiliano hayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo kuongeza Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa usalama wa chakula na mazingira endelevu kwa Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Mkutano huo wa Majadiliano ya Juu ulilenga kupata msimamo wa pamoja wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maalum kwa ajili ya Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mikataba wa Umoja wa Matanda kuhusu Mabadiliko Tabianchi (COP28) utakaofanyika kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Disemba 2020 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu

Msimamo huo wa pamoja unatarajiwa kupitishwa katika Mkutano wa 23 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2023 jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Balozi Dkt. Bernard Kibesse akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifurahia jambo na Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto alipowasili kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto akisisitiza jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evereste Ndayishimiye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akisisitiza akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula ukiendelea

Thursday, November 23, 2023

BALOZI NAIMI AWASILISHA HATI KWA RAIS WA AUSTRIA

 

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz (kulia) akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen (kushoto) tarehe 21 Novemba, 2023


Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz (kulia) akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen (kushoto) baada ya kuwasilisha  Hati za Utambulisho tarehe 21 Novemba, 2023

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz akikagua gwaride maalum alipowasili Ikulu jijini Vienna kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria tarehe 21 Novemba, 2023

 

 

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na Katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen tarehe 21 Novemba, 2023.

Baada ya kuwasilisha Hati hizo za utambulisho Serikali ya Jamhuri ya Austria ilimuahidi ushirikiano Mhe. Balozi  Aziz kwa kipindi chote atakachohudumu katika kituo hicho na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kuendelea kuimarsiha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Austria.

Naye Mhe. Balozi Aziz alishukuru na kuahidi kushirikiana na Serikali ya Austria katika utekelezaji majukumu yake na kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Austria unafikia hatua za juu

BALOZI FATMA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MAWAKALA WA AJIRA NA UONGOZI WA DIASPORA WA TANZANIA NCHINI OMAN

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab mapema wiki hii amekutana kwa mazungumzo na Mawakala wa Ajira jijini Muscat, Oman.

Balozi Fatma alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa mawakala hao ikiwa ni mkutano wake wa kwanza na Mawakala hao tangu ateuliwe kuwakilisha kituo hicho.

Pamoja na mambo mengine mazungumzo yao yalijikita katika kujadili changamoto, kupokea ushauri na kuangalia namna ya kuweka mazingira bora na yenye ufanisi katika kukamilisha mchakato wa mikataba ya ajira za kuleta Wafanyakazi kutoka Tanzania hususan wafanyakazi wa ndani.

Wakati huo huo, Mhe. Balozi Fatma alikutana na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Oman (Diaspora) kwenye mkutano uliofanyika katika makazi ya Balozi jijini Muscat, Oman. 

Lengo la mazungumzo lilikuwa ni kujitambulisha rasmi kwao na kusikiliza maoni na changamoto zinowakabili Diaspora na kujadili njia bora ya kuzitatua. 

Kadhalika, Balozi Fatma alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa ushirikiano wao ambao umewezesha kuwakutanisha pamoja Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman na pia alisisitiza umuhimu wa kuzingatia na kufuata sheria za nchi hiyo na kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuitangaza vyema.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Balozi Fatma Rajab (kulia) akizungumza na Mawakala wa Ajira wa nchini Oman (hawapo pichani) alipokutana nao jijini Muscat kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na mikataba ya ajira kwa watanzania nchini humo.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Balozi Fatma Rajab (mwenye nguo ya bluu) akizungumza na Mawakala wa Ajira wa nchini Oman alipokutana nao jijini Muscat kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na mikataba ya ajira kwa watanzania nchini humo.

Moja wa Mawakala hao akiwasilisha mchango wake katika kikao hicho.

Mkutano ukiendelea.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Balozi Fatma Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Diaspora wa Tanzania wa nchini Oman.

Picha ya pamoja.



Wednesday, November 22, 2023

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI EAC JIJINI ARUSHA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) akiteta na jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.

Mkutano huo ambao ulianza tarehe 18 Novemba 2023 kwa ngazi ya wataalam na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu umepitia na kujadili mapendekezo yatakayowasilishwa katika Kikao cha Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha tarehe 24 Novemba 2023.

Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri wa EAC pamoja na mambo mengine umejadili masuala kuhusu Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 hadi 24 Novemba, 2023; utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya kuhusu Majadiliano ya Ombi la Shirikisho la Jamhuri ya Somalia kujiunga na EAC; juhudi za utafutaji wa Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya; majadiliano kuhusu Katiba ya Fungamano la kisiasa la Jumuiya; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki; na Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri ambao ni Wajumbe kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Rwanda, Sudan Kusini na Uganda.

Kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutafuatiwa na Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC uliopangwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2023 jijini Arusha.

Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira ambao pia utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC.

Mkutano huo unalenga kupata msimamo wa pamoja wa Jumuiya ya EAC kuelekea katika Mkutano wa Kimataifa wa 28 wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) utakaofanyika kuanzia Novemba 28, 2023 nchini UAE.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha 
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukiwa umesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha
Sehenu ya ujumbe wa Sudan Kusini wakifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha 
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha 
Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Waziri Burundi anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Balozi Gervais Abayeho akifungua Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha
Sehemu ya Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha

TANZANIA YAIHAKIKISHIA UAE MAZINGIRA SALAMA YA BIASHARA, UWEKEZAJI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) mazingira salama ya biashara na uwekezaji nchini.  

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amebainisha hayo aliposhiriki katika kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam na kuwasihi kuendelea kufanya biashara na kuwekeza kwa wingi nchini.

Balozi Mbarouk alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi Imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji yanaboreshwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wengi kuwekeza nchini.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka sera imara, sheria na taratibu rafiki pamoja na kuweka misingi thabiti ya kustawisha mazingira ya biashara,” alisema Balozi Mbarouk

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Tanzania na Falme za Kiarabu zina ushirikiano mzuri wa kiuchumi katika eneo la biashara na uwekezaji ambapo UAE ni mshirika wa saba (7) wa kibiashara wa Tanzania kwa kiasi cha biashara baina ya nchi hizo kinachofikia Dola za Marekani bilioni 3.2. Kadhalika, kuhusu uwekezaji, UAE ni miongoni mwa nchi zilizowekeza kwa kiasi kikubwa nchini.

Balozi Mbarouk alipongeza juhudi za viongozi wa mataifa hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa UAE, Mheshimiwa Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, kwa uongozi wao imara wenye maono na juhudi za kuimarisha na kudumisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili 

Kwa Upande wake, Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini, Mhe. Khalifa Abdulrahman Al Marzouqi alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano baina ya UAE na Tanzania mwaka 1974, nchi hizo zimejitahidi kuendeleza na kuimarisha uhusiano huo katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Katika jitihada ya kuonesha azma ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, mikataba mbalimbali imesainiwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi zetu. Ambapo ushirikiano huu umesababisha ongezeko la kiasi cha kubadilishana biashara kati ya nchi hizi mbili kufikia Dola za Marekani Bilioni 2.2,” alisema Balozi Marzouqi

Aidha, Balozi Marzouqi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoa kwa UAE ambapo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza wakati wa hafla ya kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini, Mhe. Khalifa Abdulrahman Al Marzouqi akizungumza wakati wa hafla ya kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na viongozi mbalimbali wakishiriki katika hafla ya kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam

Mabalozi pamoja na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini, Mhe. Khalifa Abdulrahman Al Marzouqi katika hafla ya kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na viongozi mbalimbali wakishiriki katika hafla ya kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam



Tuesday, November 21, 2023

BALOZI MBUNDI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU EAC


Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.

Mkutano huo umepitia na kujadili taarifa iliyowasilishwa na timu ya Wataalamu waliokutana jijini hapo kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba 2023. Mkutano wa Makatibu Wakuu unafanyika ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Novemba 2023.
Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akifafanua jambo  kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa Makatibu Wakuu wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Sehemu ya wajumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya wakifuatilia Mkutano wa Makatibu Wakuu wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Arusha  
Mkutano wa Makatibu Wakuu wa EAC  ukiendelea
Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Makatibu Wakuu wa EAC uliokuwa ukiendelea

Monday, November 20, 2023

MKUTANO WA NGAZI YA WATAALAMU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAENDELEA JIJINI ARUSHA


Ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa Ngazi ya Wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashriki unaoendelea jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023

Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam kutoka katika Jumuiya ya Afrika Mashriki akiendesha mkutano huo unaoendelea jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023
Wajumbe kutoka Janhuri ya Uganda wakishiriki Mkutano wa Ngazi ya Wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashriki wakishiriki mkutano huo unaoendelea jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023
Ujumbe wa Tanzania ukiendelea na Mkutano wa Ngazi ya Wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashriki kuandaa Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023


Wajumbe wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashriki wakiendelea na mkutano huo kuandaa Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023

 

 

Mkutano wa Ngazi ya Wataalam kutoka katika Jumuiya ya Afrika Mashriki unaendelea jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo.


Mkutano huo ulianza tarehe 18 Novemba, 2023 unatarajiwa  kukamilisha nyaraka kwa ajili ya Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 21 Novemba 2023 na kufuatiwa na mkutano wa Baraza hilo tarehe 22 Novemba 2023.


Mkutano huo wa ngazi ya wataalam unapitia na kujadili masuala mbalimbali kuhusu Mtangamano wa Afrika Mashariki ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri kwa mapendekezo.


Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ni chombo kinachotoa miongozo ya kisera kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa uanzishwaji wake.

Mkutano wa 43 wa Baraza ulielekeza nchi wanachama, Taasisi, na Mashirika kutekeleza maamuzi yote na maelekezo yaliyosalia na kutoa taarifa ya utekelezaji wake kwenye Mkutano 44 wa Baraza hilo.

Katika kutekeleza maelekezo hayo Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikisha na Nchi wanachama, Taasisi, na Mashirika ilifanya uchambuzi wa maamuzi na maelekezo yote ambayo hayajatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na kuwasilisha taarifa hiyo kwa Baraza kwa miongozo na maelekezo.


Mkutano huo unahudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Uganda, Rwanda, na Sudan Kusini.


Baada ya kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 24 Novemba, 2023 utafanyika Mkutano wa kawaida wa 23 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya.


Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira utakaofanyika tarehe 23 Novemba, 2023






Sunday, November 19, 2023

BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAKUTANA JIJINI ARUSHA

 

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioanza tarehe 18 Novemba 2023  jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu.

 

wajumbe wa meza kuu wakiongoza Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  katika ngazi ya Wataalamu unaoendelea jijini Arusha, Mkutano huo unafanyika  tarehe 18 -20- Novemba 2023 jijini Arusha utafuatiwa na kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 21 Novemba na baadaye kufanyika mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 22 Novemba, 2023.
 

Wajumbe kutoka katika Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Rwanda na Jamhuri ya Kenya wanaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioanza tarehe 18 Novemba 2023  jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu


Wajumbe kutoka Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioanza tarehe 18 Novemba 2023  jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu

Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioanza tarehe 18 Novemba 2023  jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao

Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioanza tarehe 18 Novemba 2023  jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao
Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioanza tarehe 18 Novemba 2023  jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao

 


 

Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza jijini Arusha.

 

Mkutano huo umeanza katika Ngazi ya Wataalam wanakutana jijini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2023 na utafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 21 Novemba 2023, na kufuatiwa na Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023.

 

Mkutano wa ngazi ya Wataalam unapitia na kujadili masuala mbalimbali kuhusu Mtangamano wa Afrika Mashariki ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano wa 44 wa Baraza la  Mawaziri kwa mapendekezo.

 

Masuala yanayojadiliwa katika Mkutano huo wa wataalamu ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 - 24 Novemba, 2023; Taarifa ya utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya kuhusu; Majadiliano ya Jamhuri ya Somalia kujiunga na Jumuiya; Hatua iliyofikiwa katika kutafuta  Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo ya mchakato wa kijeshi na uongezaji muda wa mkataba wa SOFA; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya ya Afrika; majadiliano ya Katiba kuhusu Katiba ya Fungamano la  kisiasa Afrika Mashariki; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na; Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya Uandishi wa insha kwa wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Mkutano huo unahudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Uganda, Rwanda, na Sudan Kusini.

 

Baada ya kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 23 Novemba
utafanyika Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira na kufuatiwa na Mkutano wa kawaida wa 23 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya uliopangwa kufanyika jijini Arusha tarehe 24 Novemba, 2023.

 


RAIS SAMIA AMUAGA RAIS WA ROMANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemuaga Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini leo tarehe 19 Novemba 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na Rais Samia viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali wameshiriki kumuaga kiongozi huyo ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.).

Viongozi wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mgeni wake Rais wa Romania Mheshimiwa Klaus Iohannis wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika hafla fupi ya kumuaga Rais Iohannis Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Romania Mheshimiwa Klaus Iohannis akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kumuaga Rais Iohannis Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akiagana na viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini leo tarehe 19 Novemba 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam