Imeelezwa
kuwa ili Tanzania iweze kufikia malengo ya Maendeleo iliyojiwekea,
lazima iwe na Sera Bora ya Mambo ya Nje inayozingatia maoni na matakwa ya
makundi yote ya wadau nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Mhe. Ali
Suleiman Ameir ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la wadau la
kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001
lililofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05
Februari 2024.
Kongamano
hilo ambalo ni la tatu kufanyika ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kushirikisha wananchi kutoa maoni
yatakayozingatiwa katika zoezi la kurekebisha Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka
2001.
Mwenye
dhamana ya kusimamia Sera hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb)
ametaja sababu za Wizara yake kuratibu makongamano
hayo ambapo alisema linalofuata litafanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024.
Alieleza
kufanyika kwa makongamano hayo ni utekelezaji wa misingi ya utawala bora ambayo
inasisitiza umuhimu wa kushirikisha wadau katika utungaji wa Sera za nchi,
ikiwemo Sera ya Mambo ya Nje.
Alieleza
pia kuwa Sera ni Tamko linalotoa mwongozo namna nchi itakavyoshughulikia
ushirikiano na uhusiano wake na dunia. Hivyo, utungaji wa Tamko muhimu kama
hilo lazima lishirikishe wadau wote.
Mhe.
Makamba aliwambia washiriki wa Kongamano hilo kuwa Tanzania ina ushawishi
mkubwa duniani tofauti na nguvu zake za kiuchumi na kijeshi kutokana na kuwa na
Sera bora ya Mambo ya Nje. Hivyo, ili iendelee kuwa na ushawishi huo duniani
lazima itungwe Sera imara itakayozingatia maoni ya wadau wote.
Aliendelea
kueleza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ina uhusiano wa moja kwa moja na malengo ya
Maendeleo ya nchi. Hivyo, mchakato wa utungaji wa Sera ya Mambo ya Nje lazima
ushirikishe wadau kwa kuwa maendeleo ni jambo linalomgusa kila mmoja.
Alihitimisha
hotuba yake kwa kutaja baadhi ya mambo yaliyosababisha Serikali kufanya
marekebisho ya Sera hiyo. Mambo hayo ni pamoja na mabadiliko yanayotokea
duniani kama mabadiliko ya tabianchi, uvumbuzi wa teknolojia mpya, kuibuka kwa
wadau wapya wa maendeleo wenye nguvu na ushawishi na Watanzania wengi
hawakuwepo wakati wa utungaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.
Kongamano
hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Magharibi, Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Ikulu
Zanzibar, Bw. Salehe Juma Mussa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Balozi Stephen Mbundi, Naibu Katiibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said
Shaibu Mussa, Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi, Mabolozi Wastaafu akiwemo
Balozi Amina Salum Ali, viongozi wa Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Wakuu wa
taasisi za Serikali na Sekta Binafsi, Wakuu wa Vyombo vya habari, wanazuoni na
wananchi kwa ujumla.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akitoa neno wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Bw. Salehe Juma Mussa akitoa neno wakati wa Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024
|
|
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba kuhutubia Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024 |
|
Watu mbalimbali walioshiriki Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024
|
|
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akiwasilisha mada kuhusu maeneo muhimu yanayopendekezwa katika marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje |
|
Wadau mbalimbali wakifuatilia Kongamano la kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024 |