Rais wa
Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda na Mke wake Agata
Kornhouser-Duda wametembelea mradi wa matibabu ya dharura unaoendeshwa
katika hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam ili kujionea
utekelezaji wa mradi huo.
Kupitia Mradi huo Serikali ya Poland
imetoa msaada wa Dola za Marekani 1,136,703 kwa ajili ya kusaidia
utekelezaji wa mradi huo unaolenga kutoa msaada kwa sekta ya matibabu na
kusaidia elimu ya wahudumu wa afya katika mkoa wa Dar es Salaam.
Poland
pia inafadhili miradi kama hiyo katika Hospitali za Temeke,
Mwananyamala, kituo cha Afya Chamazi na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana
ya mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.