Wednesday, May 22, 2024

BALOZI KAGANDA AKUTANA NA MKURUGENZI WA UHUSIANO WA KIMATAIFA WA DJIBOUTI

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda akizungumza na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar aliyemtembelea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar akizungumza alipokutana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Kikao kikiendelea

kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda akizungumza na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar aliyemtembelea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda katika picha  na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar alipomtembelea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar na timu yake walipomtembelea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


 

 

 

 

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda amekutana na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

 

Balozi Guelleh Idriss Omar yuko nchini na Ofisi ya Uratibu wa Kitaifa ya Djibouti kuhusu Uhamiaji (BCNM) kwa ziara ya kubadilishana uzoefu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu masuala ya uhamiaji kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM)

 

Ziara hiyo inalenga kuimarisha uwezo wa wawakilishi wa Serikali ya Djibouti katika usimamizi wa uhamiaji, kubadilishana na wadau muhimu kuhusu mbinu bora za usimamizi wa uhamiaji, kuendeleza ushirikiano kati ya nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania, na kubadilishana uzoefu wa kivitendo katika usimamizi wa uhamiaji kati ya Djibouti na mamlaka za Tanzania.

Katika kikao hicho Balozi Kaganda aliithibitishia Djibouti dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kudumisha uhusiano wa karibu wa kikazi na Serikali ya Djibouti, kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano na ubia kati yan chi hizo mbili.

Naye Balozi Guelleh Idriss Omar ameshukuru nafasi ya kujifunza juu ya namna Tanzania inavyooendesha shughuli za uhamiaji wa kimataifa na uhusiano na nchi nyingine  na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili.

 

Wajumbe wengine katika ziara hiyo ni pamoja na Bi. Ifrah Ali Ahmed, Mshauri Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Mohamed Houmed Abasse, Mkuu wa Wilaya ya Tadjourah, Bw. Hassan Abdi Robleh, Mkuu wa Mkoa wa Dikhil, Bi. Amana Awaleh Oumar, anayehusika na ulinzi katika BCNM, Bi. Hasna Omara Farah, anayehusika na maendeleo katika BCNM, na Bw. Abdallah Mohamed Bourhan, Afisa Mradi wa Kitaifa (BMM) - IOM Djibouti.


Tuesday, May 21, 2024

EU KUIPATIA TANZANIA MSAADA WA BILIONI 12




Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo, akifuatilia majadiliano wakati wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ubelgiji. Kushoto kwake ni Bw. Matthias Haerynck, Mkurugenzi wa Masuala ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ubelgiji.

 

Mheshimiwa Waziri Prof. Kitila Mkumbo viongozi wengine waandamizi wa Serikali akifuatilia kwa ukaribu majadiliano katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ubelgiji.

Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead John Teri akielezea fursa mbalilmbali za uwekezaji nchini Tanzania katika Mkutano Maalumu wa Chemba ya Biashara ya Ubelgiji, Luxembourg na Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (CBL-ACP). 


Ujumbe wa Tanzania katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji ukitembelea kampuni ya Frisonat inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za chuma

Ujumbe wa Tanzania katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji ukitembelea shamba la mfano katika Chuo cha Ghent

Waziri Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo(Mb) akishiriki katika jopo maalumu kwenye Mkutano wa Ngazi za Juu kuhusu madini ya Kimkakati



Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki ziara ya kutembelea shamba la mfano katika Chuo Kikuu cha Ghent pamoja na Kampuni ya Frisonat inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za chuma. 

Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead John Teri akielezea fursa mbalilmbali za uwekezaji nchini Tanzania katika Mkutano Maalumu wa Chemba ya Biashara ya Ubelgiji, Luxembourg na Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (CBL-ACP). 

Makamu wa Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) akikabidhi zawadi maalumu kwa Rais wa Chemba ya Biashara ya Ubelgiji, Luxembourg na ACP (CBL-ACP) 


Mheshimiwa Waziri Prof. Kitila Mkumbo viongozi wengine waandamizi wa Serikali akifuatilia kwa ukaribu majadiliano katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ubelgiji.


Waziri Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi, Mipango na Uwekezaji akiongoza ujumbe wa Tanzania na wageni wengine katika hafla maalumu ya kumbukizi ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika sambamba na Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ubelgiji

Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama, Mbunge wa Jimbo la Madaba na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ambao walishiriki kwenye Kongamano wakijadiliana jambo.


Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi, Mipango na Uwekezaji akifuatilia kwa ukaribu majadiliano katika Mkutano wa Ngazi za Juu kwenye Masuala ya Madini ya Kimkakati 


Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi, Mipango na Uwekezaji akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Koen Doens, Mkurugenzi wa Ubia wa Kimataifa wa Umoja wa Ulaya baada ya mazungumzo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Bw. Kheri Mahimbali, akieleza fursa mbalimbali katika sekta ya madini wakati wa kikao baina ya ujumbe wa Tanzania na makampuni makubwa ya madini ndani ya Umoja wa Ulaya 

Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead John Teri akielezea fursa mbalilmbali za uwekezaji nchini Tanzania katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ubelgiji








Sunday, May 19, 2024

CHINA IKO TAYARI KUONGEZA MISAADA KWA TANZANIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Ushikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (CIDCA) Bw. Luo Zhaohui walipokutana kwa mazungumzo Ofini kwakwe jijini Beijing, China

China imesema itaendelea kufadhili miradi mipya ya kimkakati ya Tanzania inayoendelea, baada ya kuridhishwa na utekelezwaji ya miradi ya awali. 


Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Misaada la China (CIDCA), Luo Zhaohui, aliyasema hayo kwenye mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, yaliyofanyika jijini Beijing, China mwishoni mwa wiki.

Zhaohui alisema kuna uwezekano mkubwa kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaweza kusaini mikataba mipya ya ushirikiano na misaada Septemba mwaka huu pembezoni mwa mkutano wa Wakuu wa Nchini na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) ambao amealikwa tayari.

"Tumesikia maelezo yako ndugu Waziri na nikuahidi kwamba tutafadhili hatua ya pili ya miradi inayoelekea kukamilika awamu ya kwanza na mingine ambayo umeiomba tunaweza hata kusaini wakati Rais wako atakapokuja Septemba mwaka huu" alisema Zhaohui.

CIDCA ndiyo taasisi inayopitisha misaada na mikopo ambayo serikali ya China kutoa kwa nchi zote duniani na Waziri Makamba alikwenda kufanya mazungumzo na mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayoendelea nchini China.
Picha ya pamoja

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Mwenyekiti wa Shirika la Ushikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (CIDCA) Bw. Luo Zhaohui na ujumbe wap wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Beijing, China. 

Saturday, May 18, 2024

MKUTANO WA 16 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA FEDHA WA EAC WAFANYIKA ARUSHA

Mkutano wa 16 Wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) la Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika Mei 17, 2024 jijini Arusha Tanzania. Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya ngazi ya watalaam na Mkutano wa Makatibu Wakuu iliyofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 16 Mei 2024.


Mkutano wa SCFCEA ulifanyika sambamba na mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. Mwenyekiti wa Mkutano huo alikuwa Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb.), Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe. Saadah Mkuya (Mb.), Waziri wa Nchi. Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.


Mkutano huo ulipokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi ya mkutano wa 15 wa (SCFEA) pamoja na masuala mbalimbali. Aidha, Nchi Wanachama ziliwasilisha Miongozo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Kaulimbiu za bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 ambapo Mkutano huo pia ulipitisha Kaulimbiu ya bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kupitisha tarehe 13 Juni 2024 kuwa tarehe ya kusoma bajeti za nchi wanachama.


Vilevile, Mkutano huo ulipitisha Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili baina ya Nchi Wanachama na Mkataba Kifani wa Kuongoza Majadiliano baina ya Nchi za EAC na nchi nyingine



Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (katikati) akiongoza  Mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  uliofanyika sambasamba na  Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Mei 17, 2024 jijini Arusha. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa SCFEA uliongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Saada Mkuya na kumshirikisha pia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo Kidata na viongozi wengine waandamizi wa Serikali

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (katikati) akichangia jambo wakati wa  Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Mei 17, 2024 jijini Arusha. Kushoto ni kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo, Mhe. Waziri Mkuya na kulia ni Dkt. Mwamba

Mkutano ukiendelea

Viongozi wakiwa wamesimama wakati wa ufunguiz wa mkutano

Wajumbe wa mkutano wakifuatilia

Mkutano ukiendelea

Wajume wakifuatilia mkutano

Picha ya pamoja


 

Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb.) ameongoza Mbio za African Day Marathon

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb.) ameongoza Mbio za African Day Marathon zilizo fanyika leo jijini Dar es Salaam katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo  akianzisha Mbio za Kilomita 15, Mbio hizo zimeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Umoja wa Mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa pamoja na Shirikisho la Riadha Tanzania, mbio hizo zimehudhuriwa na wanariadha maarufu nchini akiwemo, Alphonce Simbu, Gabriel Geay, Magdalena Crispin Shauri pamoja na Jackline Sakilu.

Juu na Chini ni sehemu washiriki wakiwa wameanza mbio za Kilomita 15



Balozi wa Japan nchini Tanzania akiwa kwenye Mbio za Kilomita 15.

Balozi wa Cuba nchini naye akiwa kwenye 



 

Friday, May 17, 2024

TANZANIA, CHINA ZAINGIA ZAMA MPYA KIDIPLOMASIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. WANG Yi walipokutana Ofini kwakwe jijini Beijing kwa mazungumzo. Terehe 17 Mei 2024

  • Nia ni kujenga dunia yenye usawa 
  • China yafuta machozi waathirika wa mafuriko
  • Yamwalika Rais Samia Septemba
  • Hadhi ya Chuo cha Dk. Salim kupanda
BAADA ya miaka 60 ya uhusiano wa kihistoria, Tanzania na China leo zimetangaza kuingia katika zama mpya za uhusiano wa kidiplomasia ambao lengo lake ni kujenga dunia iliyo bora zaidi, yenye maendeleo zaidi na usalama zaidi.

Katika mkutano wa pamoja uliofanyika jijini Beijing, China, leo Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, alimweleza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, kwamba katika miaka 60 iliyopita tangu kuanza kwa uhusiano nchi hizi mbili, Tanzania imejipambanua kama rafiki wa kwenye shida na raha.

“Tanzania mara zote amekuwa rafiki za China. Kwa China, miaka 60 ina maana kubwa sana kwenye uhusiano. Hatua inayofuata sasa baada ya hapa ni kuendeleza uhusiano huu katika zama mpya za kujenga dunia yenye maendeleo, ya haki na iliyo na usalama kwa watu wote” alisema Wang.

Waziri Makamba yuko nchini China kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa mwenzake huyo na alitumia nafasi hiyo pia kueleza namna Tanzania inavyothamini mchango wa taifa hilo la bara la Asia katika maendeleo yake na kwamba wakati umefika sasa wa kuingia katika zama mpya kuendana na changamoto za dunia ya sasa.

“China ni rafiki zetu kwenye nyakati zote. Ni rafiki ambaye anatabirika na habadilikibadiliki wakati wote. Baada ya miaka hii 60 ya uhusiano uliotukuka, sasa tuingie katika zama mpya za uhusiano ambao utazingatia changamoto zilizopo kwenye kujenga dunia bora zaidi kuliko ile iliyokuwepo wakati wa waasisi wa uhusiano huu” alisema.

Katika kuonyesha uhusiano wa karibu baina ya wananchi wa mataifa hayo, Waziri Wang alisema China inatoa mchango wa dola 500,000 za Marekani, sawa na shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya mvua yaliyoikumba Tanzania mwaka huu.

Maeneo kadhaa ya Tanzania yameathiriwa na mvua kubwa za masika zilizochanganyika na zile za El Nino na Waziri huyo wa China alisema Wachina wamesikia kuhusu athari hizo na wametoa mchango huo ili kusaidia waathirika kuanza upya maisha yao. Waziri Makamba alishukuru kwa mchango huo akisema ni ushahidi mwingine wa urafiki wa kipekee baina ya nchi hizo mbili.

Katika hatua nyingine, Serikali ya China leo imetoa mwaliko rasmi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhudhuria mkutano wa masuala ya usalama baina ya China na Afrika (FOCAC) uliopangwa kufanyika Septemba mwaka huu.

Mkutano wa FOCAC hufanyika kila baada ya miaka mitatu na katika miaka ya karibuni umekuwa ni miongoni mwa mikutano muhimu kwenye uhusiano wa kimkakati baina ya nchi za Afrika na China.

Kadhalika, China imekubali ombi la Tanzania la kufanya maboresho ya Chuo cha Diplomasia cha Dkt. Salim Ahmed Salim ikiwemo kuongeza majengo, kuongeza mitaala na kukifanya kuwa cha kutengeneza ajenda kwa ajili ya masuala ya kimkakati ya kubadili mfumo wa uendeshaji wa dunia.

Dk. Salim ni mmoja wa wana diplomasia wa Tanzania wenye heshima kubwa nchini China na uamuzi wa kuongeza hadhi ya chuo hicho umezingatia hadhi yake kidiplomasia na umuhimu wake kwa nchi hizi mbili.

Katika ziara yake hiyo inayoendelea nchini China, Makamba ambaye ameambatana na Mhe. Zahor Haji Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), alitembelea na kufanya mazungumzo na taasisi na viongozi wa mashirika yanayohusika na misaada kwa Tanzania ikiwemo benki ya EXIM ambayo imeahidi kuendelea kukopesha kwenye miradi ya kimkakati.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Ren Shengjun walipokuna kwa mazungumzo jijini Beijing, China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Ushikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (CIDCA) Bw. Luo Zhaohui walipokutana kwa mazungumzo Ofini kwakwe jijini Beijing, China.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. WANG Yi na ujumbe wao wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Beijini, China. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. WANG Yi akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba yaliyofanyika jijini Beijing, China.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Mwenyekiti wa Shirika la Ushikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (CIDCA) Bw. Luo Zhaohui na ujumbe wao wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Beijing, China.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Ren Shengjun yaliyofanyika jijini Beijing, China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. WANG Yi yaliyofanyika jijini Beijing, China
azungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Ren Shengjun yakiendela jijini Beijing, China
Picha ya pamoja