Friday, November 22, 2019
Thursday, November 21, 2019
MKUTANO WA 39 BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC WAANZA JIJINI ARUSHA
Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeanza leo jijini Arusha kwa lengo la kujadili na kukubaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Februari, 2020.
Mkutano huo wa siku saba umeanza leo kwa ngazi ya maofisa waandamizi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na utafuatiwa na mkutano wa Makatibu Wakuu kisha kuhitimishwa na Mawaziri wa Wizara za Kisekta zinazohusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki Novemba 27, 2019.
Ajenda za mkutano huo zinakadiriwa kuwa tisa ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.
Agenda nyingine ni taarifa ya Baraza kwa Wakuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yanayofiwa kwenye mikutano ya Wakuu hao wa Nchi na Kalenda ya Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuishia mwezi Juni 2019.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.
Baadhi ya wajumbe wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri ulioanza leo jijini Arusha kwa ngazi ya maofisa waandamizi |
Baadhi ya wajumbe wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia
mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri ulioanza leo jijini Arusha kwa ngazi ya maofisa waandamizi
|
Wednesday, November 20, 2019
INDONESIA KUWEKEZA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Indonesia kuwekeza Tanzania
Dodoma, 20 Novemba 2019
Mkutano wa Jukwaa la Viwanda kati ya Tanzania na Indonesia utafanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar Es Salaam tarehe 21 Novemba 2019. Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo ambapo kampuni kubwa 21 za Indonesia zinazojihusisha katika masuala ya ujenzi wa miundombinu na usafirishaji; kilimo; usindikaji vyakula; utengenezaji wa nguo, vifaa tiba na madawa ya binadamu; na uchimbaji wa madini na taasisi zinazosimamia masuala ya uwekezaji Tanzania (TIC, TPSF, CTI, TCCIA) zitashiriki katika mkutano huo.
Jukwaa hilo linatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa jumuiya ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wadau mbalimbali wa Tanzania na Indonesia kubadilishana mawazo, uzoefu na ujuzi pamoja na kuweka mikakati ya kushirikiana katika sekta ya viwanda kwa faida ya pande zote mbili.
Kutoka na nchi ya Indonesia kuwa ni kubwa kiuchumi Kusini-Mashariki mwa Asia na ipo nafasi ya 16 katika kundi la nchi 20 tajiri zaidi duniani (G20), na uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji nchini, ni dhahiri kuwa kongamano hilo litakuwa na matokeo mazuri katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Tuesday, November 19, 2019
UTURIKI KUWEKEZA UJENZI WA VIWANDA VYENYE THAMANI YA DOLA MILIONI 50 SIMIYU
USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA SHIRIKA LA AALCO KUENDELEA KUIMARIKA
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika meza moja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 63 tangu kuanzishwa kwa Shiriko la AALCO |
Wageni waalikwa wakiwa kwenye maadhimisho |
Monday, November 18, 2019
TANZANIA YAKABIDHI SHEHENA YA KWANZA YA MBEGU ZA KOROSHO NCHINI ZAMBIA
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia akihutubia adhira iliyojitokeza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mbegu za korosho jimbo la Mongu, Zambia tarehe 16 Novemba, 2019 |
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi
shehena ya mbegu za korosho kwa Serikali ya Jamhuri ya
Zambia katika hafla iliyofanyika mjini Mongu nchini humo.
Korosho hizo zimekabidhiwa kufuatia ahadi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe.
Edgar Lungu kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pamoja cha
Huduma Mpakani (OSBP) Tunduma tarehe 5 Oktoba, 2019.
Katika tukio hilo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mhe.
Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na
kwa upande wa Zambia, Serikali aliwakilishwa na Waziri wa
Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita, Watendaji kutoka
Serikalini na viongozi wa Kimila.
kwa upande wa Zambia, Serikali aliwakilishwa na Waziri wa
Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita, Watendaji kutoka
Serikalini na viongozi wa Kimila.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kapita kwa naiba ya
Serikali ya Jamhuri ya Zambia ametoa shukurani za pekee
kwa Mhe. Rais Magufuli kwa upendo aliouonesha
kwa Zambia na kwa upekee kabisa kwa wananchi wa jimbo
la Mongu.
Aliongezea kusema wananchi wa Mongu
wanamatumaini makubwa kuwa, mbegu hizo zitawapa
chachu ya kuzalisha korosho kwa wingi na kunufaika
kiuchumi kama ambavyo imekuwa kwa wananchi wa
Tanzania
Waziri wa Jimbo la Mongu, Zambia Mhe. Richard Kapita
akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho |
Picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi mbegu za korosho |
Shemu ya wananchi wa Mongu, Zambia waliojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho |
Saturday, November 16, 2019
WAZIRI WA MAMBO YA NJE, PROF. PALAMAGAMBA KABUDI AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA JIJINI DODOMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) nae akiungumza wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Waziri na Watumishi wa Wizara. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri na Watumishi wa Wizara. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akichangia hoja wakati wa mkutano kati ya Waziri na Watumishi wa Wizara |
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Issa Ng'imba akitoa neno kwa Watumishi wakati wa mkutano kati yao na Mhe. Waziri |
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwasikiliza viongozi wa Wizara wakati wa Mkutano kati ya Waziri na Watumishi |
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi |
Wakurugenzi wakifuatilia hotuba |
Watumishi wa Wizara wakinukuu mazungumzo kati yao na Mhe. Waziri |
Mkutano ukiendelea |
Wakurugenzi wengine wakifuatilia mkutano |
Watumishi wa Wizara wakiwa kwenye mkutano kati yao na Mhe. Waziri |
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara kwenye mkutano |
Pichani ni Watumishi wa Wizara wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri (hayupo pichani) alipozungumza nao |
Sehemu nyingine ya Watumishi |
Balozi Mteule, Bw. Jestus Nyamanga akiwa amesimama ili kupokea pongezi kutoka kwa Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) kwa niaba ya Watumishi wa Wizara kufuatia kuteuliwa kwake kwenye wadhifa wa Balozi hivi karibuni |
Mtumishi mpya wa Wizara akijitambulisha |
Mhe. Waziri Kabudi na meza kuu wakiwaongoza Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) kuimba wimbo wa ….Tuna imani na Mhe. Rais |
Watumishi wa Wizara wakiimba wimbo huo kwa furaha
|
Friday, November 15, 2019
TAKUKURU yakabidhiwa jalada la kufanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia
Na Mwandishi wetu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imeikabidhi TAKUKURU jalada la kulifanyia uchunguzi upotevu wa
fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe amekabidhi
jalada hilo kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John
Mbungo katika ofisi ndogo za Wizara jijiji Dar es Salaam.
Hatua hiyo
imekuja kutokana na jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi
mabaya ya fedha za uma.
Uchunguzi huo
unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi
wa Tanzania nchini Ethiopia.
Kuhusu kiwango
cha fedha kilichopotea Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe, amesema kitajulikana mara
baada ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walililokabidhiwa.
|
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dkt. Faraji Mnyepe
akimkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo jalada la upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia leo
jijini Dar es Salaam
|
Wednesday, November 13, 2019
DOUBLE TROIKA YA SADC YAKUTANA KUJADILI HALI YA AMANI NA USALAMA DRC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifungua mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi na usalama (double Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto wake ni Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe. |
Baadhi ya wajumbe wa Double Troika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika mkutano Jijini Dar es Salaam
|
Mawaziri wa mambo ya Nje, Mawaziri wa Ulinzi wa SADC wakutana kujadili hali ya Usalama na Amani DRC
Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi vya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ijulikanao kama DOUBLE TROIKA wamekutana kwa dharura kujadili hali ya kisasa na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha amani katika nchi hiyo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa dharura wa DOUBLE TROIKA inayojumuisha Troika ya siasa na Troika ya Ulinzi na Usalama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa lengo la mkutano huo wa dharura ni kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha amani nchini Congo DRC na kumaliza migogoro inayotishia ustawi wa nchi hiyo iliyodumu kwa miongo mingi.
Aidha, Waziri Kabudi amebainisha kuwa mkutano huo utasaidia nchi za SADC zenye vikosi vya ulinzi na usalama nchini DRC yaani Tanzania, malawai na Afrika Kusini kuimarisha amani na DRC kwa kufanya tathmini na kukubaliana hatua za kuchukua ili vita na migogoro ya mara kwa mara inayoibuka Nchini Congo DRC ifikie tamati na amani ya kudumu ipatikane.
“Mkutano huu wa leo ni wa Troika ya Siasa na Troika ya ulinzi na usalama ambapo kupitia mkutano huu tunaamini kuwa tutafanya tathimini ya hali ya amani DRC na kukubaliana ni hatua gani za kuchukua,” amesema Prof. Kabudi
Katika hatua nyingine Prof. kabudi ameongeza kuwa ndani ya mwaka huu amani na demokrasia vimezidi kuimarika katika nchi wanachama wa SADC, kutokana na baadhi ya nchi wanachama kuendesha chaguzi za kidemokrasia zilizomalizika kwa amani katika nchi za Msumbiji na Botswana.
Aidha Prof. Kabudi amesema Tanzania na Nchi 16 wanachama wa SADC bado zinaendelea kupaza sauti kwa jumuiya za kimataifa na nchi ambazo zimeiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa mara moja kutokana na vikwazo hivyo kutokuwa na uhalali jambo linalosababisha mateso kwa raia wan chi hiyo hususani akina mama na watoto .
"Katika hili la Zimbabwe lazima sisi kama SADC tushikamane na kusafiri pamoja ili tufike kwa umoja wetu" Amesema Prof. kabudi.
Awali akitoa hutuba katika mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC), Stergomena Tax amesema kuwa ana matumaini makubwa na mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam utatathimini na kutoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu kuhusu hali ya usalama, amani na siasa katika nchi ya Congo DRC na ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ili kuhakikisha ukanda huo unakuwa salama na amani
Ameongeza kuwa amani na usalama ni nyenzo mojawapo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na hivyo kupata maendeleo yanayohitajika kwa ajili ya mataifa ya Afrika.
Subscribe to:
Posts (Atom)