Thursday, March 26, 2020
Wednesday, March 25, 2020
BALOZI KANALI IBUGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA PAKISTAN
Mazungumzo yakiwa yanaendelea |
Friday, March 20, 2020
WIZARA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2019/2020
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya Mpango wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika moja ya kumbi za Bunge jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Salim Mwinyi Rehani (mwenye suti nyeusi) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi hayupo pichani aliyekuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara ya mwaka 2019/2020
WIZARA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2019/2020
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020.
Akiwasilisha taarifa ya Wizara, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Wizara katika kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzingatia maoni na ushauri wa Kamati ya Bunge imeanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Majengo ambacho kitakuwa chini ya Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.
Amesema pamoja na kuanzishwa kwa Kitengo hicho Wizara imeendelea kushirikiana na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakifuata sheria na taratibu zilizopo.
Amesema uamuzi wa kuanzishwa kwa kitengo hicho unatokana na ushauri uliotolewa na Kamati hiyo uliyoitaka Wizara kuhakikisha mipango ya ujenzi wa majengo ya ofisi na makazi ya Balozi mbalimbali nje ya nchi unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi mkubwa.
“Uamuzi huu umetokana na ushauri ambao Kamati hii iliutoa kwa Wizara katika kuhakikisha suala la ujenzi wa majengo ya Balozi zetu unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi,” alisema Prof. Kabudi.
Mhe. Waziri amesema Wizara inaendelea na mipango ya kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika mipango na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchininikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia maendeleo na kusaidia ndugu na jamaa zao waliopo nchini na kufanya uchambuzi wa mazingira ya ushirikishwaji wao na kuangalia masuala ya kisheria, kitaasisi ushirikiano na sekta binafsi takwimu za Watanzania waishio ughaibuni na uwezo na hamasa ya kuchangia maendeleo ya nchi.
Wednesday, March 18, 2020
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC
Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC, Dkt. Stergomena Tax akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya jumuiya hiyo wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC. |
Wajumbe wa Mkutano huo ambao ni Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine waandamizi wakifuatilia hafla ya ufunguzi. |
Tuesday, March 17, 2020
DKT. NDUMBARO AKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI, SWEDEN
Naibu Waziri, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter
Van Acker pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjoberg leo jijini Dar
es Salaam.
Mazungumzo ya Mhe.
Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi wa Ubelgiji yalijikita katika
masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania
na Ubelgiji hasa kwenye sekta za Kilimo na Madini.
Balozi wa Ubelgiji,
Mhe. Acker amesema kuwa Ubelgiji itaendelea kuwekeza katika kilimo cha maharage
mkoani Kigoma, na kilimo cha Tumbako katika mikoa ya Tabora, Ruvuma, Katavi na Rukwa.
"kupitia
uwekezaji wa kilimo nchi zetu mbili (Tanzania na Ubelgiji) zimekuwa zikinufaika
sawa hivyo ni rai yangu kuona uwekezaji huu unaendelea kutoa fursa za ajira kwa
mataifa haya mawili," Amesema Balozi Acker.
Aidha, Dkt. Ndumbaro
amesema kuwa Tanzania itaendelea kuhakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake
na Ubelgiji katika sekta ya Kilimo, Uwekezaji na Biashara ili kuendelea kutoa
fursa za ajira na kukuza uwekezaji nchini.
Katika nyingine, Naibu
Waziri Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini
Mhe. Anders Sjoberg, ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa
kidiplomasia.
Pamoja na mambo
mengine, Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Sjoberg amemuahidi Naibu Waziri kuwa
Sweeden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizi
mbili zinapiga hatua katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Kwa upande wake Mhe.
Naibu Waziri amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendelea kukuza na
kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano wake na Sweden kwani uhusiano huo wa muda
mrefu umekuwa na manufaa kwa nchi zote mbili.
Naibu Waziri, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana
na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker kabla ya kuanza kwa mazungumzo
yao jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ubelgiji nchini,
Mhe. Peter Van Acker akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia
jambo Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker wakati wa mazungumzo
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakisalimiana bila kushikana mikono kabla ya kuanza kwa mazungumzo yaliyofanyika
jijini Dar es Salaam
Balozi wa Sweeden
nchini Mhe. Anders Sjoberg akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimueleza
jambo Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakati wa mazungumzo
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Monday, March 16, 2020
TEKNOLOJIA YAWEZESHA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI WA SADC KUEPUKA CORONA ( COVID-19)
Maafisa Waandamizi wa nchi za SADC wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano kutokea nchini Tanzania kupitia mfumo wa video |
Mkutano ukiendelea.
|
Sunday, March 15, 2020
KAMATI YA BUNGE YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA OFISI ZA WIZARA YA MAMBO YA NJE ZILIZOPO MTUMBA JIJINI DODOMA
Mhe. Prof. Kabudi akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya NUU |
Wajumbe wa Kamati ya NUU akiwemo Mhe. Vuai Nahodha (kulia) wakimsikiliza Prof. Kabudi (hayupo pichani). Kushoto ni Mhe. Augustino Masele. |
Wajumbe wengine wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Bonnah Kaluwa na Sophia Mwakagenda nao wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi ambaye hayupo pichani |
Mhe. Masoud Abdalla Salim, Mjumbe wa Kamati akichangia hoja wakati wa ziara yao kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mjumbe wa Kamati, Mhe. Silafu Maufi alipotoa ushauri kwa Wizara kuhusu kuboresha maeneo kadhaa ya Jengo walilotembelea |
Mhe. Almas Maige, Mjumbe wa Kamati naye akizungumza. Kulia ni Mhe. Ruth Mollel na Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (kushoto) |
Sehemu ya Wakuuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Bw. Ng'imba ambaye hayupo pichani |
Msimamizi wa Miradi ya Majengo ya Wizara, Mhandisi John Kiswaga akijibu hoja kadhaa zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa ziara yao Wizarani |
Mhe. Mwakagenda akizungumza wakati wa ziara yao |
Mhe. Prof. Kabudi akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea chumba cha ofisi yake wakati wa ziara yao kwenye jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi akimwonesha Mhe. Mwambalaswa mandhari ya nje ya jengo akiwa ndani ya ofisi yake |
Mhe. Prof. Kabudi akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama chumba cha wageni mashuhuri kilichopo kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba |
|
Mhe. Prof. Kabudi akiwaonesha eneo la nje la Jengo la Wizara |
Mhe. Mwambalaswa akimweleza jambo Mhe. Prof. Kabudi |
Jengo la Wizara kama linavyoonekana |
Mhe. Prof. Kabudi akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama kurejea ndani mara baada ya kutembelea eneo la nje la Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi akijadiliana jambo na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama mara baada ya kukamilisha ziara yao. |
Mhe. Prof. Kabudi akiagana na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama mara baada ya kukamilisha ziara yao kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma ====================================================
WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA NJE, ULINZI NA USALAMA WATEMBELEA JENGO LA WIZARA LILILOPO MTUMBA
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)
wakiongozwa na Mhe. Victor Mwambalaswa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati hiyo
wamefanya ziara ya kikazi kwenye Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki lililopo kwenye Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma leo
tarehe 15 Machi 2020.
Wajumbe
hao ambao wapo kwenye program ya kukagua miradi iliyopo kwenye Wizara
zinazosimamiwa na Kamati hiyo, wamepokelewa na mwenyeji wao Mhe. Prof.
Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki mara baada ya kuwasili.
Wakizungumza
wakati wa ziara hiyo, baadhi ya Wajumbe hao, wameipongeza Wizara kwa kukamilisha ujenzi
wa jengo hilo kwa wakati ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya kuhamia Dodoma. Pia wameishauri Wizara kuendelea kuboresha maeneo
kadhaa katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kuzunguka jengo hilo na
kukamilisha mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kuboresha mawasiliano. Vilevile,
Wajumbe wa Kamati hiyo wameitaka Wizara kuzingatia kanuni za ujenzi wa majengo
ya Ofisi za Mambo ya Nje pale Wizara itakapoanza ujenzi wa jengo lake la kudumu
katika siku zijazo.
Kwa
upande wake, Mhe. Prof. Kabudi aliahidi kutekeleza ushauri uliotolewa na
Wajumbe wa Kamati hiyo na kuwahakikishia kuwa, mapungufu kadhaa yaliyopo
yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Aidha,
akitoa taarifa fupi kuhusu ugonjwa wa Corona kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, Mhe.
Prof. Kabudi alisema kuwa, Serikali ya Tanzania imechukua hatua madhubuti kwa
ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini. Hatua hizo ni
pamoja na mikutano ya kikanda kuanza kufanyika kwa njia ya video ukiwemo
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi 2020.
Pia
Kamati ya Kitaifa inayojumuisha Sekta mbalimbali imeundwa kwa ajili ya kuandaa
mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ugonjwa huo. Kadhalika vifaa, wataalam na
maeneo ya karantini tayari yametengwa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.
“Tanzania
inaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali kuhusu ugonjwa wa Corona ambao hadi
sasa haujaingia nchini. Hatua hizo ni pamoja na kuandaa mikutano ya kikanda
ambayo itafanyika kwa njia ya video. Katika kutekeleza hilo, Mkutano wa Baraza
la Mawaziri wa SADC unaoanza tarehe 16 Machi mwaka huu utafanyika kwa njia ya
video na utafuata taratibu zote za mikutano ya kikanda wakati wa ufunguzi”
alisisitiza Prof. Kabudi.
Jengo
la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambalo lipo Mtumba
jijini Dodoma lina ukubwa wa Mita za Mraba 1,002 na vyumba 17 vyenye matumizi
mbalimbali zikiwemo Ofisi. Jengo hilo lilianza kujengwa mwezi Desemba 2018 na kukamilika
mwezi Machi 2019.
|
Saturday, March 14, 2020
PROF. KABUDI AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUJITOA MHANGA
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma |
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Ibuge naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika jijini Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi na wajumbe wengine wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Kanali Ibuge (hayupo pichani) |
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo |
Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Amani Simon Msuya akiwa na Mwakilishi wa TUGHE-Dodoma wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Wajumbe wa Baraza la Wafanayakazi wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano |
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo |
Wajumbe wa Baraza wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano |
Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Msuya nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Msuya (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza |
Mjumbe wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo wakati wa ufunguzi |
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza wakimsikiliza Balozi Hamza (hayupo pichani) |
Wajumbe wa Baraza |
Wajumbe wengine wa Baraza |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Balozi Ibuge na Wajumbe wa TUGHE-Taifa na Wizarani |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Baraza hilo |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wote wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Subscribe to:
Posts (Atom)