Friday, July 12, 2013

Tanzania na Kuwait zasaini Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya Siasa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimkaribisha nchini Mhe. Sheikh Khalifa Al Hamad Al Sabah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.

Mhe. Membe na Mhe. Al Sabah wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika masuala ya Siasa kati ya Tanzania na Kuwait. Tukio hilo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2013. Kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Al Sabah (hayupo pichani) walipokutana. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa kwanza kushoto kwa Mhe. Membe), Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Prof. Abillah Omar (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto)

Mhe. Al Sabah akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani).
Mhe. Al Sabah akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Membe.
Picha ya pamoja.

 Mhe. Membe akimpatia maelekezo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Naimi Aziz ambaye alishiriki mazungumzo kati ya Mhe. Membe na 
Mhe. Al Sabah.


Mhe. Prof. Omar (katikati) na Balozi Yahya (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kutoka kushoto ni Bw. Abas Mngwali, Bw. Hassan Mwamweta na Bi. Tagie Daisy Mwakawago.



Picha na Ally Kondo.

Mhe. Membe amuaga Balozi wa Uholanzi hapa nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiongea kwa msisitizo wakati wa hafla ya kumuaga Mhe. Ad Koekkoek ambaye ni Balozi wa Uholanzi aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo  ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2013.

Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini akiwemo Mhe. Alfonso Lenhardt (kulia), Balozi wa Marekani hapa nchini.

Mhe. Balozi Koekkoek naye akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.


Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano, Balozi Dora Msechu akizungumza machache wakati wa hafla hiyo.

Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Balozi Koekkoek wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo.

Mhe. Membe akimwonesha Mhe. Balozi Koekkoek zawadi ya picha ya kuchora ya Twiga aliyomkabidhi.

Mhe. Balozi Koekkoek akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Membe.

Balozi Msechu akibadilishana mawazo na Mhe. Balozi Koekkoek.

Thursday, July 11, 2013

Kaimu Katibu Mkuu afungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Mambo ya Nje  wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akifungua rasmi mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2013. Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 13 Julai, 2013.

Balozi Gamaha (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Kamishina wa Magereza wa Afrika Kusini, Bw. Tom Moyane (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Usalama wa Namibia, Bw. Ben Likando (Kulia) na Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Luteni Kanali Mstaafu, Tanki Mothae (kushoto) kabla ya ufunguzi wa mkutano huo.

Wajumbe wa Tanzania wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kulia ni Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wajumbe kutoka nchi wanachama wa SADC wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa Makatibu Wakuu.

Wajumbe wengine wakati wa ufunguzi.


Wajumbe wa Sekretarieti ya SADC.

Balozi Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mkutano huo.    




Picha na Reginald Philip na Olga Chitanda.

Mkuu wa Majeshi afungua Mkutano wa Wakuu wa Vyombo vya Usalama wa Asasi ya SADC


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali Devis Mwamunyange akifungua rasmi Mkutano wa Makatibu Wakuu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Julai, 2013.  Mkutano  huo ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Asasi hiyo utakaofanyika tarehe 13 Julai, 2013.

Baadhi ya Wajumbe kutoka nchi wanachama wa SADC wakimsikiliza Generali Mwamunyange (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano  huo.

Wajumbe wengine wakati wa mkutano huo.

Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Usalama nchini Namibia, Bw. Ben Likando na Bw. Tom Moyane, Kamishina wa Magereza wa Afrika Kusini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa asasi hiyo. Tanzania ni Mweneyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC  wakati  Namibia ni  Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo na Afrika Kusini ilikuwa Mwenyekiti kabla ya Tanzania.

Wednesday, July 10, 2013

Tanzania na India zasaini Makubaliano ya Pamoja ya Mkutano wa JPC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Preneet Kaur wakisaini Makubaliano ya Pamoja ya Mkutano wa 8 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission-JPC) kati ya Tanzania na India mara baada ya mkutano huo kumalizika tarehe 09 Julai, 2013.Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. John Kijazi (wa kwanza kulia waliosimama nyuma ya Mhe. Membe) akifuatiwa na Bw. Omar Mjenga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Balozi wa India hapa nchini, Mhe.Debnath Shaw (wa kwanza kushoto)

Wajumbe mbalimbali wakishuhudia uwekwaji saini makubaliano hayo.

Wajumbe wa Sekrtarieti kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakishuhudia tukio hilo la uwekaji saini makubaliano.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur wakibadilishana Makubaliano hayo mara baada ya kusaini.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur wakionesha kwa Wajumbe na Waandishi wa Habari  (hawapo pichani) Makubaliano hayo mara baada ya kusaini.


Picha na Reginald Philip.

Hafla ya Chakula cha Jioni yafanyika kwa heshima ya Waziri wa Mambo ya Nje wa India

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha katika hafla ya Chakula cha Jioni Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Preneet Kaur (mwenye nguo ya pinki walioketi) na ujumbe wake ambao walikuwa nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na India uliofanyika tarehe 08 na 09 Julai, 2013.

Wajumbe kutoka Tanzania na India wakati wa hafla hiyo.

Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Kaur zawadi ya kinyago. Kulia ni Bw. Omar Mjenga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia.

Mhe. Kaur akisikiliza maelezo kuhusu zawadi hizo za vinyago alizokabidhiwa na Mhe. Membe.

Tuesday, July 9, 2013

Mhe. Rais Kikwete akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Preneet Kaur alipofika kwa ajili  ya mazungumzo rasmi. Mhe. Kaur yupo nchini  kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India.

Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Mhe. Kaur kabla ya kuanza mazungumzo.

Mhe. Kaur akifafanua jambo Mhe. Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yao.

Mhe. Rais Kikwete akimsindikiza Mhe. Kaur mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Mhe. Rais Kikwete akiagana na Mhe. Kaur mara baada ya mazungumzo yao. Kushoto kwa Mhe. Rais ni Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. John Kijazi (kulia) akisisitiza jambo huku Bw. Cliford Tandari (katikati), Naibu Katibu Mkuu, Tume ya Mipango na Bw. Omar Mjenga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wakimsikiliza kwa makini walipokuwa eneo la Ikulu wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Rais na Waziri wa Mambo ya Nje wa India.

Monday, July 8, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kikao cha 15 cha Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (The SADC Ministerial Committee of the Organ on Politics, Defence and Security Cooperation), kitafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam tarehe 10-13 Julai, 2013.

Kikao hicho kinachohusisha sekta ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kitatanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu na Maofisa Waandamizi tarehe 10 na 11 Julai, 2013 na kitahudhuriwa na Nchi zote wanachama wa SADC isipokuwa Madagascar, ambayo imesimamishwa uanachama.

Mawaziri watakutana tarehe 13 Julai, 2013, chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mheshimiwa Bernard Kamilius Membe (Mb).

Pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa Kusini mwa Afrika, uimarishaji wa Demokrasia, Utekelezaji wa  Mpango Mkakati wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Mikataba ya ushirikiano katika Nyanja za Ulinzi na Usalama pamoja na Ushirikiano baina ya SADC na Umoja wa Ulaya (EU).

Washiriki wa vikao vya Maofisa Waandamizi wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam tarehe 9 Julai, 2013 wakati Mawaziri watawasili tarehe 12 Julai, 2013.  

Kikao hicho cha Mawaziri kitafuatiwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi, utakaofanyika Lilongwe, Malawi, tarehe 17-18, Agosti, 2013, ambao utahitimisha Uenyekiti wa Tanzania wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, ulioanza tangu Agosti, 2012.  Mwenyekiti anayefuata wa Asasi hiyo atakuwa Namibia wakati Uwenyekiti wa SADC utachukuliwa na Malawi.

Nchi Wanachama wa SADC ni Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Sheli Sheli, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.


IMETOLEWA NA:


WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

8 JULAI,  2013


Mhe. Membe afungua Mkutano wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission-JPC) kati ya Tanzania na India unaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro kuanzia tarehe 08 hadi 09 2013. Mkutano huo unaowashirikisha Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini na India utajadili pamoja na mambo mengine masuala ya ushirikiano katika sekta za Uchumi, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Elimu, Afya, Utalii, Kilimo na Nishati na Madini.

Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo.

Wadau wengine wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Wadau kutoka India.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya India, Mhe. Preneet Kaur akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Wadau wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Kaur (hayupo pichani)

Wadau zaidi.

Meza kuu kabla ya ufunguzi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza machache kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo. Anayeonekana pembeni ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India.

Wajumbe wa Sekretarieti wakati wa mkutano huo.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur walioketi, katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Omar Mjenga (kulia) akiwa na Mjumbe kutoka India wakati wa Mkutano huo.


Picha na Reginald Philip na Olga Chitanda.