Wednesday, April 23, 2014

Mhe. Naibu Waziri azindua Kambi ya Airtel Rising Stars International Soccer

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Kambi Maalum ya Kimataifa ya Mafunzo ya Mpira wa Miguu kwa vijana wa kike na kiume wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika Viwanja vya Azam vilivyopo Chamazi jijini Dar es Salaam tarehe 23 Aprili, 2014. Kambi hiyo inadhaminiwa kwa ushirikiano kati ya kati ya Kampuni ya Simu ya Airtel-Tanzania na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza.
Baadhi ya vijana hao wakimsikiliza kwa makini Mhe. Naibu Waziri (hayupo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso ambao ni wadhamini wa kambi hiyo kwa kushirikiana na Manchester United akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mhe. Mahadhi akimsikiliza Bw. Colaso, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel-Tamnzania (hayupo pichani wakati wa uzinduzi huo.
Mmoja wa Walimu kutoka Manchester United Bw. Neil Scott akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara akiwa na mmoja wa wadau wa michezo wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Ayoub Nyenzi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso kwa pamoja na Walimu wa Vijana hao chini ya miaka 17 wakimsikiliza Bw. Nyenzi (hayupo pichani) kutoka TFF alipokuwa akizungumza. Kulia ni Bw. Andrew Stokes na katikati ni Bw. Neil Scott.
Wanamichezo na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri.
Mshereheshaji Bw. Ephraim Kibonde akiendelea na kazi
Mhe. Maalim akipongezwa na Bw. Colaso baada ya kutoa hotuba.
Mhe. Maalim akielekea kuzindua rasmi kambi hiyo kwa kupiga mpira.
Mmoja wa vijana hao ambaye ni mlinda mlango akiwa tayari kudaka mpira kutoka kwa Naibu Waziri.

Mhe. Naibu Waziri akijiandaa kupiga mpira kuashiria kuzindua kambi hiyo ya vijana.
Mhe. Maalim akimsikiliza Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi Juliana Yasoda ambaye pia alishiriki uzinduzi huo.

Mhe. Naibu Waziri akizungumza na Waandishi wa Habari
Vijana hao wakiwa kwenye mazoezi
Mhe. Naibu Waziri katika picha ya pamoja na viongozi walioambatana na wanamichezo.
Mhe. Maalim katika picha ya pamoja  na wanamichezo.
Picha na Reginald Philip




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje azindua Airtel Rising Stars International Soccer

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) amezindua rasmi Kambi Maalum ya Kimataifa ya Mafunzo ya Mpira wa Miguu kwa vijana wa kike na wa kiume wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania.

Uzinduzi wa Kambi hiyo umefanyika katika Viwanja vya Azam vilivyopo Chamazi Jijiji Dar es Salaam tarehe 23 Aprili, 2014 na inadhaminiwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Simu ya Airtel-Tanzania na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhe. Dkt. Maalim amesema kuwa, kambi hiyo inalenga kuwapatia mafunzo maalum vijana hao wadogo ili kuwawezesha kuwa wachezaji mahiri katika mchezo huo ambao unapendwa na watu wengi duniani ikiwemo Tanzania.

“Mimi binafsi kama ilivyo kwa mamilioni ya Watanzania, mpira wa miguu una nafasi maalum katika mioyo yetu na tunazitambua na kuzipongeza jitihada zinazofanywa na Kampuni ya Simu ya Airtel kwa ushirikiano na Manchester United katika kusaidia maendeleo ya mchezo huo hapa Tanzania na sehemu nyingine za Bara la Afrika. Asanteni sana Airtel na Manchester United” alishukuru Mhe. Maalim.

Mhe. Maalim alieleza kuwa, mafunzo hayo ambayo yatasimamiwa na Waalimu kutoka Shule za Mpira wa Miguu za Timu kubwa ya Manchester United, yanalenga kuwaandaa vijana hao wadogo na kukuza vipaji vyao katika mafanikio ya mpira wa miguu Afrika kwani watu wanahitaji kuona mapinduzi katika mchezo huo na kuondokana na matokeo mabaya katika mashindano ya kimataifa.

“Ushiriki wa watoto wetu kwenye mafunzo haya ambayo yatajikita katika kuwajengea uwezo kiakili, kimwili na kisaikolojia, yatawasaidia kuwa na umoja, yatawapa kujiaamini na hatimaye kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao kutokana na afya njema na pia kuwa wachezaji wa kulipwa Barani Afrika na duniani hapo baadaye”, alisema Mhe. Maalim.

Mhe. Maalim aliongeza kuwa, anaona fahari kubwa kama mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuwepo kwenye uzinduzi huo ikiwa ni katika kuhamasisha Diplomasia ya Michezo ambayo kwa sasa ni muhimu katika kukuza urafiki, undugu, ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya mtu mmoja mmoja kwa maana ya wachezaji na pia kwa nchi na nchi kama ilivyo kwa vijana hao ambao wametoka mataifa ya nje 11.

“Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa sasa inahamasisha Diplomasia ya Michezo ikiwa ni njia mojawapo za kuimarisha mahusiano na mataifa mengine kupitia michezo. Wizara inaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Wizara yenye dhamana ya michezo na Taasisi nyingine zote za michezo na kitendo cha mimi kuwepo hapa leo ni katika kuongeza nguvu kwenye jitihada hizo ili nchi yetu iendelee kimichezo,” alisisitiza Mhe. Maalim.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya kuwekeza kwenye michezo.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Ayoub Nyenzi ambaye alimwakilisha Rais wa Shirikisho hilo,  alimshukuru Naibu Waziri kwa kuzindua Kambi hiyo ambayo ni ya pili kwa Tanzania baada ya ile ya mwaka 2011. Aidha, aliwaasa vijana hao kuzingatia mafunzo watakayopewa kwani ndio msingi wa maisha yao hapo baadaye.

Kwa upande wao Walimu wa vijana hao kutoka Manchester United Bw. Andrew Stokes na Bw. Neil Scott walisema kwao ni upendeleo wa pekee kufundisha vijana hao na kwamba Manchester United imedhamiria kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kuendeleza michezo.

Kambi hiyo ambayo ipo kwa siku tano itahusisha vijana 74 kutoka mataifa 12 ya Afrika ikiwemo Tanzania. Jina la nchi na idadi ya vijana kwenye mabano ni kama ifuatavyo; Tanzania (19), Niger (17), Chad (4), Kenya (4), Malawi (4), Shelisheli (2) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (6). Nchi nyingine ni Burkina Faso (4), Congo Brazaville (2), Gabon (4), Madagascar (2) na Siera Leone (6).

-Mwisho-














Sunday, April 20, 2014

Waziri Membe awa Mgeni Rasmi Tamasha la Pasaka

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na mkewe Mama Dorcas Membe wakiwasili kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Pasaka. Mhe. Membe alikuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo lililofanyika siku ya Pasaka tarehe 20 Aprili, 2014.
Mhe. Membe na mkewe wakisalimiana na Waandaaji wa Tamasha la Pasaka akiwemo Kiongozi wao Bw. Alex Msama (wa  kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Taifa.
Mhe. Membe akiwa ameongozana na Mwandaaji wa Tamasha la Pasaka  Bw. Msama kuingia uwanjani.
Mhe. Membe akisalimia umati wa watu (hawapo pichani)  waliohudhuria Tamasha hilo.
Umati wa Watu waliohudhuria Tamasha la Pasaka.
Mwandaaji wa Tamsha la Pasaka Bw. Msama nae akisalimia watu waliohudhuria
Mama Membe akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Bibi Angela Kairuki ambaye pia alishiriki kwenye Tamasha la Pasaka.
Mmoja wa Waimbaji wa Nyimbo za Injili, Bi. Upendo Nkone akitumbuiza wakati wa Tamasha la Pasaka.
Mhe. Membe akimpongeza Bi. Nkone mara baada ya kutumbuiza.
Mmoja wa Wachungaji waliohudhuria Tamasha la Pasaka akisoma risala maalum kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Membe.
Mhe. Membe akitoa hotuba wakati wa Tamasha la Pasaka.
Umati wa watu wakishangilia wakati Mhe. Membe (hayupo pichani) akihutubia.
Balozi Mbelwa Kairuki (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye pia alikuwepo kwenye Tamasha la Pasaka.
Mhe. Membe akiwa na Bw. Richard Kasesera ambaye pia alihudhuria Tamasha la Pasaka.

Picha na Reginald Philip.

Saturday, April 19, 2014

Waziri Mkuu ahitimisha Maonesho ya miaka 50 ya Muungano

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Mizengo Peter Kayanza Pinda akiongozana na Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais alipowasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufunga rasmi Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  rasmi
 19 Aprili, 2014
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda, akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe za ufungaji wa Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Wananchi kutoka  vitongoji mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda alipokuwa akihutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhe. Pinda akiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa na moja ya kikundi cha ngoma (hawapo pichani) kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa ufungaji wa maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Wengine katika picha ni Mhe.  Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mhe. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala  ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kikundi cha Ngoma kikitoa Burudani mbele ya mgeni rasmi Mhe. Pinda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za ufungaji wa Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally akipokea Cheti cha Ushiriki wa Wizara kwenye Maonesho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akizungumza na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wananchi wakiwa katika Banda la maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Picha na Reginald Philip.

Thursday, April 17, 2014

Waziri Membe akabidhi rasmi Tuzo ya Mhe. Rais Kikwete

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa maelezo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kumkabidhi Tuzo ya Heshima ya Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa ziadi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 aliyoipokea kwa niaba ya Mhe. Rais Kikwete tarehe 9 Aprili, 2014 Jijini Washington D.C, Marekani. Heshima hiyo kwa Rais Kikwete ilitolewa na Jarida Maarufu la Kimataifa la African Leadership Magazine Group.
Mhe. Rais Kikwete na Wajumbe wengine waliokuwepo akiwemo Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu wakimsikiliza Mhe. Membe.
Mhe. Membe akimkabidhi rasmi Mhe. Rais Kikwete Tuzo yake. 
Mhe. Rais Kikwete akionesha Tuzo hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mhe. Membe.

Picha na Reginald Phillip.


Wednesday, April 16, 2014

Katibu Mkuu amwakilisha Waziri kumpokea Rais Mstaafu wa Zanzibar alipotembelea Maonesho ya miaka 50 ya Muungano

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akimkaribisha Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume (katikati) kuzungumza na wananchi alipotembelea maonesho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 19 Aprili, 2014. Bw. Haule alikuwa mwenyeji wa Mhe. Karume Viwanjani hapo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.).

Mhe. Karume akizungumza viwanjani hapo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mhe. Karume na Bw. Haule wakisikiliza maelezo kutoka kwa Maafisa walipotembelea Banda la maonesho la Benki Kuu ya Tanzania Viwanjani hapo.





President Kikwete congratulates Queen Margrethe II of Denmark


PRESS RELEASE

H.E President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.M Queen Margrethe II of Denmark on the occasion of her 74th birthday on 16th April 2014.

“Your Majesty Queen Margrethe II,

   Amalienborg Palace,

   COPENHAGEN,

   Denmark.

It is my pleasure on behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania to congratulate Your Majesty on the occasion of your 74th birthday.

As you celebrate your 74th birthday allow me to take this opportunity to express my sincere appreciation on the excellent relations that happily exist between our two countries and peoples. 

The celebration of your birthday offers us yet another opportunity to reaffirm our commitment to continue working closely together in enhancing the existing bilateral ties between our two countries. I am confident that the bonds of friendship, co-operation and partnership that our two countries enjoy will continue to grow in greater heights for mutual benefit.

Please accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health, peace and prosperity for the people of Denmark”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania, 

Dar es Salaam.

16th April 2014

 

Tuesday, April 15, 2014

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharrif Hamad, akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Maonesho ya Miaka 50 ya  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 16 Aprili, 2014 na kuzihusisha Wizara na Taasisi za Muungano.  Lengo la maonesho hayo ni kuwaeleza wananchi mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano, changamoto na namna ya kuzikabili pamoja na matarajio ya baadaye kuhusu Muungano huo.
Mhe. Makamu wa Rais akimsikiliza Balozi Silima Haji ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar akimweleza majukumu ya Idara hiyo kwa upande wa Zanzibar katika kudumisha Muungano.
Mhe. Hamad akifurahia jambo wakati akipata maelezo  kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara. Bw. Mkumbwa aliezea kuhusu mafanikio ya Wizara katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Balozi Silima akitoa maelezo kuhusu Sera ya Mambo ya Nje kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la Wizara.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizarani na Taasisi za Wizara wakiwa katika Sare nadhifu za Maonesho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi    zilizoachwa wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.

Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:






Balozi Dora Mmari Msechu, ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M.H. Mzale ambaye amestaafu.





Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba, ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi utaeuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.




 
 








Kadhailika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine kuwa Balozi na Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kabla ya Uteuzi huu, Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala kayika ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.

Umetolewa na

(John M. Haule)
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
15 APRILI, 2014