Tuesday, April 15, 2014

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharrif Hamad, akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Maonesho ya Miaka 50 ya  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 16 Aprili, 2014 na kuzihusisha Wizara na Taasisi za Muungano.  Lengo la maonesho hayo ni kuwaeleza wananchi mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano, changamoto na namna ya kuzikabili pamoja na matarajio ya baadaye kuhusu Muungano huo.
Mhe. Makamu wa Rais akimsikiliza Balozi Silima Haji ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar akimweleza majukumu ya Idara hiyo kwa upande wa Zanzibar katika kudumisha Muungano.
Mhe. Hamad akifurahia jambo wakati akipata maelezo  kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara. Bw. Mkumbwa aliezea kuhusu mafanikio ya Wizara katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Balozi Silima akitoa maelezo kuhusu Sera ya Mambo ya Nje kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la Wizara.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizarani na Taasisi za Wizara wakiwa katika Sare nadhifu za Maonesho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.