Wednesday, September 10, 2014

Tanzania and Oman keen to develop EPZA


Ambassador Hassan Simba Yahaya,third from right, Director of Middle East Department at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation leading Tanzania delegation in the discussions with the CEO of Oman's State General Reserve Fund regarding development of Bagamoyo Special Economic Zone.  The meeting which took place in Muscat, Oman was also attended by Dr.Adlehem Meru, Director General of EPZA, Mr.Madeni Kipande, Acting Director General of Tanzania Ports Authority, His Excellency Saleh, Tanzania Ambassador in  Oman and other senior government officials

Tanzania delegation (R) in discussion with Oman delegation



Rais Kikwete amwapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ali Siwa. Hafla hiyo ilifanyika, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa kwanza mstari wa mbele) pamoja na wageni waalikwa  wakifuatilia tukio la kuapishwa kwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda.
Balozi Siwa akisaini Hati ya Kiapo mbele ya Mhe. Rais Kikwete
 Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi vitendea kazi, Balozi Siwa.
Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Siwa mara baada ya kiapo.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Siwa. 
Mhe. Rais Kikwete na Balozi Siwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Mhe. Rais Kikwete  katika picha ya pamoja na Familia ya Balozi Siwa.

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Norway  nchini  Mhe. Hanne Maria Kaarstad. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2014.
Balozi Kaarstad akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kaarstad akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Kaarstaad mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi huyo, Ikulu.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Kaarstaad.
Mhe. Rais Kikwete pamoja na Balozi Kaarstaad katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Norway.
Balozi Kaarstad akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya  kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kaarstad akisikiliza Wimbo wa Taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma (kulia), Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
Maafisa kutoka Ubalozi wa Norway wakisikiliza wimbo wa taifa lao.
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa taifa la Norway kwa heshima ya Balozi wake (hayupo pichani). 

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Rwanda nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Sagore Kayihura. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2014.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Kayihura mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb.)-kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Rais Kikwete na Balozi Kayihura (hawapo pichani)
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kayihura pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Rwanda hapa nchini.
Balaozi Kayihura akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kayihura akisikiliza wimbo wa taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma (kulia), Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki pamoja na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.

Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Kulwa ikipiga wimbo wa taifa kwa heshima ya Balozi Kayihura wa Rwanda nchini (hayupo pichani)

Balozi Marmo awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Romania

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anawakilisha pia nchini Romania, Mhe. Philip Marmo (kulia) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Romania, Mhe. Traian Basescu tarehe 02 Septemba 2014.

Mhe. Marmo (kushoto) katika picha ya pamoja na Rais wa Romania, Mhe. Basescu.

Tuesday, September 9, 2014

AU EXECUTIVE COUNCIL MEETS IN ADDIS ABABA ON EBOLA OUTBREAK

Minister of Health, Hon. Dr. Seif Rashid (MP) led the Tanzania Delegation in an emergency meeting of The Executive Council of the African Union on Ebola Outbreak held in Addis Ababa, Ethiopia, 8th September, 2014. Behind Hon. Rashid is Hon. Dr. Mahadhi Juma Maalim (MP), Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation and H.E. Naimi Aziz, Ambassador of Tanzania to Ethiopia. The Meeting which is being convened following unprecedented spread of Ebola  is expected to consider the outbreak of the disease, with a view to developing a common understanding of the epidemic and  collective approach so as to effectively contain its spread. 
Hon. Mahadhi and Ambassador Naimi listening to ongoing discussions during an emergency meetingon Ebola outbreak held in Addis Ababa.

Monday, September 8, 2014

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi wapya wa Rwanda na Norway hapa nchini



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Eugene Sayore Kayihura. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofinini kwa Mhe. Membe tarehe 08 Septemba, 2014.
Waziri Membe akizungumza na Balozi Kayihura mara baada ya kuwasilisha Nakala za hati za utambulisho. Katika mazungumzo hayo Mhe. Membe alimhakikishia ushirikiano Balozi huyo na kumwomba awe huru katika kutekeleza majukumu yake ya kazi wakati wote akiwa hapa nchini.
Balozi Kayihura akiwa na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi wa Rwanda hapa nchini aliofutana  nao. Katikati ni  Bw. Sano Lambert na  Bw. Ernest Bugingo.
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Kayihura wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kayihura.


.................Mhe. Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway hapa nchini, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad. Hafla hiyo ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Waziri tarehe 08 Septemba, 2014.
Mhe. Membe akizungumza na Balozi Kaarstad mara baada ya kupokea Nakala za hati za utambulisho za Balozi huyo

Balozi Kaarstad na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani)
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kaarstad.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 10 Septemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.


Katika ziara hiyo nchini, Mhe. Museveni atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam. Rais Museveni ataondoka baadaye siku hiyo hiyo kurejea nyumbani.



IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mratibu Mkazi mpya wa UN nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mratibu Mkazi mpya wa  Umoja wa Matiafa hapa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.  Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe tarehe 08 Septemba, 2014.
Mhe. Membe akizungumza na  Bw. Rodriguez mara baada ya kupokea Hatiza ke za Utambulisho. ambapo alimhakikishia ushirikiano.
Bw. Rodriguez pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) na Bi. Hoyce Temu, Afisa kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Membe akiagana na Bw. Rodriguez mara baada ya mazungumzo yao.

Katibu Mkuu akutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ireland, Bw. Niall Burges mara baada ya kukutana kwa mazungumzo. Bw. alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Bw. Haule na Bw. Burges wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan
Bw. Haule, Bw. Burges na Mhe. Gilsenan wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Idara za Ushirikiano wa Kimataifa na Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto) na Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kulia)

Wednesday, September 3, 2014

Naibu katibu Mkuu ashiriki hafla ya miaka 69 ya Taifa la Vietnam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akisoma hotuba wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba, 2014 na kuhudhuriwa na Mabalozi  wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wageni waalikwa.
Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vo Thanh Nam (kushoto) akiwa na Balozi wa Cuba nchini. Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (wa tatu kushoto) pamoja na Bi. Samira Diria (wa kwanza kulia), Afisa Mambo ya Nje wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam.
Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Zakaria Anshar (kushoto) akiwa na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Vietnam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam.
Sehemu ya Wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza Balozi Gahama akihutubia wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Kaimu Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya akimpongeza Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vo Thanh Nam kwa miaka 69 ya uhuru wa taifa lake.

Picha na Reginald Philip