Wednesday, September 26, 2018

Mabalozi na Watu mbalimbali wamiminika kwenye Balozi za Tanzania kusaini vitabu vya maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere

 Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Lee In-Tae akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Tanzania Abuja, Nigeria kufuatia ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere ambayo imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.                                     
 Balozi wa Jamhuri ya Burundi nchini Italia Mhe. Justine Nisubire akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kufuatia ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere ambayo imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.    
                                 
 Balozi wa Eritrea nchini Italia, Mhe. Fessahafion Pietros akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kufuatia ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere ambayo imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.                                     
Balozi wa Brazil nchini Uholanzi, Mhe. Regina Maria Cordeiro Dunlop akiweka saini kitabu cha Maombolezo kilichofunguliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere ambayo imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.                                                                                        
Balozi wa Rwanda nchini Uholanzi, Mhe. Jean-Pierre Karabaranga akiweka saini kitabu cha Maombolezo kilichofunguliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere ambayo imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Mkuu (Dean ) wa Mabalozi ambaye ni Balozi wa Dominica nchini India, Mhe. Frank Hans Dannenberg Castellanos akisaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa na Ubalozi wa Tanzania kufutia ajali ya Mv. Nyerere iliyosababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali.           

Mkuu (Dean ) wa Mabalozi ambaye ni Balozi wa Dominica nchini India, Mhe. Frank Hans Dannenberg Castellanos akifanya mazungumzo na Mhe. Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini India mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha Maombolezo.

Balozi wa Mali nchini Ufaransa akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018
Balozi wa Morocco nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018

Balozi wa Iraq nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018

Balozi wa Kyrgyzstan nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018

Kiongozi wa Watanzania waishio Qatar naye akisaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar
Balozi wa Cuba nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa  kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018


Balozi mstaafu wa Comoro nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018


Balozi wa Uswisi nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018



Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiwa na Balozi wa Uswisi nchini humo alipofika Ubalozini kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo

Balozi wa Eswatini nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018

Balozi wa Kenya nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018


Balozi wa Afrika Kusini nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa   kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018



Balozi wa Ghana nchini Qatar akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018

Balozi wa Japan nchini Rwanda akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018. Pembeni anayeshuhudia ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu


Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, Balozi Walter Stevens akisaini kitabu cha maombolezo kwenye  Ubalozi wa Tanzania nchini humo kuomboleza vifo vilivyotokana na ajali ya  kuzama kwa kivuko cha M.V Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018

          




Tuesday, September 25, 2018

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA KWA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA NA KIKANDA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA KWA VIONGOZI WA MATAIFA MBALIMBALI NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA NA KIKANDA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kupokea salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi wa mataifa na mashirika mbalimbali ya kikanda na kimataifa kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018 na kusababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali.

Baadhi ya salamu zilizopokelewa zinatoka kwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopo Kisumu, Mheshimiwa Dkt. Ali Said Matano

Salamu zingine zimetoka kwa Waziri wa Nchi wa Uingereza, Mheshimiwa Harriett Baldwin na Ofisi ya Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga.

Viongozi hao wameeleza kusikitishwa kwao na taarifa za vifo vilivyosababishwa na  ajali hiyo na kuwatakia majeruhi kupona haraka.

Sehemu ya nukuu za salamu hizo zinasema “Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa niaba ya Sekretarieti ya SADC na mimi binafsi naomba kwa dhati upokee salamu zetu za pole kwako wewe Mheshimiwa Rais, Serikali, Wananchi wa Tanzania na familia zilizopoteza wapendwa wao. Tunaomboleza na Watanzania na tunaomba Mungu awape nguvu familia zilizoathirika na tukio hilo na roho za marehemu zipate pumziko la amani milele. Ninawaombea majeruhi uponyaji wa haraka” ni sehemu ya nukuu ya salamu kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Stergomena.

Naye Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria Kisumu, Mhe. Dkt. Matano, ametoa pole kwa Watanzania na kukumbusha umuhimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujenga  Kituo cha Uratibu na Uokoaji Majini (MRCC) iliyokubalika ijengwe jijini Mwanza.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dodoma.
25 Septemba, 2018


Monday, September 24, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI NA BALOZI ZA TANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI NA BALOZI ZA TANZANIA NJE YA NCHI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kupokea salamu za rambirambi kutoka kwa marais, mawaziri wakuu wa mataifa mbalimbali duniani kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018 na  kusababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali.

Baadhi ya salamu zilizopokelewa ni pamoja na kutoka kwa Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, Rais wa Urusi, Mheshimiwa Vladmir Putin, Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier, Rais wa Saharawi, Mheshimiwa Brahim Ghali, Mtawala wa Kuwait, Mtukufu Sheikh Sabah Al-Ahmad al Jaber Al-Sabah, Baba Mtakatifu, Papa Francis, Rais wa Italia, Mheshimiwa Sergio Mattarella, Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Finland, Mheshimiwa Sauli Niinistö, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange na Rais wa Jamhuri ya Sudan, Mheshimiwa Omar Hassan Ahmed Al-Bashir.  

Viongozi wengine ni Waziri Mkuu wa Israel, Mheshimiwa Benjamin Netanyahu, na Waziri Mkuu wa Sweden, Mheshimiwa Stefan Löfven.

Viongozi hao wameeleza kusikitishwa kwao na taarifa za vifo vilivyosababishwa na  ajali hiyo na kuwatakia majeruhi kupona haraka.

Sehemu ya nukuu za salamu hizo zinasema “Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nilipokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyosababisha vifo vya watu wengi, majeruhi na wengine kutojulikana walipo. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Kenya naomba upokee na kufikisha salamu zetu za rambirambi kwa wafiwa na wananchi wote wa Tanzania kufuatia ajali hiyo na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka” ni sehemu ya nukuu ya salamu kutoka kwa Mheshimiwa Rais Kenyatta
“Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nilishtushwa na taarifa za ajali hiyo mbaya iliyotokea Mkoani Mwanza. Kwa niaba ya Serikali ya China, wananchi na mimi binafsi natoa pole kwa wafiwa wote na majeruhi” inasema sehemu ya salamu kutoka kwa Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping.
Naye Rais wa Urusi, Mheshimiwa Putin amesema “Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, tafadhali naomba upokee salamu zangu za rambirambi kufuatia ajali iliyotokea. Naomba salamu hizi ziwafikie wafiwa wote na ninawaombea majeruhi wapone haraka”

Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea salamu za rambirambi kutoka kwa balozi mbalimbali zinazowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na mashirika ya kimataifa yaliyopo nchini, ikiwemo ubalozi wa Marekani, ubalozi wa Ufaransa, ubalozi wa Sudan Kusini, Ubalozi wa Falme za Kiarabu (UAE), Serikali ya Brazil, Ubalozi wa Cuba, ubalozi wa Nigeria na salamu kutoka kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Kimataifa nchini.

Wakati huohuo, Wizara imepokea salamu za rambirambi kutoka kwa mabalozi wanaowakilisha Tanzania kwenye nchi mbalimbali. Salamu zilizopokelewa zinatoka kwa mabalozi wote wa Tanzania  katika nchi za Qatar, Ufaransa, Uingereza, Uholanzi, Afrika Kusini, Sweden, Nigeria, Burundi, Uganda, Kenya, Ubelgiji, Zambia, Msumbiji, China, Japan, Brazil, Comoro, Algeria, Sudan,  Canada,

Kadhalika tumepokea salamu kutoka kwenye balozi zetu zilizoko Marekani, Uturuki, Rwanda, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Kuwait, Saudi Arabia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zimbabwe, Malawi, Uswisi, India, Italia, Jamhuri ya Korea, Urusi, Israel, Ethiopia, Ujerumani, Oman na Malaysia.

Baadhi ya nukuu ya salamu za rambirambi za mabalozi hao zinasomeka kama ifuatavyo “Inna Lillah Wainna Illah Rajiuon.  Kwa  niaba  ya  Ubalozi  Abuja  na  Watanzania  waliopo  katika  eneo  letu  la  uwakilishi,  tunatoa  pole  kwa  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  familia  na  Watanzania  kwa  ujumla  kwa  msiba  mkubwa  uliotufika.  Mwenyezi  Mungu  atupe  subira  na  faraja  katika  kipindi  hiki  cha  majonzi  na  aziweke  roho  za  marehemu  mahali  pema  na  majeruhi  wapone  haraka, Amin  Amin,”  ni kauli yake Mheshimiwa Muhidin Ally Mboweto, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Dkt. Wilbroad Slaa anasema “kwa niaba ya wenzangu katika kituo cha Stockholm tunatoa pole za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu na familia zote zilizoguswa na msiba huu mkubwa. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na kuwatia nguvu na ujasiri ndugu wote walioguswa na msiba huu”.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Balozi Modest Mero alisema haya; “Ubalozi wa New York tunatoa pole kwa ajali mbaya ya Meli ya MV Nyerere iliyopelekea wengi kupoteza maisha na wengi kuumia.  Tunawaombea marehemu pumziko la milele na wote waliojeruhiwa wapone haraka.”

Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Mbelwa Kairuki alieleza masikitiko yake kwa kusema kuwa “nasi huku Beijing tunaungana na wenzetu kutoa pole kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Watanzania na wanafamilia walioguswa msiba huu mzito. Mwenyezi Mungu awape nguvu na awajalie moyo wa subira wakati wote mnaposhughulika na msiba huo.

Japan na diaspora yetu tunatoa pole kwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote kwa msiba huu uliotokana na kuzama kwa kivuko. Mungu atupe nguvu wote tuliobaki na awape pumziko la amani wenzetu waliotutangulia. Kwa majeruhi tunawaombea wapone haraka na wavumilie mstuko huu mkubwa katika maisha yao. Marehemu wapumzike kwa amani”. Hizi ni salamu kutoka kwa Mheshimiwa Mathias Chikawe, balozi wa Tanzania nchini Japan.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Abu Dhabi alisema haya; “Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi, tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali ya MV Nyerere.Kwa niaba ya watumishi wote wa Ubalozi, tunatoa mkono wa pole kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Watanzania wenzetu wote kwa msiba huu mkubwa. Mwenyezi Mungu awajaalie marehemu wapumzike mahali pema na awajaalie majeruhi kupona mapema. Amin”.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Dkt. Asha-Rose Migiro akieleza kuguswa na ajali hiyo alitoa kauli hii “Ubalozi wa Tanzania London unajumuika na Watanzania wenzetu kutoa pole kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, familia na ndugu wa wale wote waliopatwa na msiba kutokana na ajali hii. Tunawaombea majeruhi wapone haraka na warejee katika shughuli zao za kujikimu na kulijenga taifa letu”.

Kwa upande mwingine, Wizara imepokea salamu za rambirambi kutoka Baraza la Diaspora wa Tanzania ulimwenguni kote (TDC Global) ambao wameeleza masikitiko makubwa kufuatia ajali hiyo mbaya. Sehemu ya ujumbe wao unasomeka kama ifuatavyo; “TDC Global, kwa masikitiko makubwa, inatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Watanzania wote, ndugu, jamaa na marafiki kwa vifo vilivyotokana na ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya visiwa vya Bugorora na Ukara katika Ziwa Victoria. Kama TDC Global, tunaungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu mzito kwa taifa letu. Pia tunatoa pole kwa majeruhi wote na kuwaombea wapone haraka”.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dodoma.
24 Septemba, 2018


Saturday, September 22, 2018

Ubalozi wa Tanzania nchini India wahitimisha maonesho maalum ya utalii

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bibi Devotha Mdachi akizungumza wakati wa kuhitimisha maonesho maalum ya utalii yaliyofanyika  nchini India kwenye baadhi ya miji mikubwa ya New Delhi, Mumbai, na Ahmedabad. Maonesho hayo ambayo yalifanyika kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India yalilenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo Hifadhi za Taifa za Wanyama kama Ngorongoro, Serengeti, fukwe zilizopo Zanzibar na Mlima Kilimanjaro. Pia wakati wa maonesho hayo Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda alitumia fursa hiyo kutangaza kuanza rasmi kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania mjini Mumbai mwezi Novemba 2018. 
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akizungumza na mmoja wa wadau  kutoka India aliyeshiriki maonesho hayo maalum ya utalii

Afisa kutoka Tanzania akitoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ya India walioshiriki maonesho
ya maalum ya utalii yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania

Wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wakijadili masuala mbalimbali kuhusu sekta hiyo na kubadilishana uzoefu 

Mtaalam kutoka Tanzania akitoa ufafanuzi kwa mdau wa sekta ya utalii wa nchini India

Balozi Luvanda akiwa na mmoja wa wadau walioshiriki maonesho hayo


Friday, September 21, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Mjukuu wa  Malkia wa Uingereza nchini, (Prince William)

Mjukuu wa Malkia wa Uingereza “Prince” William anatarajiwa kufanya ziara nchini kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2018.  Ziara hiyo inakuja kufuatia maombi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanya naye mazungumzo wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uingereza mwezi Aprili 2018.
“Prince” William atakapowasili nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha, atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam; Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.
“Prince” William ni mmoja wa wanaharakati duniani wanaopinga biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na Uingereza imekuwa ikisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na vitendo vya ujangili.
“Prince” William ataondoka nchini tarehe 29 Septemba 2018 kuelekea nchini Kenya.

                                                        -Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 21 Septemba 2018

Thursday, September 20, 2018

Maonesho Maalum ya Utalii yaendelea nchini India

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki maonesho maalum  ya kutangaza vivutio vya utalii na kuanza kwa safari za Air Tanzania nchini India. Maonesho hayo yalifanyika mjini Gujarat. Ubalozi huo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) umeandaa maonesho maalum kwenye miji mbalimbali ya India huku tayari maonesho ya aina hiyo yakiwa yamefanyika mjini New Delhi tarehe 17 Septemba, 2018. Safari za shirika la ndege la Tanzania kupitia ndege yake mpya ya Dreamliner zitaanza safri mjini Mumbai mwezi Novemba, 2018 kwa lengo la kurahisisha usafiri kwa watalii, wafanyabiashara na wanafunzi kutoka India kuja nchini.

Monday, September 17, 2018

Ubalozi wa Tanzania nchini India watangaza kuanza rasmi kwa safari za Air Tanzania nchini humo

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akizungumza wakati wa maonesho maalum ya utalii yaliyofanyika  katika Hoteli ya Roseate, Aerocity jijini New Delhi, India tarehe 17 Septemba, 2018. Mhe. Balozi Luvanda pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kutangaza kuanza rasmi kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania mjini Mumbai mwezi Novemba 2018. maonesho hayo yatafanyika kwenye miji mingine miwili ya India ambayo ni Ahmedabad na Mumbai.
Mhe. Balozi Luvanda akitangaza rasmi kuanza kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania nchini India huku  picha ya Ndege ya Shirika hilo aina ya Dreamliner ikionekana. Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Bi. Devotha  Mdachi ambaye yupo nchini India kushiriki maonesho hayo aliyoshiriki kuandaa anaonekana akichukua kumbukumbu ya tukio hilo
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devotha Mdachi naye akizungumza wakati wa maonesho yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi hiyo.

===============================================================================

Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na Shirika la Ndege Tanzania umeandaa Maonesho Maalum ya Utalii na kutambulisha rasmi kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania zitakazofanyika Mjini Mumbai nchini humo kuanzia mwezi Novemba, 2018.


Maonesho hayo ambayo yatafanyika kwenye miji mikubwa mitatau ya India yaani New Delhi, Ahmedabad na Mumbai yanalenga kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nnchini.

Akizungumza wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Hoteli ya Roseate, Aerocity jijini New Delhi, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda alisema kuwa anaona fahari kubwa kushiriki maonesho hayo muhimu kwa Tanzania na India na alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kuanza wa safari za kwanza za ndege ya shirika la ndege la Tanzania mjini Mumbai. 

Balozi Luvanda alisema kuwa safari za ndege hiyo nchini India ni fahari kubwa kwa Tanzania kutokana na ukweli kwamba nchi hizi mbili zina mahusiano ya kihistoria kwani mbali na kuunganishwa na Bahari ya Hindi, Tanzania na India ni marafiki na zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, utamaduni na mawasiliano ya mtu mmoja mmoja.

Mhe. Balozi Luvanda alisisitiza kuwa, safari za ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania nchini India hususan katika mji wa Mumbai zitaimarisha sekta ya utalii nchini kwa kuongeza idadai ya watalii kutoka nchini humo ambao kwa sasa takribani watalii 40,000 kutoka nchini humo wanatembelea Tanzania kwa mwaka. Pia zitarahisha safari za wanafunzi wa kitanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali vya India ambao idadi yao  imeongezeka na kufikia 2500 kwa mwaka.
“Ninayo furaha kubwa kuwajulisha kuwa shirika letu la ndege yaani Air Tanzania limefufuka. Na kuthibitisha hilo Shirika litaanza safari zake mjini Mumbai mwezi Novemba, 2018. Nawaomba msisite kutumia ndege yetu kwa safari zenu za utalii, biashara hata kwenda kusalimia ndugu zenu waliopo Tanzania na wale waliopo Tanzania kuja kusalimia ndugu huku India” alisisitiza Balozi Luvanda.

Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wageni walioshiriki maonesho hayo ushirikiano, amani na usalama pale watakapokuwa Tanzania na kwamba Tanzania ni chaguo sahihi kwa utalii na wasisite kuja kwa shughuli mbalimbali za manufaa kwa nchi hizi mbili.