Monday, January 7, 2019

Zao la Korosho lapata soko Nchini Algeria

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria, Mhe. Saad Belabed. Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi alieleza kuwa Algeria ipo tayari kununua korosho ya Tanzania. Dkt. Ndumbaro amesema mazungumzo hayo ni moja ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwakomboa kiuchumi Watanzania kwa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nje ya nchi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam. 
Balozi Belabed akiendelea kumwelezea jambo Dkt. Ndumbaro 
Mazungumzo yakiendelea.
Dkt. Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Saad Belabed mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

Dkt. Ndumbaro Apokea Nakala za Hati za Utambulisho

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Brazil, Mhe. Antonia Augusto Cesar leo jijini Dar Es Salaam. Baada ya kupokea hati hizo, Dkt. Ndumbaro alifanya mazungumzo na Balozi Mteule, Mhe. Cesar ambapo aliahidi kuwa Serikali itampa ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, alimweleza vipaumbele vya Serikali ya awamu tano na kuiomba Brazil iunge mkono katika kufanikisha vipaumbele hivyo.

Balozi Mteule Cesar akizungumza jambo mara baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Maafisa ubalozi wa Brazili wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mteule Mhe. Cesar na Dkt. Ndumbaro (hawapo pichani).

Amb. Nassor Present Letters of Credence to the President of Palestine

The Ambassador of Tanzania to Egypt, H.E Issa Suleiman Nassor (R) who is also accredited to the State of Palestine  present his letters of credence to the President of Palestine, H.E Mahmoud Abbas in Cairo Yesterday. H.E  Nassor presented the letters of Credence when President Abbas was in a working visit in Egypt.

Friday, January 4, 2019

Tangazo la Nafasi za Kazi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tangazo la Nafasi za Kazi
Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons- OPCW) imetangaza nafasi za kazi za Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Umma na Afisa wa Masuala ya Umma (Public Affairs Officer P-4 and Public Affairs Officer P-2).  

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania, hususan wanawake kuchangamkia nafasi hizo ambapo mwisho wa kufanya maombi kwa nafasi ya Public Affairs Officer P-4 ni tarehe 24 Januari 2019 na ile ya Public Affairs Officer P-2 ni tarehe 9 Januari 2019.  

Maombi yafanywe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti www.opcw.org ambayo pia ina maelezo zaidi kuhusu nafasi hizo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
4 Januari 2019

Friday, December 21, 2018

Katibu Mkuu akutana na Watumishi wa Wizara

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye kikao cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mnyepe aliwataka Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na uzalendo. Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani)


Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu


Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani)
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe na Watumishi wa Wizara


Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya Watumishi wakiwa kwenye kikao kati yao na Katibu Mkuu


Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia matukio wakati wa kikao kati yao na Katibu Mkuu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mnyepe akiwaonesha Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) nyaraka ambazo ni miongozo wanayotakiwa kuifuata katika utekelezaji wa majukumu yao.
Watumishi wa Wizara kwenye kikao hicho
Watumishi wengine wa Wizara wakiwa kwenye kikao hicho
Kikao kikiendelea
Kikao kikiendelea


Watumishi wa Wizara wakifuatilia kikao kati yao na Katibu Mkuu 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Kikao kikiendelea
Watumishi kutoka Idara na Vitengo mbalimbali wakifuatilia kikao
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao na Katibu Mkuu wa Wizara (hayupo pichani)
Wakurugenzi wa Wizara wakifuatilia kikao kati ya  Katibu Mkuu na Watumishi wa Wizara

Baadhi ya Watumishi wa Wizara wakiwa kwenye kikao

Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara
Watumishi wa Wizara wakifuatilia kikao
Watumishi wa Wizara wakisikiliza maelekezo 
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura akizungumza wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara na Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (kulia)
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Utawala (hayupo pichani) 
Kikao kikiendelea huku Watumishi wa Wizara wakifuatilia kwa makini

Juu na chini ni sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki kikao kati yao na Katibu Mkuu
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe akiagana na Watumishi mara baada ya kumaliza kikao

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha biashara

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakiweka saini taarifa ya mkutano wao ambao ulikuwa unajadili namna ya kuondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kiforodha kati ya Tanzania na Uganda. waliosimama nyuma kushuhudia uwekaji saini huo ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na Uganda uliojadili namna ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara na visivyokuwa vya kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda tarehe 19 Desemba 2018.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
20 Desemba 2018

Wednesday, December 19, 2018

Ujenzi wa Ofisi ya Wizara Ihumwa, Dodoma washika kasi

Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo kwenye Mji wa Kiserikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma. Ujenzi wa Ofisi hizo zinatarajiwa kumalizika ifikapo mwezi mosi mwakani.
Mkandarasi Mkuu wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akielezea maendeleo ya ujenzi huo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo walitembelea eneo hilo
Juu na Chini  sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Mkandarasi Mkuu alipokuwa akiwaelezea maendeleo ya ujenzi huo.
Juu na Chini Wakuu wa Idara na Vitengo wakijionea maendeleo ya ujenzi 









Tanzania na Morocco kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Afya wa Morocco, Mhe. Prof. Anas Doukkali yaliyofanyika jijini New Delhi, India wakati wa Mkutano Maalum wa 4 wa Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika jijini humo hivi karibuni. Pamoja na mambo mengine Mawaziri hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya afya hususan katika kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi na kubadilishana ujuzi.
Mawaziri wakiendelea na mazungumzo huku wajumbe waliofuatana nao kutoka Tanzania na Morocco wakifuatilia mazungumzo hayo
Mhe. Waziri Ummy akiagana na Mhe. Prof Anas mara baada ya mazungumzo yao.
=======================================================
TANZANIA NA MOROCCO KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA AFYA

Mhe.Ummy Mwalimu  amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe.Prof. Anas Doukkali, Waziri wa Afya wa Falme ya Morocco pembezoni mwa Mkutano Maalum wa 4 wa Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika jijini New Delhi hivi karibuni.

Pamoja na mambo mengine, Mawaziri hao walijadili namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Morocco hususan katika Sekta ya Afya ikiwemo uzalishaji wa dawa za binadamu, mafunzo kwa wataalam wa afya, wakiwemo Madaktari, Wauguzi hususan wa idara za wagonjwa mahututi katika Hospitali zote za Mikoa na Wilaya.

Aidha, walijadili namna ya kubadilishana ujuzi wa Wataalam wa Afya kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi, kuimarisha huduma za afya katika kukinga magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) na yanayoambukiza kama vile VVU/UKIMWI pamoja kuimarisha huduma za mama na motto.

Kwa upande wake, Mhe. Ummy aliiomba Serikali ya Morocco kusaidia kujenga Hospitali ya Wazazi (Maternity Hospital) jijini Dodoma ambapo Mhe. Prof. Anas amesema atapeleka ombi hilo kwa Mfalme wa Morocco, Mtukufu Mfalme Mohamed VI.

Katika kuhakikisha makubaliano hayo, yanatekelezwa mapema, wamekubaliana Wizara kuteua Mtumishi Mwandamizi mmoja awe mratibu wa masuala hayo. Pia, wamekubaliana kuwa uandaliwe Mkataba wa Ushirikiano (MoU) ili waweze kusaini makaubaliano hayo na kuanza kuyatekeleza mapema iwezekanavyo.             

Sambamba na hilo, Waziri wa Afya wa Morocco, Mhe. Prof. Anas ameahidi kuitembelea Tanzania mwishoni mwa mwezi Februari, 2019 ili kujionea utoaji wa huduma za afya nchini, ambapo ameahidi kuja na Wataalam wa Wizara yake pamoja na Wawekezaji kutoka Morocco hususan kwenye eneo la viwanda vya dawa.

-Mwisho-