Friday, December 21, 2018

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha biashara

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakiweka saini taarifa ya mkutano wao ambao ulikuwa unajadili namna ya kuondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kiforodha kati ya Tanzania na Uganda. waliosimama nyuma kushuhudia uwekaji saini huo ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na Uganda uliojadili namna ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara na visivyokuwa vya kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda tarehe 19 Desemba 2018.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
20 Desemba 2018

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.