WAZIRI WA
AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA
MAWAZIRI WA AFYA KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO ULIOFANYIKA JIJINI NEW DELHI,
INDIA KUANZIA TAREHE 12-14 DISEMBA, 2018.
Tanzania imeshiriki katika
Mkutano Maalum unaojadili Afya ya Mama na Mtoto unaojulikana kama "4th
Partnership for Maternal,Newborn and Child Health 2018" uliofanyika katika
jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba,2018.
Katika Mkutano
huu,Tanzania imewakilishwa na Mhe.Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mkutano huu ulifunguliwa
na Mhe.Shri Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India tarehe 12 Desemba, 2018. Mkutano
huu unawakutanisha pamoja Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali duniani kwa lengo
la kujadili changamoto zilizopo katika eneo la Afya ya Mama na Mtoto na kuweka mikakati
ya pamoja ya kuzitatua changamoto hizo ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya
ya Mama na Mtoto.
Katika hotuba yake ya ufunguzi,
Waziri Mkuu wa India alieleza mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza vifo vya
mama mjamzito na watoto wachanga kufuatia mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali
ya India na kuzitaka nchi washiriki kuweka mipango thabiti itakayotekelezeka katika
kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Kwa upande wake, Mhe.Ummy
Mwalimu alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kupunguza vifo vya
mama na motto nchini Tanzania ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za afya katika
ngazi za chini kwa kuboresha vituo vya Afya na kuajiri watumishi wapya kwenye maeneo
yenye upungufu. Pia, ameeleza hatua nyingine zinazochuliwa na serikali ni kumlinda
mwanamke kutokana na unyanyasaji wa jinsia ambapo madawati ya jinsia yamezinduliwa
katika majeshi ya polisi na magereza ili kuhakikisha mwanamke analindwa wakati wote.
Kadhalika, Mhe.Ummy ameueleza mkutano huo mikatikati iliyopo nchini ya kuhakikisha uboreshaji
na utoaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto unakuwa endelevu, ambapo aliweka bayana
mipango hiyo ni pamoja na Kuongeza bajeti ya fedha katika sekta ya Afya, kuimarisha
huduma za afya ya Mama na Mtoto kuanzia ngazi ya jamii.
Mipango mingine ni kuimarisha huduma kwa kuboresha
vituo vya afya na kuajiri watumishi wanaohitajika, kutoa elimu ya uzazi wa mpango
kwa walengwa pamoja na kutoa huduma stahiki ili kupunguza na kumlinda motto kutokana
na maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Suala jingine la msingi
zaidi ni kuilinda jamii kwa kutoa elimu ya kutosha kuhusu magonjwa ya saratani hususani
saratani ya mlango wa kizazi ambayo sasa ni tatizo kubwa kwa akina mama duniani
kote.
-Mwisho-
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.