Seneta
wa Kaunti ya Uasin Gishu, Mhe. Profesa Magrate Kamar akifunga Maonesho ya 19 ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Jua Kali/Nguvu Kazi jana yaliyofanyika kwa muda
wa siku kumi katika Kaunti ya Uasin Gishu mjini Endoret Kenya. Kwenye hotuba yake Prof. Kamar aliwataka
wajasiriamali kuongeza mawasiliano miongoni mwao ili kukuza soko la bidhaa zao
ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zimekuwa na viwango bora
Naibu
Katibu wa Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto wa Zanzibar, Bi. Mau Makame Rajab akitoa neno la shukrani
katika sherehe ya kufunga maonesho ya 19 ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya Jua Kali/Nguvu Kazi jana zilizofanyika katika Kaunti ya Uasin
Gishu mjini Eldoret, Kenya.
|
Afisa
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hassan Mnondwa akipokea cheti cha pongezi jana
kwa mchango wake wa kufanikisha kufanyika kwa maonesho ya 19 ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki ya Jua Kali/Nguvu Kazi yaliyofanyika katika kaunti ya Uasin Gishu, Eldoret nchini Kenya
|
|
Afisa
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira, Bi. Sara Daudi akipokea cheti cha
pongezi jana kwa mchango wake wa kufanikisha
kufanyika kwa maonesho ya 19 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Jua Kali/Nguvu
Kazi yaliyofanyika katika kaunti ya Uasin Gishu, Eldoret.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.