Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria, Mhe. Saad Belabed. Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi alieleza kuwa Algeria ipo tayari kununua korosho ya Tanzania. Dkt. Ndumbaro amesema mazungumzo hayo ni moja ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwakomboa kiuchumi Watanzania kwa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nje ya nchi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.