Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Roberto Mengoni. Wawili hao walijadiliana umuhimu wa kuibua maeneo mapya ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Italia hussusan katika sekta ya biashara na uwekezaji. Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo pia kueleza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano za kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.